Lowassa mgeni rasmi harambee Jimbo Katoliki Ifakara

Kwa namna nionavyo mie nadhani ni uamuzi tu wa jeshi la police kufanya escort kwa misafara hiyo kulingana na sababu zao za kiusalama wa mkoa huo kwa wakati husika lkn tofauti na hivyo hata huyo Rais mstaafu mwenyewe huwa hana escort ya Police mbali na ile pikipiki inayo mfungulia njia"
 
Kajichomeka!!sema kweli kajichomeka live?aah!tumezoea sikia watu huchomekwa!wamepanda mombasa raha nini?
 
Naam! Shughuli ya kumsimika Askofu Libena ndo imeisha..baadhi ya viongozi waliopewa nafasi ya kuzungumza wakati wa ibada ni pamoja na rais mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ally Hassan Mwinyi, na waziri mkuu aliyejiuzulu bwana Edward Lowossa. Wakati mzee mwinyi alipokuwa akiingia msafara wake ulikuwa na viongozi kama waziri wa sheria na katiba bi Celina Komboni,waziri wa afya Dr Hadji Mponda,mbunge wa kilombero Abduli Mteketa kwa kutaja wachache. Wakati wakiondoka, msafara ulikuwa na viongozi wawili tu. Mzee mwinyi na EL. Swali ni EL huwa anapewa 'eskoti' ya polisi? Au amedandia msafara wa mzee mwinyi?

Tumfanye Lowassa awe taasisi sasa maana hata akijikuna utasikia "Lowassa katumia mkono wa kushoto badala ya ule wa kuume alipokuwa anajikuna. Mkewe Regina ashuhudia!!"
 
mkuu kuna post humu nimejibu mtu na kumueleza umakini wa kanisa katoliki kwa kila jambo, kama kanisa wangeona EL anatatizo kwa hakika wasingethubutu kumualikana hata siku moja. Viongozi wa kanisa langu huwa hawakurupuki hata siku moja na kama kuna jambo ni lazima walijadili na wakijiridhisha ndio utaona matokeo. Nina imani kubwa sana na kanisa langu na viongozi wake wote pamoja na maamuzi yao pia

Poleni wafuasi wa EL,huyu mtu EL atakuwa mchafu mpaka mwisho wa dahari,hakuna cha viongozi wa kanisa ktk hili na Tumwache Mungu Aitwe Mungu Hakimu wa Mahakimu.Nina hasira na MIFISADI YOTE HATA WANAOSHABIKIA KUNDI LAO.
 
Katika Sherehe za leo Kardinal Pengo ametoa TAMKO kuwa Lowassa hakualikwa kama mgen rasmi ila alialikwa mke wake ambaye ni mkatoliki ndo Lowassa naye akajipenyeza. lakin cha kushangaza kulingana na kardinal ni kuwa baada ya kujipenyeza akapewa nafasi ya kusalimia wananchi ndo akatumia mwanya huo kuonngea mambo ambayo hata kanisa halikutegemea hayaongee kama "Ajira kwa vijana na Mengine mengi". Kinachomshangaza Kardinal ni kuwa Lowassa kaongea kama mgen rasmi wakati alitakiwa asalimie tu. Na pia kardinali ametolea ufafanuzi juu ya kualikwa katika harambe kuwa ni uamuzi wa mtu binafsi sio wa Kanisa Katoliki ifahamike hivyo kwani hata kauli ya Kikwete ni chaguo la Mungu yalikuwa ni matamshi ya mtu mmoja.

Source: redio Maria TZ
 
Niulize tena, mke wa Lowassa ana uhusiano gani na jimbo la Ifakara? Na kama ni mke wake aliyealikwa kwa nini Lowassa apewe nafasi ya kusalimia? Na huu wimbo wa ajira kwa vijana kanisani wa nini? Ukweli hapa Kardinali Pengo amejiingiza kwenye mchezo. Naamini siko peke yangu nikisema kuwa kauli ya Pengo (kama kweli kasema hayo) itawafadhahisha waumini wengi sana. Haya ni masalia ya mtandao wa 2005 na sote tunajua mtandao umekigawa CCM - chama kikongwe, na sasa mtandao (hata kama ni masalia) utaligawa kanisa. I hope I am wrong.
 
Back
Top Bottom