hata mie nimestuka sana genge lote lile tena likiwa na mama lowasa kubebelea pampasi za mil tano kweli?Leo katika taarifa ya habari ya ITV imeoneshwa M/Kiti wa BAWACHA-Taifa Halima Mdee akiwa na Mama Regina Lowassa wametoa shilingi milioni 5 katika Hospitali ya Morogoro.
Hio pesa ni ndogo sana kwa watu ambao wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi walikuwa wakitoa mamilioni ya pesa. Mke wa Lowassa kufunga safari kutoka Monduli hadi Morogoro kwenda kutoa shilingi milioni 5 ni kuonesha mamilioni aliokuwa akiyamwaga Lowassa yameisha?.
Hilo limeshangaza wengi hapa Bumbuli...hata mie nimestuka sana genge lote lile tena likiwa na mama lowasa kubebelea pampasi za mil tano kweli?
sio wiki ni.kila baada ya siku 2Lowassa bado anawaumiza vichwa hawa magamba akifanya jambo moja lina watikisa wote. Huyu mzee bado ni asset ya kuwaangusha hawa magamba. Hayupo madarakani lakini wiki haiishii bila kuona thread inayomhusu
Mimi sina cha kujifunza kwani kama ni kuwafahamu wanasiasa basi nina u-profesa (sio kama wa Kikwete lakini). Mwanasiasa wa kiafrika anaji-behave kulingana na mazingira aliyopo na upepo unavyovuma. Akiona upepo unaovuma ni ''safari za nje kwa wingi'' basi atatetea kuwa zina tija na kusifia kabisa. Akiona upepo unaovuma ni ''kukataza safari za nje'' basi atasifu na kusema kusafiri nje ni uzezeta. Hivyo kwa Lowassa wala sishangai kwani hakuona umuhimu wa tume huru ya uchaguzi wala wizi wa kura alipokuwa CCM lakini mara baada ya kutoka macho yakafumbuka.Kati ya mwaka 2011 hadi 2015 kulikuwa na changizo katika taifa lote, miskitini na makanisani. Katika kila Harambe ilikuwa lazima utasikia Mgeni wa heshima ni Lowassa. Akifika anasema nimechangiwa na marafiki zangu, mwisho anaweka milioni kadha.
Hali hii ilimfanya Lowassa aonekane kama "mtu wa watu". Akavuma nchi zima. Akateka mikoani na wilayani.
Mwaka huu, sijasikia tena akienda kuchangia tena.
Tunajifunza nini juu ya harakati zake?
Ina maana makanisa na miskiti haiitaji tena michango yake?
Nini tofauti ya watoa misaada wa nje na wa ndani?