Lowassa leo kuibua mazito

Lowassa leo kuibua mazito

Status
Not open for further replies.
Siasa za Lowassa na Chadema bwana kama Mchezo wa watoto!
 
Elimu inahitajika sana tena sana maana kuna watu wanajua siasa ni sawa na club za yanga na simba.
Julius aliwamba siasa ni kilimo siasa ni maendeleo lakini watu kama wewe ni shida kwa maendeleo ya Taifa.
CCM walikuwa wanakusanya matokeo pale nyuma ya Shorpers Plaza na Mlimani City haujaona??
Kuhusu wabunge halina hata shaka kwamba mumepora majimbo mengi pamoja na hayo mbona Msigwa alichukua Iringa akiwa na Madiwa watatu tu hilo ulioni?
Mantiki yako hapa sijui ni nini!???
Tatizo lenu ni kwamba mko rahisi sana kujazwa uongo vichwani mwenu na mkauamini!!!!!!!
Empty head!!!!!!
 
Alikuwa kwaajili ya mission maalumu amesha ikamilisha na mbowe atimuliwe Chadema + Lowasa!! Fredrick Sumae yupo wapi????????
 
Atatuambia nini ccwatanzania tumuelewe yeye aende akachunge ng'ombe wake monduli
 
Nani alimuindozi lowasa katika nafasi ya urais? Mbowe!!! Hahahaha....
 
Mkutano ulishafanyika. Nimeona video clip yake. Sasa hebu tukuulize na wewe mbona kwa mfano mwakz 2010 sehemu nyingi unakuta kashinda mbunge wa upinzani lakini madiwani wengi ni ccm? Mfano iringa mjini mbunge wa chadema akiwa na madiwani watatu tu. Hebu tuambie pia hiyo logic yako inafanyaje kazi hapa?

Inategemeana na population ya hizo kata km ni mjini kati ni tofauti na kata za nje ya mji pia inategemeana na muamko wa hiyo kata. Ni sawa na kuzungumzia ushindi wa lowasa majimbo yenye watu 6000 kule zanzibar pemba na jimbo lenye watu 30000 unguja. Hiyo ndo logic
Sasa mikoa ya Mbeya, Mwanza, Singida, Tanga, Morogoro, Kigoma na Tabira ambazo ndo zina watu wengi mgombea ana 26% na only Kilimanjaro na Arusha jamaa akashinda 63% na dar wakagawana almost sawa ukategemea huyu atashinda hiyo ni miujiza.
 
TAARIFA YA MH EDWARD NGOYAI LOWASSA KWA VYOMBO YVA HABARI JUU YA HALI YA KISIASA NCHINI NA MUSTAKABALI WA ZANZIBAR: 15 Nov 2015
Ndugu Waandishi wa Habari na Watanzania wenzangu
Kama nilivyo waambia Viongozi Wakuu wa UKAWA walikaa juzi kutafakari hali ya kisiasa nchini na hususan Zanzibar na matukio yaliyoandamana na Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktober mwaka huu.
Wakuu wa UKAWA kwa kauli moja walikariri tamko lao la kumuunga mkono kwa dhati, Mh. Maalim Seif Sharif Hamad kwa ushindi wake dhahiri na kuitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar imtangaza kuwa Rais wa Zanzibar mara moja. Viongozi wa UKAWA walilaani vikali uamuzi wa ZEC kufuta uchaguzi halali na wakaonya kuwa mbinu mpya za kutaka uchaguzi urudiwe hazikubaliki na zitahatarisha amani na utilivu Zanzibar. Viongozi wa UKAWA walimpongeza Maalim Seif na viongozi wote wa CUF Zanzibar kwa busara na ustahimili wao mkubwa na jitihada zao zinazoendelea kulinda amani na utulivu nchini humo.
Kinyume na Tanzania bara, uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa wazi na wa amani. Vyama vyote vya siasa na hata wawakilishi wa Kimataifa walikiri hivyo mpaka pale ilipobainika kuwa CCM inashindwa. Wakuu wa UKAWA walikataa dhana kuwa uchaguzi ule ule unaodaiwa kufutwa kwa kuwa ulikuwa na mizengwe, ulizaa matokeo halali wa Wawakilishi wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano na ya Urais wa Tanzania lakini batili kwa wajumbe la Baraza la Wawakilishi na Rais wa Zanzibar. Dhana hii haina mantiki yoyote bali ni ubabe wa kisiasa tu.
Haiwezekani chungu kimoja kikapika halali na haramu kwa pamoja. Kwa kigezo cha ZEC kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa batili basi matokeo yake yote ikiwa ni pamoja na yale ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano pia ni batili. Hii ina maana kuwa hata ushindi unao-daiwa na Bwana Magufuli, mbali ya kuwa ni matokeo haramu ya wizi kwa kura za Tanzania bara, pia ni batili kisheria kwani hana ridhaa ya watu wa pande zote mbili za Muungano.
Aidha kwa kauli moja Wakuu wa UKAWA walikubaliana kuwa hali si shwari nchini licha ya ukimya wa Wananchi. Wananchi wanaelewa fika kuwa CCM na Serikali yake wamepora ushindi wao na sasa inaendelea kushinikiza kwa vitisho vya majeshi yenye silaha yanayoranda mitaani ili matokeo ya wizi huo wa waziwazi yakubalike. CCM na serikali yake wanajua kuwa haikubaliki na hata ifanye vipi haiwezi kushinikiza nafsi za Watanzania.
Kama CCM inadai kuwa imeshinda kwa nini ihitaji majeshi, magari ya washa washa na silaha za vita ili wakubalike? CCM ilitayarisha mkakati wa kuhujumu uchaguzi na ndiyo maana ikanunua magari, na vifaa vya vita kwa mabilioni ya fedha ili kuutisha Umma wakati wananchi wanakufa kwa kukosa dawa na huduma hospitalini. Kama CCM inadai imeshinda kwa nini wana hofu kubwa mpaka kuhujumu uhuru wa vyombo yva habari, kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na kutunyima viongozi wa UKAWA hata fursa ya kuwashukuru Wananchi kwa kutuunga mkono katika safari yetu ya kuleta mabadiliko?
Hii ni aibu kwa taifa letu.
Tuna ushahidi wa kutosha kuonyesha jinsi matokeoa ya Uchaguzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano yalivyochakachuliwa na kiasi cha kura zilizoibiwa. Wakati muafaka tutaweka bayana ushahidi huo ili Watanzania wajue kwa nini UKAWA inasema kwa dhati kuwa haitambui matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi na kwa nini haitashirikiana na serikali ya sasa ambayo ni batili kisheria. Kama sheria ingeturuhusu tungekuwa mahakamani kupinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi. Uamuzi huo umetekelezwa tu kwa sababu ya fitna ya sheria mbovu zilizotungwa kuhakikisha kuwa CCM inabaki madarakani milele. Hii lazma tuendelee kuikataa na kuipinga kwa nguvu zetu zote.
UKAWA itaendelea kuwataka Watanzania wakatae matokeo batili ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania Bara na waendelee kuwa watulivu. UKWAWA itaendeleza harakati za kisiasa katika nyanja mbalimbali ili kutekeleza azma ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
Aidha UKAWA itaendelea kudai Katiba ya Wananchi itakayohakikisha kuwa Tanzania inakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Serikali inayowajibika kwa Umma. Ni wazi kuwa uchaguzi mwingine katika mazingira ya sasa na chini ya Katiba ya sasa hauwezi kuzaa matunda tofauti. Bila Katiba mpya ya Wananchi, Tanzania haitakuwa na demokrasia na itaendelea kuwa nchi inayotawaliwa kwa mizengwe na udikteta wa CCM. Asanteni kwa kunisikiliza.
 
Hayo ni mazito ya Lowasa. Poleni mliosubiri. In short huyu kaja kuua chama zindukeni!
 
Sitaki kuamini kama leo ameongea yote hayo Mzee Wa dk tano?au umepakua kwenye tovuti maana ndio zake.
Anyway sio issue wakati nyie mnatoa tamka Ccm wanaongeza jimbo jingine leo la Lulindi.
 
Ni bora tu atoe tamko watu tuingie mstuni tuzichape ili heshima iwepo. Hakuna cha amani bali ni uvumilivu wa woga. Nasema tumechoka, tumechoka, tumechoka. Bora zipigwe tu ! Viongozi wetu watoe go ahead vijana tuingie msitune. ..
 
Wanamtafuta mchawi saa hizi jua limezama. Hawa nyumbu wana matatizo sana huwa hawakumbuki nyuma. Mlaumuni Mbowe na matusi yenu kwa kumkosesha Lowassa urais na sio Lubuva.
 
Ni bora tu atoe tamko watu tuingie mstuni tuzichape ili heshima iwepo. Hakuna cha amani bali ni uvumilivu wa woga. Nasema tumechoka, tumechoka, tumechoka. Bora zipigwe tu ! Viongozi wetu watoe go ahead vijana tuingie msitune. ..

Mil nane tuliompa Mr President tuko ready tutawafata hukohuko msituni tuwamalize kabisa tuondoe hii kansa mapemaaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom