Lowassa kwa sasa anahitaji sala na dua zetu tu

MTANZANIA620

Member
Jun 20, 2023
34
30
Kumeibuka kundi la wanaojinasibisha na kutamba kama Marafiki wa hayati Edward Ngoyai Lowassa wakati huu ambao ameaga dunia wakileta simulizi za kuashiria wakati wa uhai wake alionewa, alidhulumiwa, alitendwa, alisalitiwa na hakupewa nafasi ya kusikilizwa huku mtuhumiwa kwenye hilo ikitajwa CCM na Rais mstaafu Jakaya Kikwete... Baadhi wameenda mbali hata kutaka kutuaminisha ni yeye pekee aliyestahili kuwa Rais wa nchi yetu.

Tunawakumbusha ya kwamba maelezo na mtazamo walionao hauna msaada kwa wakati na nyakati hizi kwani kwa sasa muhimu kwake ni kumuombea sala na dua apumzike kwa amani.

Biblia inasema heri wakimbiliao nyumba za matanga hivyo tuendelee kuiombea familia yake faraja katika kipindi hiki kigumu!

Tuachane na porojo zisizo na tija kwa sasa.

Pumzika kwa Amani Oleiguanani Edward Lowassa.

Sent from my Infinix X678B using JamiiForums mobile app
 
Sala na Dua za kazi gani? Zinaweza kubadilisha chochote kwa sasa?
 
Back
Top Bottom