Lowassa kuwa Mwenyekiti na Sumaye kuwa Katibu Mkuu CHADEMA

Jongwe2

Member
Sep 8, 2015
96
26
Kuna habari za ndani ya CHADEMA kuwa Edward Lowassa atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na Fredrick Sumaye atakuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Mtoa habari hizo nyeti ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu amesema makubaliano hayo yamefikia hatua za mwisho kabla ya kupelekwa kwa wajumbe wengine.

Wachunguzi wa mambo wanaona ni mkakati wa CHADEMA kujiandaa na uchaguzi wa 2020.
 
Lazima iwe hivyo. Mbowe hana shida na Chama tena, kishapiga mkwanja wake ana shida gani tena.?
 
Kuna habari za ndani ya CHADEMA kuwa Edward Lowassa atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na Fredrick Sumaye atakuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Mtoa habari hizo nyeti ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu amesema makubaliano hayo yamefikia hatua za mwisho kabla ya kupelekwa kwa wajumbe wengine.

Wachunguzi wa mambo wanaona ni mkakati wa CHADEMA kuajiandaa na uchaguzi wa 2020.

Kwamba mwenyekiti ni Lowassa si jambo la kushangaa kwani kawaida ukiwa umenunua kampuni lazima uhakikishe unachukua na madaraka katika kampuni ili ulinde maslahi yako. Kuhusu Sumaye ninashindwa kuelewa anakwenda kufanya nini wakati hana maslahi yoyote.

Ikitokea kweli kwamba itakuwa hivyo, nadhani kazi ya Lowassa kuiua Chadema itakuwa imeisha kitakachobaki ni Lowassa kufanya mabadiliko katika CDM ili kweli iwe mikononi mwake.
 
Ndoto safi ya mchana! Mhesh Mbowe apate muda wa kutosha kushiriki mambo ya Kibunge. Anahitajika kiongozi mwenye muda wa kutosha wa kwenda kuimarisha chama mashinani kuongeza demokrasia nchini.
 
CHADEMA kimehama kutoka chama cha demokrasia na maendeleo na sasa ni chama cha mafisadi na walafi
 
Itakuwa ni maajabu ya karne kwa freeman aikael nkurunzinza kuachia uenyekiti! Huyo lowassa kwa sasa kisiasa ni bora mrema
 
Je post hii nayo ina ujira? Lumumba bado malipo yanaendelee kwa post kama hizi?
 
Kuna habari za ndani ya CHADEMA kuwa Edward Lowassa atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na Fredrick Sumaye atakuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Mtoa habari hizo nyeti ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu amesema makubaliano hayo yamefikia hatua za mwisho kabla ya kupelekwa kwa wajumbe wengine.

Wachunguzi wa mambo wanaona ni mkakati wa CHADEMA kuajiandaa na uchaguzi wa 2020.

Is it a matter of fact or opinion?
 
Chadema kitakuwa chama cha Kifisadi, maana manyangumi wote wamekimbilia huko. Hivi wadau kingunge, masha, na mwapachu wako wapi? Au limetimia lile neno Ukawa itageuka Ukiwa. By Nyumbu kigeu geu.
 
Kwamba mwenyekiti ni Lowassa si jambo la kushangaa kwani kawaida ukiwa umenunua kampuni lazima uhakikishe unachukua na madaraka katika kampuni ili ulinde maslahi yako. Kuhusu Sumaye ninashindwa kuelewa anakwenda kufanya nini wakati hana maslahi yoyote.

Ikitokea kweli kwamba itakuwa hivyo, nadhani kazi ya Lowassa kuiua Chadema itakuwa imeisha kitakachobaki ni Lowassa kufanya mabadiliko katika CDM ili kweli iwe mikononi mwake.

Ziara anazoanza Lowasa ni za kujitembeza kwa wanachama wamjue akijiandaa kuwa mwenyekiti wao wa Taifa.Waswahili wanasema Chema Chajiuza kibaya chajitembeza
 
Itakuwa ni maajabu ya karne kwa freeman aikael nkurunzinza kuachia uenyekiti!

Kama ni kweli Lowasa alinunua chama Mbowe lazima afunge virago.Lengo la lowasa kuwa mwenyekiti itakuwa ni kutaka kumiliki chama ili adhibiti ruzuku za CHADEMA arudishe pesa yake aliyonunulia CHama.Kama Alinunua CHADEMA kwa bilioni 10 na ikiwa ruku ya CHADEMA ni bilioni moja kwa mwezi ina maana atakuwa karudisha hizo bilioni 10 kwa miezi kumi tu au mwaka mmoja tu hiyo miaka mingine 4 iliyobaki kabla ya uchaguzi wa 2020 atakuwa kapata bilioni 48 faida.Yaani ukichukua ruzuku ya miaka mitano itakuwa bilioni 60 UKITOA Bilioni 10 alizonunulia chama utapata bilioni 50 Faida kwake akitoa bilioni 10 Kuzuga zuga CHADEMA kama gharama za uendeshaji basi atafutika mfukoni bilioni 40 faida.

Kwa hesabu hizi LOwasa lazima atakuwa anautaka uenyekiti kwa udi na uvumba arudishe pesa yake na atengeneze faida kwenye hilo deal aliloingia nalo CHADEMA.Plan A ilikuwa kugombea uraisi Plan B kupiga hela CHADEMA na kuwafisadi.

CHADEMA wameliwa.Mumechuka wapiga deal lazima Richmond ingine ifumuke huko
 
Ziara anazoanza Lowasa ni za kujitembeza kwa wanachama wamjue akijiandaa kuwa mwenyekiti wao wa Taifa.Waswahili wanasema Chema Chajiuza kibaya chajitembeza

Ziara zimeahirishwa mpaka baadae, ila ndiyo maandalizi ya kuwa chairman
 
Back
Top Bottom