Lowassa kukaangwa kama Yesu!

Hatma ya CCM ni uwamuzi wao katika uteuzi wa mgombea urais wakikosea tu UKAWA wanachukua nchi kilaini na hakika mbinu za kuchakachua zitashindwa.Jeuri yao kuwa yote wakamuwea atakubalika si sasa ni Enzi za mwl nyerere pekee
Kuna taarifa kwamba CCM wana mpango wa kurefusha kifungo cha makada waliofungiwa kwa mwaka mmoja zaidi mpaka uchaguzi utakapokwisha lengo kubwa hasa likiwa kumkaanga Lowasa.

Kada maarufu wa CCM ambaye hakutaka kutaja jina lake anayefanya kazi Makao Makuu ya CCM, Dodoma alisema kuwa mpango huo wa kumuangamiza Lowasa umekamilika na hakuna mtu anayeweza kuupindua.

"Si unajua kwamba amehukumiwa pamoja na makada wenzake...hivyo njia nzuri ni kuwafungia wote ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wafuasi wake (Lowasa) na kugawanyika kwa chama. Unajua huyu mtu ana wafuasi wengi sana hivyo tukimfungia ovyo anaweza kukigawa chama chetu". Alisema.

KAMA YESU?
Wakristo mnakumbuka wakati mtoto Yesu alipozaliwa, mafarisayo waliwaua watoto wote wa kiume lakini target yao hasa ilikuwa ni kumuua Yesu. Naona CCM wameamua kukopa mbinu hiyo kwa kum-target Lowasa. Hili ni jambo la ajabu sana.

MAONI YANGU
CCM mnajaribu kuliziba jua kwa kutumia ungo lakini mjiandae vizuri kwa madhara yatakayotokea. Lowasa hazuiliki.

:israel:
 
Hatma ya CCM ni uwamuzi wao katika uteuzi wa mgombea urais anayekubalika wakikosea tu UKAWA wanachukua nchi kilaini na hakika mbinu za kuchakachua zitashindwa.Jeuri yao kuwa yeyote watakayemuweka atakubalika si sasa ni Enzi za mwl nyerere pekee
 
Nadhani ifikie hatua tuheshimu imani za watu, huwezi kumfananisha Lowassa na Yesu Kristo, kwa context ipi? Mtaje muhammad basi
 
CCM jiandaeni kumkubali Lowasa...huyu ni mwali wenu, mnapaswa kumkubali jinsi alivyo na hakuna jinsi ya kumuepuka. Kwanini mnawekea mikingamo ya ovyo ovyo? Nyota ya mtu iking'ara hakuna awezaye kuizima isipokuwa Mungu tu. Kwani CCM mmekuwa Mungu hadi mumzibie njia Laigwanan Lowasa? Acheni hizo figisufigisu zenu.

Rais ajae hawezi toka kaskazini! Prince riz moko.
 
Wamkaange, wamchemshe watajua wenyewe sisi tunachotaka October 2015 waondoke watuachie UKAWA ile nyumba yetu ya magogoni
 
CCM jiandaeni kumkubali Lowasa...huyu ni mwali wenu, mnapaswa kumkubali jinsi alivyo na hakuna jinsi ya kumuepuka. Kwanini mnawekea mikingamo ya ovyo ovyo? Nyota ya mtu iking'ara hakuna awezaye kuizima isipokuwa Mungu tu. Kwani CCM mmekuwa Mungu hadi mumzibie njia Laigwanan Lowasa? Acheni hizo figisufigisu zenu.
Gamba haling'oki hilo mpaka litue magogoni.
 
Tafadhali usitumie hilo jina Yesu .Show some respect tpaul
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom