CHADEMA: Rais Magufuli mfuate Lowassa akushauri juu ya tatizo la sukari

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,488
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimemtaka Raisi wa Jamhuri ya Muungano John Pombe Magufuli amfuate Lowasa ampe mbinu za kumaliza tatizo la sukari.

===============

Monduli. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Rais John Magufuli kuweka siasa kando na kuomba ushauri kwa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ili kutatua tatizo la kuadimika kwa sukari.

Kauli hiyo ilitolewa na naibu katibu mkuu wa Chadema, Salim Mwalimu juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Moto wilayani hapa Mkoa wa Arusha ambako Lowassa alizungumza na wananchi

kuwashukuru kwa kumpigia kura na akatangaza mpango wa kuzunguka nchi nzima kwa lengo hilo.

Tangu Rais atangaze kudhibiti uagizaji sukari kutoka nje na baadaye Bodi ya Sukari kutangaza bei elekezi, bidhaa hiyo muhimu imepanda bei kutoka Sh1,800 hadi kufikia Sh5,000 kwa kilo na kwa sasa imeadimika madukani, wakati Serikali ikisaka wafanyabiashara inaowatuhumu kuwa wameificha kwenye maghala kwa lengo la kuihujumu.

Akizungumza kabla ya kumruhusu Lowassa kuongea na wananchi hao, Mwalimu alisema inaonekana tatizo la sukari linaelekea kuishinda Serikali na hivyo inahitaji msaada wa ushauri.

“Tatizo la sukari kalianzisha yeye mwenyewe Magufuli na sasa anashindwa kulitatua,” alisema Mwalimu na kuongeza:

“Mtu pekee atakayemsaidia ni Lowassa. Huyu alijipanga na alijiandaa kuongoza nchi.”

Mwalimu alisema Lowassa amevumilia mengi kwa kuwa amenyanyaswa, ameonewa na kusimangwa lakini hakujibu.

“Amepitia kipimo cha mwisho cha utu, ni cha mwisho. Walimuonea mchana kweupe akavumilia. Walimsimanga mchana kweupe mpaka watoto wadogo walikuwa wakimuona Lowassa kama vile saizi yao, akavumilia,” alisema Mwalimu.

“Ninajua vijana waliumia, mzee. Lakini leo warudi nyuma wafikirie maisha yao. Ni nani angetoka nyumbani kwa kauli moja ya Lowassa, kumshika mtoto wake mkono kumpeleka shule kama Lowassa angeangalia ushetani na kumuacha Mungu,” alisema akirejea kauli ya Lowassa kuwa alikuwa akipigiwa simu na watu kumtaka atoe kauli baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana kutangazwa, lakini akaawaambia watulie.

Lowassa, ambaye aligombea urais kwa tiketi ya Chadema baada ya kuenguliwa CCM, alishika nafasi ya pili kwenye mbio hizo akipata kura milioni 6.07 idadi ambayo ni rekodi kwa mgombea wa upinzani tangu siasa za ushindani zirejeshwe mwaka 1992. Magufuli aliibuka mshindi kwa kupata kura milioni 8.8.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Lowassa aliwataka wananchi kuendelea kutulia, akisema mwaka 2020 hauko mbali na Chadema inaendelea kujipanga upya ili kuhakikisha inashika dola na kuondoa kero zao.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Chadema kutoka makao makuu, mkoa pamoja na makada waliojiunga wakitokea CCM wa wilaya ya Monduli, Lowassa alisema wafuasi wa ukawa wajiandae kwa mikutano hiyo.

Huku akishangiliwa na wananchi hao waliokuwa wakimkatisha kwa kelele za shangwe, Lowassa alisema kwa kushirikiana na viongozi wenzake wamejipanga kufanya ziara ya kuijenga Chadema nchi nzima.

“Nina hakika tumewashika pabaya CCM na tumewaumiza sana. Sasa kwa kushirikiana na viongozi wenzangu tutazunguka nchi nzima tunataka kuiweka Chadema kwenye chama cha siasa na si uanaharakati,” alisema.

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba 25 mwaka jana, Lowassa aliwashukuru wananchi kwa kumpa kura nyingi akisema hata walioiba kura zake wanajua na dunia inajua kuwa alishinda.

“Niliamua kukaa kimya kwani najua ningesema jambo moja nchi yetu ingeangamia. Na vijana kila kona ya nchi walikuwa wakinipigia simu wakidai wanasubiri neno kutoka kwangu,” alisema.

“Sikufurahishwa na kwenda Ikulu kwa mikono iliyojaa damu. Kuna siku nitakwenda Ikulu kwa mikono safi ya Watanzania, nina hakika na rafiki zetu wanajua kabisa kwamba hawakushinda.”

Chanzo: Mwananchi
 
Ni kweli Lowasa na Rostam ni moja ya waagizaji wakuu watatu wa sukari nchini.

Hivyo vibali kubanwa kumewaathiri sana.waagizaji wakuu waliokuwa wanamiliki vibali vya kuagiza sukari ni EL&RAco,Zakaria na MO...kwa taarifa yako biashara hii humpa muagizaji faida ya hadi bilioni 50 kwa mwaka.
 
Kwa nini wanajikomba na kumwabudu sana namna hii huyu jamaa! ndo shida ya chadema hawana discipline. asa lowasa ndo ana leseni za sukari au transporter au supplier?

waandishi mtaua vyama vyetu kwa kureport namna hii, mngetafuta another way of expressing this, utafikiri tape recoder bana. mnaboa
 
Mafisadi ndo wameficha sukari CHADEMA wanajua Na Lowassa anajua watanzania Na dunia inajua
 
Ni kweli Lowasa na Rostam ni moja ya waagizaji wakuu watatu wa sukari nchini.Hivyo vibali kubanwa kumewaathiri sana.waagizaji wakuu waliokuwa wanamiliki vibali vya kuagiza sukari ni EL&RAco,Zakaria na MO...kwa taarifa yako biashara hii humpa muagizaji faida ya hadi bilioni 50 kwa mwaka.
kumbe! Babalao na mafisadi et lije liwakomboe watanzania wakati limeshirikiana na wahindi kuficha sukari! Rositamu arudishwe nchini afilisiwe
 
Yaani Rais amfuate Lowassa..!! Jamani tuwe na heshima kidogo.. Rais sio mwenzako... hii ni kama dharau fulani, muda huu sio kampeni, ni muda ww kupiga kazi...

Heading za newspapers hazijakaa vema..!! Kama zinamshusha Rais sana... mmhh
 
Wengine wakisikia Jina Lowassa wanaishiwa na usingizi. Subirini huo mchamchaka wakuzunguka nchi nzima kukijenga CHADEMA.

CHADEMA no chama kinachokuwa na endeleeni kutapatapa wasioitakia CHADEMA mema.
 
Aende monduli akawasaidie wananchi wake kupata sukari..wasituletee siasa za media hapa
 
Yaani Rais amfuate Lowassa..!! Jamani tuwe na heshima kidogo.. Rais sio mwenzako... hii ni kama dharau fulani, muda huu sio kampeni, ni muda ww kupiga kazi...

Heading za newspapers hazijakaa vema..!! Kama zinamshusha Rais sana... mmhh

Mbona Rais huwafuata hata wazee?
 
Mnabisha nini wakati hakuna sukari.waandishi wanapoandika amuulize Lowasa ni kumchochea rais awe na aibu kuwa kumbe hili swala la sukari lipo.

Tatizo wengine mmezaliwa na pesa kibao ndo mana mnanunua sukari kwa bei yeyote. ukweli kwa sisi wa hali ya chini hatuwezi kununua sukari. upinzani unasaidia mno kwenye uhamasishaji wakisema wawaache CCM tutakoswa hata chunvi na CCM mna bahati uchuguzi mpaka miaka mitano lakini ingelikuwa leo uchaguzi ndo ilikuwa kwicha habari mmewakera sana watu juu ya swala la sukari.
 
Duuh..hii ni kali aisee.amfate Lowassa!hivi mnajua kama Magufuli ni rais au mmepitiwa!ni hivi ngazi aliyofika Magufuli huyo Lowassa hajafika.na inawezekana asifike..sasa mkubwa hawezi kumfuata mdogo.

Lowassa ni mdogo sana kwa Magufuli..
 
Hili la sukari bado tatizo. Jana nimenunua kilo moja kwa shs 3,000 baada ya kuhangaika maduka kadhaa bila mafanikio. Hili la sukari jamaa walichemsha.

Huo ndio ukweli. Kwenye kusifia tutasifia, na kwenye kukosoa tukosoe wazi pia. Viongozi wakuu wamefanya maamuzi ya ovyo ambayo yamesababisha kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi.
 
CHADEMA waanze tu kumwabudu Lowasa Maana wanamuona kama Mungu mtu hivi.
 
Back
Top Bottom