Eng. Y. Bihagaze
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 1,487
- 913
Nduguzetu
Jumapili hii ya tarehe 9-Novemba, kwenye viwanja vya wazi vya Tanganyika packers , eneo la Kawe ndani ya Jiji la Dar-es Salaam ile Helcoptel iliyotajwa sana na vyombo vya habari Itazinduliwa na Mheshimiwa Edward Lowasa aliyekuwa Waziri wetu mkuu. Helcopter Itatua katika viwanja hivi saa nane mchana kwenye eneo maalum ilipo tengewa.
Mbali na Mheshimiwa lowassa pia Maaskofu wakuu zaidi ya 40 Kutoka makanisa ya Kipentekoste nchini watahudhuria. lakini pia Maaskofu wa makanisa ya Lutheran, Englican na Catholic sambamba na masheick kutoka BAKWATA nao watahudhuria uzinduzi huu wa kihistoria.
Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, ambao ndio wamiliki wa helcopter hii limemaliza taratibu nyingi za kusajili hadi kupata ruhusa ya Kuruka zilizochukua miezi Toka ilipo wasili nchini. Mbali na shughuli za kanisa lakini kanisa limeitoa helkopter hii ifanye shughuli za kijamii na ndio lengo mama hasa. shughuli hizi ni pamoja na Uokoaji wakati wa majanga.
helkopter hii aina ya Robinson R44 ambayo kwenye dunia ya vyombo vya angani inaitwa 'TOP-Vision' imeundwa kwa muundo wa kisasa zaidi wenye kioo kikubwa kinacho saidia abiria na rubani kutazama pande zote wawapo ndani. muundo huu unasaidia sana kwenye majanga kama mafuriko au vyombo vinavyozama majini. Chopaa hii ina uwezo wa kunyanyua mzigo unaokaribia tani moja ikiwa na maana inaweza kuwainua watu zaidi ya kumi kwa kamba.
lakini pia Chopaa hii ina uwezo wa kutua juu ya maji na kuendelea na safari zake. ni moja kati ya helcopter ambazo zinapendwa zaidi ulimwenguni kwa sasa. Robinson zimeundwa kwa mtindo wa kuinua pangaboi lake JUU sana kuepusha ajali. Chopaa hili halina makelele mengi wala Vumbi. watu wengi kwenye ulimwengu wa sasa huitumia kwenye sherehe na harusi mbalimbali. viongozi wengi wa siasa huzitumia kwenye kampeni.
baadhi ya watu wanahoji gharama za mafuta, Robinson inatumia kimiminika cha +petrol inayoitwa AV-Gas ambayo kwa lita ni Tsh3,200 tu. kutoka hapa hadi dodoma na kurudi unaweza kutumia mafuta ya 540,000 tu sawa na gari dogo. Robinson R44 inakimbia hadi kilometa 300 kwa saa. ina maana ni dakika 32 kutoka Dar hadi Morogoro.
uzinduzi wa Chopaa hii ni mwangaza mzuri kwa Watanzania. ni chachu kwa kila mmoja apendaye maendeleo kununua mashine zinazoleta faida sana kwa jamii. sisi sote tunakumbuka Ndugu zetu wengi wamemezwa na maji kwa kukosa nyenzo za kuwaokolea. tatizo la helikopter nyingi ni ukosefu wa marubani mahiri "Compitent pilot" Toka kanisa limeweka mawazo ya kuanza Kumiliki vyombo hivi vya angani pia tumeweka nguvu nyingi Kusomesha vijana wetu wenye akili safi nje ya nchi ili wawe marubani wazuri kwenye Ulimwengu wa anga tunao ukaribia. Ni maono ya Mchungaji Kiongozi kuwa na Chuo cha urubani Tanzania ambacho maandalizi yake yameshaanza. lakini pia kanisa limeanza mchakato wa kuagiza ndege ndogo za abiria sita na nane Jet aircraft zenye uwezo wa kukimbia kwa kasi kiasi cha kilometa 1200 kwa saa, kiasi cha kutumia dakika hamsini (50 minutes) kutoka Dar hadi Kigoma.
mbali na hapo kanisa linatarajia kuleta ndege 'cessna aircraft' zenye uwezo wa kuchukua hadi abiria 32, hizi zitafanya huduma za jamii kwa ujumla. Yote haya ni kufanya miji ifikike kwa urahisi na wepesi ili nchi yetu ipige hatua za kasi kwenye maendeleo. Mtu anaweza kutumia Jet Aircraft ndani ya masaa 11 akaitembelea Mikoa Yote Tanzania.
Kanisa linakamilisha ujenzi wa Kiwanja Cha ndege eneo la Kinzudi Salasala na wakaazi wote wa jiji hili la Darisalam na mikoani wanakaribiswa kupata huduma hizi ambazo hapo awali tulikaririshwa kwamba ni za watu wenye pesa nyingi mno kitu ambacho si kweli. Ikumbukwe kanisa halitumii mashine hizi kibiashara. mara nyingi tunaamini Mungu amesababisha tukawa na vyombo hivi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. hivyo shughuli zote za lazima kwa washirika wa kanisa na wananchi zitatolewa bure na kama gharama itakuwepo basi ni ndogo sana kama kuchangia mafuta na si vinginevyo. Ni maono ya mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima kuhakikisha kila tulicho fikiri hakiwezekani sasa kinawezekana tena si kwa gharama ambazo wengi tunaziogopa bali kwa gharama za kila mtu hasa mtanzania wa kawaida kuzimudu.