TAARIFA MUHIMU; Lowassa kuhutubia live usiku huu; Mgombea Urais wa CHADEMA ambaye pia anawakilisha UKAWA, Edward Lowassa atahutubia taifa usiku huu moja kwa moja kupitia Kituo cha Televisheni cha ITV mara baada ya taarifa ya habari. Hii itakuwa Kwa ajili ya Watanzania ambao kutokana muda kuwa mfupi hawakupata fursa ya kusikia hotuba yote aliyopanga kuitoa leo Kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za kitaifa za CHADEMA na UKAWA.