Lowassa kufagiliwa kahama wamruka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa kufagiliwa kahama wamruka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BigMan, Jan 5, 2012.

 1. B

  BigMan JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]magazeti ya mtanzania na majira mnamo januari 02,2012 yalitoka na moja ya story kurasa za ndani kwamba el alishangiliwa sana pale jina lake lilipotajwa katika shairi huko kahama sasa mwenyekiti wa mamalaka ya maji kahama ambapo ndipo sherehe husika zilifanyika na ambaye pia ni katibu mwenezi wa ccm kahama amekanusha katika taarifa ake kwa vyombo vya habari ambayo ni hii ifuaayo:..

  LOWASA HAJAMWAGIWA SIFA KAHAMA BALI SELIKARI YA AWAMU YA TATU NA NNE[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari nchini zinazomweleza waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowasa kuwa amemwagiwa sifa mkoani Shinyanga, ni upotoshaji wa vyombo vya habari ulijaa maslahi binafsi ya baadhi ya waandishi wa habari hizo.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Mimi ni Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Safi na Usafi wa Mazigira Mjini Kahama naitwa Ndugu Marco Mipawa Ng’wanangolelwa, nalazimika kutoa maelezo juu ya kauli hiyo iliyoshamiri kwenye magazeti mbalimbali ya tarehe 02/01/2012.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Ninachofahamu mimi zilisifiwa awamu ya tatu ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyoongozwa na Rais Mkapa, kwa kuthubutu kuanzisha ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka ziwa victoria kuja Kahama; na awamu ya nne inayoongozwa na Rais Kikwete, kwa kupokea kijiti na kukamilisha ujenzi huo na siyo Mh. Lowasa peke yake!”.Ndugu Ng’wanangolelwa alisema.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Kama Mwenyekiti ndiye nilikuwa mwenyeji kwenye sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ofisi za Mamlaka mjini Kahama tarehe29.12.2011; ambazo zilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge (Mb) kama mgeni raism na kwamba wazo la kumtaja Mh. Lowasa tu kwenye ufanikishaji wa mradi huu wa maji ni la mwandishi mwenyewe tu ambaye wala hakuwepo kwenye shughuli hiyo.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Inawezekanaje sisi kumtaja Waziri tu na hali yeye siyo mkuu wa nchi na kumwacha rais?” Ngwanangolelwa alihoji na kuongeza kuwa, hapa ni dhahili kuna ‘wazo binafsi tu la mwandishi wa habari’ ambaye anataka kuwawekea maneno mdomoni wananchi wa Kahama, Shinyanga na kanda ya ziwa kwa ujumla .[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Watu wanatambua mchango wa Mh. Lowasa kwa nafasi zake kama waziri wa maji kwenye awamu ya rais Mkapa, na waziri mkuu kwa rais Kikwete; lakini ilivyokuzwa kwenye magazeti hayo ni ushabiki usio na maana unaolenga kuwalaghai watu waone kama kwamba, ni Mh. Lowasa peke yake tu, ndiye aliyefanikisha zoezi hili wakati ni swala la serikali nzima.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Mimi nilikuwepo kwenye sherehe hizo kama mwenyeji wa naibu waziri wa maji aliyekuwa amealikwa na mamlaka ya maji kama mgeni raimi; alikuwepo Kaimu Mkuu wa Mkoa Mama Masenza, Katibu Tawala wa mkoa na viongozi wote wa wilaya ya Kahama, wakati shairi linasomwa hatukuyasikia haya kwa picha iliyotolewa na mwandihshi huyo[/FONT] [FONT=&quot]Nina imani wote tulilisikia vizuri shairi la Ndugu Nkanjiwa na halikumtaja Lowasa tu bali lilianza na wakuu wa nchi; baada ya hapo liliwataja mawaziri kwa ubeti mmoja tu likisema, nanukuru:- [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot] “Mawaziri walo maji, Hongera usimamizini, Lowasa na Mwandosya, Mradi wanikiwani’ Katibu Mkuu Sayi,Utendaji wa Imani, MAJI SAFI NA SALAMA KUWASA MAMBO SHEGANI.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot] Na hii ndiyo sehemu pekee iliyomtaja Mhe. Lowasa baada ya kuwa wametajwa Mkapa na Kikwete kwenye ubeti uliotangulia. Wewe unahisi hapa kuna nini?. Haya ya Lowassa peke yake yametoka wapi?.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Mimi binafsi nina shahada ya kwanza ya uandishi wa habari kutoka Chuo kikuu cha St Augustin cha Mwanza na nadiriki kusema hashangazwi na jambo hili la kunyambulisha habari ,kwa sabababu anafahamu siku hizi kuna waandishi wa habari za watu na za umma .[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Ninachowaomba tu wana habari wenzangu tujaribu kujitahidi kutumikia umma hata kama tuna shida kupita kiasi [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Labda niwakumbushe sababu ya kutoa ufafanuzi huu,baadhi ya magazeti ya hapa nchini yalitamka kwamba wananchi mkoani shinyanga wamesifia Lowassa kwa kuwapelekea maji na kunukuriwa kwa shairi la Ndugu Marco Nkanjiwa lililoimbwa kwenye sherehe za ufunguzi wa ofisi ya mamlaka ya maji mwishoni mwa mwaka jana mjini Kahama mkoani Shinyanga[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Mmh kuna mtu atashangazwa na uthubutu wa huyu jamaa.
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni! EL ndio anastahili sifa.
   
 4. m

  mams JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hata kama hamkushangilia, bado ni ukweli uliowazi kuwa yeye ndiye aliyethubutu kuvunja mwiko wa matumizi mbadala wa ziwa victoria. Aliandika historia hiyo na bado itaendelea kuwepo.
   
 5. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ukweli upo pale pale lowasa walimfagilia na kumshangilia mno na bahati nzuri na mimi nilikuwepo na nilishangilia. Huyo anayejiita mwenyekiti wa bodi si kweli. Bodi ilishakwisha muda wake tangu tarehe 24.12.2011. Yeye ni katibu mwenezi wa ccm na pia ni diwani aliyekataliwa kwenye uchaguzi wa 2010 na wakazi wa kahama. Hivyo anayosema ni wivu na chuki binafsi au ametuma ku neutralize hali ya hewa
   
 6. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pesa za mafisadi ni hatari sana!!
   
 7. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  kivuli cha EL kitaendelea kutesa sana tunavyozidi kukaribia 2015; yaani mpaka kutajana kwenye mashairi inakuwa such a big deal?
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  bado mbio za kumsafisha braza EL kazi kweli kweli.. :confused:
   
 9. d

  daniel paul Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza huyu anaejiitamwenyekiti wa bodi sio kweli ni diwani mshindwa asiye kuwa na sera anaishi kifisadi tu hapo kahama
   
Loading...