Lowassa kuanza kampeni wiki ijayo

Lowassa kuanza kampeni wiki ijayo

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
Habari za kuaminika kutoka kwa mmoja wa watu walio karibu na Lowassa zimedai kuwa Mbunge huyo wa Monduli, wiki ijayo ataanza rasmi kumpigia kampeni za nguvu mgombea waChama cha Mapinduzi (CCM), Sioi Sumari, mara baada ya kurudi kutoka Ifaraka atakakohudhuria sherehe za kumsimika rasmi askofu wa jimbo jipya la Ifaraka la kanisa Katoliki, Salitarus Libena, Machi 19, mwaka huu.

Imedaiwa kuwa Lowassa ataendesha kampeni akipita kila kata za jimbo la Arumeru Mashariki,katika kile kilichoelezwa ni kuhakikisha kuwa mgombea huyo wa CCM ambaye ameoa mtoto wa mbunge huyo, Pamela Lowassa, anashinda katika uchaguzi huo.

MY TAKE Aangalie asiropoke kama Mkapa.
 
Anaenda tena Ifakara na tulisikia kwamba hatakiwi tena kule???
 
nadhani mh.lowasa atasafisha hali ya hewa hapo arumeru,ambayo imewakuta ccm
 
aangalie asijeakalipuliwa kama Mkapa, mana kuna mwakyembe na mwandosya wanaomuhusu
 
Labda hapa tutapima uwezo wake tena; lakini vile vile kama kwa Mkapa atakaposimama ajue kabisa na yeye ni target vile vile. Swali kubwa ni je CDM inaweza kumshambulia EL au itamuonesha heshima?
 
Mwanasiasa aliye na nguvu na ushawishi mkubwa kwa sasa ndani ya Tanzania hii ni Lowasa! Kajipanga vizuri sana kwenye kila nyanja.
 
Mwanasiasa aliye na nguvu na ushawishi mkubwa kwa sasa ndani ya Tanzania hii ni Lowasa! Kajipanga vizuri sana kwenye kila nyanja.

kama wameru ni waroho wa pesa za kifisadi basi kauli yako ina ukweli maana EL ni sabuni ya roho ya pesa za kifisadi,
 
kama wameru ni waroho wa pesa za kifisadi basi kauli yako ina ukweli maana EL ni sabuni ya roho ya pesa za kifisadi,
Mtabaki na hiyo mentality kuwa Lowasa ni fisadi..
Wameru wanamkubali Lowassa. He is their hero!
 
Chadema hawana ubavu wa kumvaa Lowassa

Hawana ubavu kiaje??
Kwani kampeni ni pesa au sera?
Kwa Arusha Lowasa hana chake huku si km sehemu nyingine arifu....kisiasa Arusha iko next level
 
Back
Top Bottom