Lowassa kapita dirishani kwangu

Lowassa kapita dirishani kwangu

Watu wa Gongolamboto tumefarijika Sana kuona Rais mtarajiwa akipita mtaani kwetu kwenye kila aina ya uchafu akitaka kujua matatizo yetu ya kimaisha yaliyosababishwa na CCM ili ayatatue atakapochaguliwa kuwa rais.Kwa bahati nzuri kapita dirishani kwangu ilinilazimu nitoke nje kwani niliona watu wengi wakiimba LOWASSA!LOWASSA!LOWASSA HAKUNA KAMA WEWE.Lazima nimpatie kura yangu rais huyu.Amekuja kutuona sisi malofa,wapumbavu na vibaka.Wewe ndiyo kiongozi
Halafu mkuu wewe una bakhat kweli mwenzetu, mimi ikitokea tu japo akanipungia ule mkono wake naweza zimia kwa furaha, yaan huyu mzee ana mvuto wa ajabu halafu ukimwangalia unaona kabisa ni mzee wa kimasai aliyetosheka na yupo tiyari kuwasaidie na wengine ili nao watosheke kama yeye, hana roho ya kwa nini yan, anamwagika tu mwaaaaah...

halafu mzee ni photogenic kinoma yan, dah!! kila kigezo mzee anacho, yan kweli Mungu akishakuwekea tick ya YES bhana basi ni YES tu yan.

nitamvizia huyu mzee kwenye kampeni hadi anipungie tu walau mkono wake kwa mbali, najua maisha yangu yatabadilika sana kutoka kwenye ulofa nilionao.
 
uploadfromtaptalk1440446219490.jpg
Wote ndio walewale..kaja ukawa baada ya kukatwa kama asingekatwa angekuwa wapi acha kudanganya wananchi..uyo ana uchu wa madaraka...angehama tangu alivyojiuzulu uwaziri..sio baada ya kukatwa kwani Ukawa hakuna viongozi wanaoweza kuongoza nchi mpaka aje apewe yeye..,,?

Magufuli kila anapopita hawezi kuzomewa. Hata huyo fisadi wako kapita kwenye barabara zilizojengwa na Magufuli
Yaani we simbrisi kabisa!Unaweza nitajia barabara hata moja iliyojengwa na Magufuli?Unajua kama barabara zinajengwa kwa kodi zetu au unaropoka tu?

Kujenga barabara ni moja ya majukumu ya kazi yake na sio "offer" kwa watanzania.
 
Magufuli kila anapopita hawezi kuzomewa. Hata huyo fisadi wako kapita kwenye barabara zilizojengwa na Magufuli

Magufuli anapesa za kujenga bara bara? Anaaminishwa kusimamia badili kauli pesa ya kodi unayolipwa ww ndio ilijenga si yeye
 
Watu wa Gongolamboto tumefarijika Sana kuona Rais mtarajiwa akipita mtaani kwetu kwenye kila aina ya uchafu akitaka kujua matatizo yetu ya kimaisha yaliyosababishwa na CCM ili ayatatue atakapochaguliwa kuwa rais.Kwa bahati nzuri kapita dirishani kwangu ilinilazimu nitoke nje kwani niliona watu wengi wakiimba LOWASSA!LOWASSA!LOWASSA HAKUNA KAMA WEWE.Lazima nimpatie kura yangu rais huyu.Amekuja kutuona sisi malofa,wapumbavu na vibaka.Wewe ndiyo kiongozi
ametua kutoka sayari gani ili leo aje huko sijui wapi kwenu? umasikini unaletwa na uvivu walo si ccm. hao walio na hela wamezitoa wapi? asubuhi upo kijiweni unatia story unafikir ccm itakupa pesa? according to mkapa ww ni........................
 
Wote ndio walewale..kaja ukawa baada ya kukatwa kama asingekatwa angekuwa wapi acha kudanganya wananchi..uyo ana uchu wa madaraka...angehama tangu alivyojiuzulu uwaziri..sio baada ya kukatwa kwani Ukawa hakuna viongozi wanaoweza kuongoza nchi mpaka aje apewe yeye..,,?
atakuambia mbona hamjampeleka mahakamani sijui kutokupelekwa mahakamani ndio kunafuta wizi wake
 
Kweli wewe lofa! kwa mwimbo huo wa una imani na MASAI PORI...... kweli wewe ni ZOBA!
 
Magufuli kila anapopita hawezi kuzomewa. Hata huyo fisadi wako kapita kwenye barabara zilizojengwa na Magufuli

we mpumbavu sana aise... magufuri kajenga au kodi zetu ndo zimejenga
 
wana-mabadiliko bwana!! yaani tunajifanya kama uchaguzi huu tumeelimika hatudanganyiki kuliko chaguzi zote zilizopita ila hali halisi yawezekana tumekua ma "mbumbumbu mzungu wa reli" kuliko chaguzi zote,,, iweje mtu aje kujua shida za "wapumbavu na malofa" eti kuzi ekspiriens fest hendi LEO wakati anatuhitaji tumpigie kura??? au wakifanya chama tawala ndo inakua nongwa?!! mara elfu utawaliwe hata ko. rodani zako kuliko kutawaliwa akili,,, huo ni utumwa mbaya sana kuliko aina nyingine zote za utumwa
 
Watu wa ajabu sana, Lofa na mpumbavu kaamua kutembelea na kuwasalimu wenzake mtaani kelele za wivu kibao kama wake wenza.
Badala watu wawekeze nguvu zao Kule Katavi aliko mzee wa kilometa wao wwnafuatilia Edo kila aendako
 
[h=3]KAMPENI ZA MAGUFULI ZAITIKISA MPANDA[/h]

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mpanda wakati akiwasili kwenye viwanja vya Azimio tayari kwa mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ambapo alihutubia wananchi hao waliojazana kwa wingi.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mpanda mkoani Katavi na kuwaambia wananchi hao kuwa hatokuwa na msamaha kwa watu wasiotimiza majukumu yao.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo pinda akimtambulisha Mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe magufuli kwa wakazi wa Katumba mkoani Katavi.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi Mishamo mkoani Katavi .

Wakazi wa Mishamo Katavi wakionyesha mabango ya kumchagua Magufuli kwenye mkutano wa kampeni.

Wananchi wa Mishamo wakimsikiliza Dk.John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni za CCM mkoani Katavi.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akihutubia wakazi wa Katumba kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM kwa nafasi ya Urais Dk. John Pombe Magufuli.

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Katumba mkoani Katavi.
Umati wa wakazi wa Katumba kwenye jimbo la Nsimbo wakimsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom