Lowassa hujatimiza maono yangu


N

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2008
Messages
255
Likes
7
Points
35
N

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2008
255 7 35
Wanajamvi,
Ilikuwa mnamo mwaka 1992, wakati huo nikiwa kidato cha tatu shule moja Sumbawanga, nikapata habari kuwa waziri anayewapeleka puta wahindi na matapeli wa viwanja Dar, waziri anayeota mvi kabla ya wakati wake sababu ya kuchapa kazi anakuja kutembelea mkoa wa Rukwa.

Basi siku hiyo mnamo kama saa tano nikatembea toka Sumbawanga wenyeji hadi maeneo katika ya chanji na kizwite kwenda kumpokea huyo mheshimiwa, by that nilikuwa kama 14 hivi.

Kulikuwa na watu wengi kidogo hasa viongozi wa serikali nikapenya katikati ya Marehemu mbunge Theonas Kinyonto (alikuwa ananifahamu) Nguvumali nikasogea karibu kabisa na the then mkuu wa mkoa Dr kiwanuka.

Basi ile Lowassa anashuka tu kwenye gari mimi nikawa hatua chache kutoka kwake, kweli kule kumuona nilipata tumaini sana na nikamkubali maana nilikuwa nimesoma sana habari zake nyingi positive kuhusu utendaji wake wa kazi.

Japokuwa nilikuwa siko smart (vumbi la Swanga) halafu mtoto mdogo katikati ya viongozi wa serikali Lowasa alivyoniona alitabasamu na kunishika mkono na kusema '' eeeh hujambo''.

Kufupisha stori tangu siku nilisema siku moja huyu baba atakuja kuwa rais wa nchi hii, nakumbuka nilimueleza hata Kinyonto ambaye nilimzoea sana.

Katika maisha siku zote ambalo huwa nalitaka 98% huwa linakuwa, je lowasa kuwa rais itakuwa lini. Nadhani kwa vile nilipata haya maono siku nyingi natakiwa kufuatilia na kuhakikisha kuwa yanatimia na wajibu huo ni wangu mwwenyewe.

Nawakaribisha wale wote ambao wana maono kama ya kwangu au wanaopenda lowasa awe rais hata kama ni 2015 karibuni sana tutimize ndoto yangu ya miaka 17 iliyopita. Najua yeye hakumbuki labda yule aliyekuwa msaidizi wake maana yeye tuliongea naye kwa kirefu kidogo. Hapa sio mahali pa kuleta Richmond sijui nini Dowans pelekeni kweye thread nyingine, we havee heard enough of those stuff
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Mbona ameshafulia kama unakumbuka baba wa taifa kwa wakati fulani alimwambia aachane na urais yeye aendelee na biashara zake, anyway ngoja tone ndoto yako na mwl ipi itakuwa sahihi.
 
bht

bht

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
10,335
Likes
212
Points
160
bht

bht

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
10,335 212 160
wenye maono wengi mwaka huu wa uchaguzi!!!!
 
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
7,112
Likes
1,331
Points
280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
7,112 1,331 280
Inaelekea maono yako yatakuwa kama ramli ya sheikh Yahya Hussein kuhusu urais na Kikwete. Lowassa amethibitika kuwa ni mwizi wa rasilimali za Taifa akishirikiana na mafisadi wenzie wanaojulikana, kwahiyo urais atakuwaanauona akienda kwenye gwaride za kitaifa wakati rais stahili atakapokuwaanakagua gwaride; watakaompinga Kikwete nao huko ccm kuwania urais pia hawatakufa!!Maono yako toka Sumbawanga na ramli ya sheikh Yahya vyote vitakuwa batili!!
 
Dark City

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Messages
16,277
Likes
296
Points
180
Dark City

Dark City

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2008
16,277 296 180
wenye maono wengi mwaka huu wa uchaguzi!!!!
Ni kweli kwani hata Shekh Yahya hajatokea kimiujiza. Kuna wenye maono ya kweli lakini kuna wale wanaotafuta kazi au ambao wako kazini tayari (wako kwenye payroll wenzio). Nilitegemea kuwa mleta hoja alitakiwa kuangalia probability & odds za kitu anachojaribu kuwasilisha kwa wenzake. Mhh akina Tomaso ngoja tukapate Kahawa kwanza; kwani leo jam ya kwenda Kimara imepumua ili kusherekea mapinduzi ya Zenji!
 
A

AmaniGK

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2008
Messages
1,100
Likes
31
Points
145
A

AmaniGK

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2008
1,100 31 145
Ntambalaswa bana!! yaani umetafuta habari ya kumsafisha Lowasa ukakosa kabisa ukabakia kukumbuka ulivyoambiwa "Eeh hujambo?" mi nilifikiri labda ungetuambia jinsi alivyotetemesha wahindi wakati huo, au ungetueleza ni mambo gani aliyoyazungumza wakati huo mpaka kufikia kuuleta huo mfano wako mrefu ulioweka hapo juu..
 
kkakuona

kkakuona

Member
Joined
Jan 12, 2010
Messages
70
Likes
0
Points
0
kkakuona

kkakuona

Member
Joined Jan 12, 2010
70 0 0
Wanajamvi,
waziri anayewapeleka puta wahindi na matapeli wa viwanja Dar, waziri anayeota mvi kabla ya wakati wake sababu ya kuchapa kazi anakuja kutembelea mkoa wa Rukwa.
mmmmh. labda utueleze wahindi aliochachafya Lowasa ni wepi kwa issue gani.
je Richmond, DAWASCO, TRL, national ID nk nk ndo zilikuwa zinamuotesha mvi siyo. Kwa maslahi ya nani? taifa au mafisadi?
 
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,505
Likes
234
Points
160
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,505 234 160
Tuombe mwenyezi Mungu apishie mbali maono yako hayo. Lowassa kuwa kiongozi wa Tanzania ni disaster.
 
Mponjoli

Mponjoli

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
667
Likes
15
Points
35
Mponjoli

Mponjoli

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
667 15 35
Me umenikumbusha mbali, chanji,kizwite, sumbawanga wenyeji..........

Lowassa kajiharibia mwenyewe,nasikia aliyembomolea masaki kashinda kesi na serikali inatakiwa imlipe Tshs 8 billion
 
M

Marigwe

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
227
Likes
5
Points
35
M

Marigwe

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
227 5 35
Ndugu Ntambaswala
Hapa ninanukuu maelezo ya Mzee Kasori ambaye alikuwa msaidizi wa Baba wa Taifa hadi anafaariki 1999. Angalizo;asiyesikia la mkuu huvunjika mguu. Kama jana (12/01/10) uliangalia mahojiano kati ya Mrema na Star Tv asubuhi utanielewa.
"Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.

Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alonipigia simu na kusema yafuatayo: "Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma". Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema "Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali". Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.

Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa "Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma". Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa "Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa"!

Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa "Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa" kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; "Kawawa sikumwambia hivyo"! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali. Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa "Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam". Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.

Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?. Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema "Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?". Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia "NDIO ALINIAMBIA". Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.

Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa "Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge. Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?". Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!

Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.

Angalia tunavyofanya "total transgression of CCM regulations and ethics." Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri. Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!! Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa."

Bwana Ntambaswala sina tatizo wala ugomvi na maono yako. Wasiwasi wangu ni mustakabali wa Tanzania. Basi. Hebu muulize Magufuli anao ujasiri wa kumnyang'anya Edward ile Ranchi kule Handeni ambayo anaikagua kwa helicopta aliyoinunua siku za karibuni?

 
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
476
Likes
3
Points
35
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
476 3 35
Mi nilishasema, Lowassa hasafishiki hata kwa sabuni za magadi.Ujanja wa aina hiyo wa kuanza kutumia wana member kujisafisha hautfanikiwa, yeye aendelee na biashara zake kama kawaida.Halafu hizo ndoto za mchana tena huko sumbawanga nachelea kusema kwamba ni batili utazisubiri saaana!
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
197
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 197 160
hakuna maona wala nini , huyo Lowassa ni hardworker tatizo tamaa,nakama ikatokea akawa rais huyo jamaa ana visasi, anamarafiki wahovyo hovyo, wezi,wahujumu , walawiti wa uchumi na ustawi wa nnchi hii, baadhi ya marafiki zake ni Karamagi nasikia wanashirikiana baadhi ya biashara, Rostam AZIZ...huyu ni fisadi mkuu, anaurafiki na kina Manji nanasikia anaukaribu na Manji Yusuph maana alikua nyuma yake katika sakata la uuzaji wa yale majengo ya MIFUKO YA JAMII.
lowasa kimeo wa kisiasa hafai-hafai ni mtu wa hatari kabisa, natamani nisiine hiyo siku ambayo lowasa ataapishwa kua Ris wa jamuhuri yetu tukufu.
 
N

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2008
Messages
255
Likes
7
Points
35
N

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2008
255 7 35
Baada ya miaka 17 je maono haya yatatimia? duu na mwenendo huu wa CCM sijui itakuwaje?
 
Horseshoe Arch

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Messages
11,662
Likes
5,559
Points
280
Horseshoe Arch

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2009
11,662 5,559 280
1992 miaka 14,kidato cha tatu...Lowasa...lowasa...lowasa...
 
N

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2008
Messages
255
Likes
7
Points
35
N

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2008
255 7 35
Nimerejea tena kupima kama maono yangu yanaendelea vyema..........Sijui mwelekeo ukoje kwa huyu mheshimiwa?
 
T

tibihika

Member
Joined
Mar 18, 2013
Messages
39
Likes
0
Points
0
T

tibihika

Member
Joined Mar 18, 2013
39 0 0
Wanajamvi,
Ilikuwa mnamo mwaka 1992, wakati huo nikiwa kidato cha tatu shule moja
Sumbawanga, nikapata habari kuwa waziri anayewapeleka puta wahindi na
matapeli wa viwanja Dar, waziri anayeota mvi kabla ya wakati wake sababu
ya kuchapa kazi anakuja kutembelea mkoa wa Rukwa.

Basi siku hiyo mnamo kama saa tano nikatembea toka Sumbawanga wenyeji
hadi maeneo katika ya chanji na kizwite kwenda kumpokea huyo mheshimiwa,
by that nilikuwa kama 14 hivi.

Kulikuwa na watu wengi kidogo hasa viongozi wa serikali nikapenya
katikati ya Marehemu mbunge Theonas Kinyonto (alikuwa ananifahamu)
Nguvumali nikasogea karibu kabisa na the then mkuu wa mkoa Dr
kiwanuka.

Basi ile Lowassa anashuka tu kwenye gari mimi nikawa hatua chache kutoka
kwake, kweli kule kumuona nilipata tumaini sana na nikamkubali maana
nilikuwa nimesoma sana habari zake nyingi positive kuhusu utendaji wake
wa kazi.

Japokuwa nilikuwa siko smart (vumbi la Swanga) halafu mtoto mdogo
katikati ya viongozi wa serikali Lowasa alivyoniona alitabasamu na
kunishika mkono na kusema '' eeeh hujambo''.

Kufupisha stori tangu siku nilisema siku moja huyu baba atakuja kuwa
rais wa nchi hii, nakumbuka nilimueleza hata Kinyonto ambaye nilimzoea
sana.

Katika maisha siku zote ambalo huwa nalitaka 98% huwa linakuwa, je
lowasa kuwa rais itakuwa lini. Nadhani kwa vile nilipata haya maono siku
nyingi natakiwa kufuatilia na kuhakikisha kuwa yanatimia na wajibu huo
ni wangu mwwenyewe.

Nawakaribisha wale wote ambao wana maono kama ya kwangu au wanaopenda
lowasa awe rais hata kama ni 2015 karibuni sana tutimize ndoto yangu ya
miaka 17 iliyopita. Najua yeye hakumbuki labda yule aliyekuwa msaidizi
wake maana yeye tuliongea naye kwa kirefu kidogo. Hapa sio mahali pa
kuleta Richmond sijui nini Dowans pelekeni kweye thread nyingine, we
havee heard enough of those stuff
Sheikh Yahya mwingine hapa.kama Richmond, Dowans haikuhusu si uende Burundi au kwingineko ambako viongozi wao hawana vielement vya ufisadi?hujawahi kuwa na maono yenye neema kwako kuliko kuwa mnajimu wa negative aspects?
 
M

mfwimi

Member
Joined
Sep 28, 2012
Messages
59
Likes
0
Points
0
M

mfwimi

Member
Joined Sep 28, 2012
59 0 0
kwa maana ya utendaji kazi naungana na wewe hajatokea kama yeye hadi sasa, ila kwa maana ya fitina za kisiasa anachafuliwa sana,lakini ndo mtu anayeweza nyoosha nchi hii kwa hapa ilipofika namaanisha Lowassa
 
N

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2008
Messages
255
Likes
7
Points
35
N

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2008
255 7 35
Mhhh kazi kweli kweli. Nataka kubadili mawazo
 
N

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2008
Messages
255
Likes
7
Points
35
N

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2008
255 7 35
Hivi kweli wataka jina lake? Ina maana maono yangu yalikuwa fake? Haiwezekani HE SHALL BE
 

Forum statistics

Threads 1,238,341
Members 475,888
Posts 29,316,743