Mgombea urais kupitia muungano wa UKAWA, Edward Lowassa amewapongeza waislamu kwa kupata MUFTI Mkuu na kuwaomba waislamu wote kumpa ushirikiano kama walivyofanya kwa MUFTI Shaban Bin Simba...
Vile vile amempongeza binafsi MUFTI (mteule) Aboubakar Zuberi kwa kuchaguliwa kwake....
View attachment 286018
Lowasa ndiye kiongozi pekee anayeweza kutuunganisha watanzania wote wa karne hii ya ubepari na ubinafsi. Huyu ndiye mtu atakayerehesha thamani ya maskini mbele ya tajiri kwani amekua mstari wa mbele kuchangia shughuli za maendeleo bila kujali dini au kabila.
Magufuli alitoa mabilioni mfukoni kwake kujenga kanisa la dhehebu lake kule Chato karibu na hoteli yake lakini hajawahi kuchangia hata kisima cha msikiti wa waislam.
Lowasa ameshiriki kwenye harambee ya maendeleo ya dini na madhehebu yote kwa moyo mmoja bila kubagua. Lowasa anapenda dini na madhehebu yote kwa vitendo.
Lowasa anataka dini zote zipate fursa sawa za kimaendeleo ndio maana siku zote ameshirikiana nao.
Kuna viongozi wengine hata wakiitwa kwenye kuchangia maendeleo ya watu wa dini nyingine hawaendi kabisa wanatafuta wawakilishi.
Watanzania tuwe makini sana na CCM kwani ilishatugawa siku nyingi ndio maana haitaki watu wa dini na madhehebu yote wapate fursa sawa za kiuongozi na kimaendeleo.
Lowasa aliomba waumini wenzake wamuombee lakini CCM imepotosha kwa kusema kuwa ni udini.
CCM walifikiri kuwa wanamchafua kumbe ndio wanazudi kutugawa na kujenga chuki miongoni mwetu.
Mwenye akili haambiwi tazama. Wote tulioko kanda ya ziwa tunaona jinsi ssm inavyiratibu siasa za ukabila na udini nyumba kwa nyumba bila kujua kuwa hii nchi sio lazima itawaliwe na magufuli. Siasa hizi za chuki ndizo zinazowafanya SSM wawe waoga wa kutolewa madarakania.