Lowassa hajakurupuka kurudi CCM, namuunga mkono 100%

Bavicha endeleeni kujipa matumaini tu ila kuhama kwa Lowasa Chadema ni pigo kubwa sana kisiasa;

Just imagine mgombea wa nafasi ya Urais kuhamia chama shindani..ni pigo kubwa sana..inaonesha ni kwa namna gani chama kilichohamwa hakina uwezo wa kushika dola.
 
Rose amezndika ukweli mtupu hongera sana , Bila Chadema wamepata bahati nzuri sana lowasa kuondoka mwenyewe kwa hiari na muda ukiwa bado kuelekea uchaguzi mkuu ujao ,hivyo wanachohitaji ni kujipanga tu , Jiwe kalamba dume yaani walikuwa na upinzani mmoja tu mwenge nguvu ccm Mr membe ,kwa kukosa akili na taarifa kuongeza wawili tena Rostam Aziz na Jana Edward Lowasa ,kweli akili ni nywele ,hajui kuwa watakuwa wanamhujumu kimya kimya ,kwani jinsi alivyowananga hawajamsamehe bado .
 
Kama mnasema alifanyiwa uonevu mbona hamkuruhusu kura za maoni halafu mnajiita chama cha demokrasia
 
Mkuu hakuna mtanzania atakayepatika kufanya haya wakati ccm ikiwa bado hai.CCM ya sasa imekusanya the so called politicians and some incompetent individuals-ambao hawawezi fanya kitu kingine nje ya madaraka haya ya kuteuliwa au kujiteua. Mtu mmoja pale Lilongwe aliwahi kuniambia kuna States man/women na kuna politicians

States man/women ana angalia Taifa-Maswali anayojiuliza ni-Tanzania na watanzania waweje after 20,30 years-Hawa madaraka si Muhimu kwao,wao cha muhimu kwao ni nchi-Watu hawa kwa bahati mbaya wapo wachache sana africa na majority hawajihusishi na hizi siasa uchwara na siasa maji taka-ni watu wanaojiheshimu-nadhani Salim Ahmed Salim was among them
Politicians-The Magufuli type-wanafikiria-nashindaje uchaguzi niendelee kuwa madarakani?-mtu wa aina hii hawezi fikiria Tanzania wala watanzania,yeye anafikiria kwanza kulinda madaraka yake
Uko kichwani kwangu 100%.
Africa na hasa Tanzania, tumejikuta ktk dimbwi la tawala za ki dictator, kwa sababu ya ubinafsi wa viongozi wa kiafrica kujiwazia wao badala ya taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Rose Mayemba

Jana tare 1/3/2019 Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzuru kwasababu ya wizi wa mabilioni ya pesa kupitia shirika fake la kufua umeme(DOWANS ) Mhe Edward Lowassa alitangaza kuondoka CHADEMA na kurudi Chama cha mapinduzi ambako aliondoka mwaka 2015 baada ya kuhujumiwa kugombea nafasi ya Urais ndani ya Chama chake

Ikumbukwe kwamba Mhe Edward Lowassa ndiye mwanasiasa pekee aliyeonekana kukubalika ndani na nje ya Chama cha Mapinduzi miaka hiyo huku wajumbe wote wa mkutano Mkuu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wakiamini kwamba ndiye Rais watakayemsimika baada ya swahiba wake Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza muda wake.

Sote tulishuhudia mambo yakienda kinyume pale mjini Dodoma baada ya jina la Mhe Lowassa kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho na Ndugu John Pombe Magufuli kuibuka kidedea.

CCM walimnyang'anya Mhe Lowassa haki yake ya kupigiwa kura huku watanzania wakijionea kwa macho jambo ambalo liliua ndoto yake ya muda mrefu ya kuwa Rais wa nchi hii.

Hapa ndipo ugonjwa wa hamahama ulipozaliwa, wanaccm wengi hawakuridhishwa na hujuma zile za wazi na kuamua kwenda kujiunga na vyama ambavyo vinasimamia misingi ya haki Demokrasia.

Pamoja na wanachama wengi na viongozi mbalimbali kukihama Chama hicho kwa Sababu za uonezi Mhe Edward Lowassa alihama kwasababu aliamini kwamba wananchi walikuwa na imani nae hivyo ndoto yake ya kuwa Rais ingeweza kutimia akiwa popote, hakuamini kabisa kwamba CCM inaweza kumfanya ashindwe kuwa Rais wa nchi hii. Na ukweli ni kwamba CHADEMA hawakufanya makosa kumpitisha Mhe Lowassa wa wakati ule kuwa mgombea kwasababu hakuna asiyejua kwamba yeye ndiye aliyekuwa chaguo la wananchi, Ccm wanajua na Dunia inajua, hakuna aliyekuwa na nguvu ya kumshinda Lowassa.HAKUNA.

Baada ya Mhe Edward Lowassa kupewa ridhaa ya kugombea kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wananchi walimpokea kwa Shangwe kubwa na kumpigia kura za kutosha.Kila alipokwenda vijana kwa wazee walionesha viparata vyao vya kupigia kura kuashiria kwamba walidhamiria kuiondoa CCM madarakani. Kimsingi Mhe Lowassa alishinda uchaguzi 2015. CCM wakishirikiana na jeshi la polisi walipoka ushindi wa Mhe Lowassa, matokeo ya uchaguzi ule nakumbuka yalitangazwa kwa mtutu wa bunduki, polisi walitapakaa kila mahali kuhakikisha hakuna kiumbe kinajaribu kufanya chochote baada ya kutangazwa kwa Matokeo yale. Kimya kilitanda nchi mzima, hakuna aliyeshangilia wala kufurahia Matokeo yale na huo ndio ukawa mwisho wa Mzee wetu EDWARD LOWASSA.

Hakuwa na nguvu tena ya kufanya jambo lolote, alipokea matokeo kwa Shingo upande huku watu wengine wakimtia moyo kwamba atashinda awamu ijayo.

Ikumbukwe pia kwamba Mhe Edward Lowassa alivumilia matusi na kejeli za kila aina wakati wa kampeni zake, wengine walisema ni Mgonjwa, wengine wakasema anajinyea hovyo Kama mtoto huku wengine wakimwita marehemu. Lakini kwasababu lengo lake lilikuwa ni kutimiza ndoto yake ta kuwa Rais alipuuza na kusonga mbele. Kimsingi alidhihakiwa sana.

KWANINI NASEMA LOWASSA AMEFANYA MAAMUZI SAHIHI KURUDI CCM?

Kila nabii na zama zake. Lengo la Mhe Lowassa kuhama Chama ilikuwa ni Urais ambao wananchi walimpa na CCM wakampora. Urais huu ninaousema hapa kwasasa hauko mikononi mwa Mhe Lowassa tena, zama zake zilishapita na hana mvuto tena kama ilivyokuwa wakati wa zama zake.

Zama zako zikishapita zimepita, huwa hazirudi japokuwa Mzee wetu alitaka kulazimisha King(wacheza bao wanajua) akijiaminisha kwamba pengine nafasi yake Bado ipo.

Vijana kwa wazee kwasasa wamebadili pambio wanaimba wimbo mwingine kabisa, kwasasa mtaani kila unapopita unasikia LISSU! LISSU!LISSU hadi kero.

Hakuna namna ya kuzuia haya ili tumsaidie Mzee wetu Lowassa, walewale waliomshangilia na kumtaka sana 2015 wamebadilika wanamshangilia na kumtaka sana Tundu Lissu. Hili CHADEMA haina mamlaka nalo na wala haiwezi kuzuia kelele za watu kumtaja Lissu. Kiufupi hizi ndo zama zake,zikipita watu watakuja na maamuzi mengine tena ambayo sisi binafsi hatuyajui.

Sasa Mzee wetu Lowassa tunataka aendelee kubaki Chadema akisubiri nini?

Kwa wakati tulionao hawezi kuja kuwa Rais tena,sio kwa kubaki Chadema wala sio kwa kurudi CCM. Ndoto yake ya Urais imekwamia hapo.

Hasara alizozikimbia CHADEMA ni kwamba utawala tulionao unawanyanyasa sana wapinzani naye hakuzoea mambo hayo. haoni sababu ya kuendelea kupambana na CCM wakati ndoto yake ya Urais imekufa. Lowassa hakuwahi kuwa na tatizo na CCM yeye shida yake kubwa ilikuwa ni Urais

Haoni faida ya kufilisiwa mali zake na kuweka rehani maisha yake wakati hakuna manufaa tena, kuwa mpinzani inahitaji kujitoa mhanga. Mhe Freeman Mbowe anajeruhiwa kila siku na Serikali ya CCM na hajabadili msimamo kwasababu ndio maisha aliyochagua tangu ameamua kuwa mwanasiasa sio Lowassa. Lowassa alitaka Urais tu na sisi tulimpa kwasababu wananchi walimtaka lakini si mwanaharakati huyu, hawezi kustahimili.

Tumuache Mzee wetu apumzike, amepigania ndoto yake imeshindikana sasa ni wakati wa yeye kupumzika na kuendelea kula mema ya nchi.

Sisi tunasonga mbele, vita hii tutashinda, usiniulize tutashinda lini wewe pambana ukiamini siku na saa isiyo na jina mnara wa Babeli utaangushwa tu.

KIZA NI KINENE KWASABABU ASUBUHI IMEKARIBIA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Lowassa anakubalika ndani ya CCM kwanini mlimkata? Acheni Unafiki Watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi magu angeamua kukomaa nayo jamaa akaonekana ana hatia si ange fia jera ka doto akitoka yy
Angekomaa nayo CCM ingepigwa na gharika na niwengi tu wangeishia huko ndio maana hakuthubutu. Wanalindana na kulinda chama chao kinachowalisha.
 
Lowasa ni kama kondomu ukimjitaji una Tumia then unatupa. Tanzania tuna dhambi kubwa?!
 
Sina hakika kama alikwenda CDM kutafuta urais.Fikiria mbali zaidi.
 
I can't wait for 2020.
Mungu nipe uhai nishuhudie makuu yako.
 
Nilisimamia kura za Chadema Kama wakala niseme tu ukweli Chadema tulishinda kwa wakati huo lowassa alikua mtaji ila kwa leo habali ya mjini ni lisu Mwana wa mgwai
 
Lowassa maisha yake comfortable hana shida na siasa kilichokuwa kinamsumbua ni ndoto tu ya kuwa raisi siku moja na hilo nadhani keshalikubali ni ndoto za alinacha.

Kurudi kwake CCM mi naona ni kama unofficial statement ya kwamba anakwenda ku-retire siasa rasmi; sana sana CCM watamtumia uchaguzi ujao baada ya hapo anazimika kucheza na wajukuu.

Kwa CDM lazima waelewe binadamu tu ambae kakutana na misuko suko kwenye maisha (unfortunately ndio wengi wetu) atakwambia 'never put your fate in someones hands'; itakuwa taasisi ambayo kila siku inakutana na changamoto bado tu awajajifunza uimara wa chama chao sio mtu bali misingi na taratibu (well of course na clever team ya mikakati).

Huku kulia lia ni utoto.
 
Lowasa hakuwahi kuhama ccm ndio maana hakurudisha kadi ila tu chadema walijichanganya kwa tama zao
Na 2020 anakuja mwingine na mzigo wa maana kuwazuga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom