Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

mimi si mpinzani bwana , ntapinga kila kitu na hata kitu changu ninachoamini ukiniunga mkono sintakupongeza ntalalamika umeniibia hiyo ndiyo tanzania zaidi ya uijuavyo
 
Hiyo ndiyo dhamira ya ccm kwa sasa na hili litawezekana pamoja na kuwasaidia wananchi katika ujenzi wa nyumba bora za kisasa chama changu pongezi kwa kuwajali watanzania

Azma hii ya ccm haipo kwenye ilani yao ya uchaguzi, wanalazimika kuifanya kutokana na ubora na maono ya ilani ya chadema maana ndio ilikuwa na haya wanayo ongea leo japo waliyakataa kuwa hayawezekani.

Naamini wanavyozidi kuicheza hii ngoma ya chadema ipo siku watakuja kukubali kuwa hata huduma za afya bure zinawezekana.

Washauri wakikubali mambo kama haya wawe wanakidhi na takwa la kitaaluma kwa ku-acknowledge source kuwa wanayosema yanapatikana kwenye ilani ya chadema ya mwaka 2010 na ukarasa wa 92 mgombea akiwa Dr Slaa. Kukubali mawazo ya wengine ni hekima ya kibusara kufanya vinginevyo ni wizi wa kitaaluma.
 
Kwani lile wingu la kuleta mvua kutoka Thailand alishalileta huko tz?
 

Mkuu achaneni la Lowasa, kuna watanzania wengi wenye vision nzuri na wasio mafisadi!
hiyo ni gear tu ya kusaka urais
 

Umenikumbusha Romnesia theory ambayo obama alikuwa anaipinga unasema kitu tofauti na unachofanya, kutenda na kuamini kutokana na historia yako
 
Na kasema kwa nchi changa kama ya kwetu muhimu kuwa na intersectoral articulation kwa maana ya elimu,kilimo,miundombinu,viwanda kuwepo na direct link baina ya sekta na sekta..lowasa hata akikosa urais lazima tukubali kuwa ana vision na dira.

si vision tu na dira EL ndo anaeiweza hii nchi sikiliza maelezo yake yote yana tija kwa manyonge ila sidhani kwa system ya CCM labda awe peke yake.
 
Lowasa namkubali aje mbele ya umma tu atuambie ukweli tutamwamini na atuahidi serikali ya mseto ili abanane na kina Lisu ndani ya serikali.
 

Mkuu usibabaike na kauli, hawa jamaa ni wazuri kuongea lakini utendaji ni zero!
Hii ni gear tu ya kutafuta kukubalika miongoni mwa wananchi 2015 kama presidential candidate! Janja ya nyani, fisadi ni fisadi, Hakuna fisadi mzuri!
 
Mwanangu Mohamed Mtoi umeniwahi kusema alama za mnafiki. Maana kabla ya kusoma hitimisho la mawazo yako nilihisi kama naona unafiki mtupu. Hata hivyo, Lowassa amechelewa. Kama angekuwa anawapenda watoto wa kitanzania hivyo basi asingeingiza Richmond ukiachia mbali wizi mwingine alioufanya hata kabla ya hapo. Ashindwe na azidi kunyong'onyea hata kuteketea.
 
Channel ten ilipaswa kumhoji EL ilikuwaje 2010 magamba walidhamini matangazo yakupotosha wakati wa campaign za Dr. Slaa kuwa elimu bure haiwezekani? Tena kupitia channel ten hiyo iyo?
 

Hili li EL linaweza sana kuongoza inchi lakini limezidi kuwa lafi !!!
Kama sio hivo mbona mambo yangekua mazuri kitambo ! anyway, tusubiri vya kufikirika !!
 
Natamani sana tuwe na journalists navyombo vya habari vinavyoweza ku-retreave controversial statements za wanasiasa walagai kama magamba.
 
Lowasa bana kama Karume wakiwa ndani hawsemi na hawatendi wakiwa nje ndio utaona wanashikiria bango,pia waongelee na hela za Uswisi na nje kuwa nazo zinaweza kurudi
 
mimi si mpinzani bwana , ntapinga kila kitu na hata kitu changu ninachoamini ukiniunga mkono sintakupongeza ntalalamika umeniibia hiyo ndiyo tanzania zaidi ya uijuavyo

Mkuu.
Weka sawasawa kisu kwenye mfupa! Nani kapinga na leo anakuja kukubali kuwa yanawezekana? Mpinzani ni yupi aliyesema kuwa ina wezekana akapigwa kuwa haiwezekani?

Ngoja nikusaidie kwa kiwango chako cha uelewa.

Chagua herufi ya jibu sahihi kwenye maswali yafuatayo hapa chini.

1. Chama kilicho andika kwenye ilani yake ya 2010 kuwa elimu ya bure inawezekani kuanzia msingi hadi sekondari ni?

A. Chadema
B. CCM
C. CUF

2. Chama kilicho kuwa mstari wa mbele kuwaaminisha wananchi kuwa swali hilo hapo juu (swali la 1) haliwezekani ni.

A. CUF
B. Chadema
C. CCM

Jipange urudi upya mkuu. Uache kufiri kwa kupiga mbizi. "Mbona mna akili za samaki nyie, alaaaa" - Dr Karume.(Kauli ya aliye kuwa raisi wa Zanzibar akiwaambia wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu ya ccm ukumbi wa kizota- Dodoma)
 
Duuuuh kaanza campaign mapema mzee wa Mvi!
 
Natamani sana tuwe na journalists navyombo vya habari vinavyoweza ku-retreave controversial statements za wanasiasa walagai kama magamba.

Mkuu.
Umenena kilicho kwenye kina cha mtima wangu! Ccm wamekuwa kama kinyonga anayejegeuza geuza kutokana na mazingira, waliyo kataa jana kwa kushupaza misuli ya shingo ndiyo wanayakubali leo kwa kulegeza misuli ya kope huku wakiwa wamerembua macho!

Waendelee kushukuru umbumbumbu walio ujenge kwa watanzania wengi hasa wa vijijini, siku wakigeuka na kujua kuwa kudanganywa ni dhambi na dharau kubwa ya ki-utu watalia na kusaga meno.
 

Mkuu Mtoi
Elimu ya bure kwa maana ya bure haiwezekani; labda tu angesema gharama zipunguzwe na kwa wale wanaotaoka kwenye familia zisizo na uwezo serikali iwaekee upendeleo maalumu; ukichunguza kwa undani serikali bado inatoa elimu ya bure ni wangapi katika hao wanaochukua mikopo wanarudisha? Kwa mantiki hiyo sera ya elimu bure bado ipo. Serikali iliweka Bodi ya mikopo ya elimu kuwaridhisha IMF na WB wanajua fika 80% ya wanaochukua mikopo hawana uwezo wa kulipa na wala haitalipwa; kama kweli serikali ingetaka watu wajilipie wenyewe basi ingeachia mabenkina taasisi nyingine za fedha kukopesha; zimetumika hekima za kisiasa tu mkuu elimu bado tunatoa bure; mh. Lowasa ana ajenda binafsi; alikuwa waziri mkuu mbona hakulisema hilo akiwa madarakani? Mwanasiasa wa upinzani anaweza kusema lolote ili mradi tu atafute kura unakumbuka Dr. Slaa alisema akiingia madarakani mfuko wa sementi utakuwa shs. 5000 hivi lilikuingia akilini hilo? Lowasa ni mpinzani ndani ya nafsi yake hana jipya! Nuru ya kisiasa hailazimishwi huachiwa kujangazia yenyewe hawa wanaotaka kulazimisha mambo wana ajenda zao; Labda tu kama anataka kuwa mkweli awaeleze watanzania utajiri huo ghafla kaupata wapi? Tunajua siku Lowasa alipoanza serikalini hadi leo angeanza na hilo kwanza kabla ya kuwadanganya watu!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…