Lowassa: Elimu bure inawezekana Tanzania

Lowassa: Elimu bure inawezekana Tanzania

October 25 wataelewa tu.
it's just a matter of time
lowasa for president.
vote for LOWASSA.
 
Uloi nga mâché68;13922711 said:
Inaonekana wewe umezaliwa miaka ya 2000. Elimu bure mpaka Vyuo Vikuu Sera hiyo haipo popote duniani kwenye Uchumi wa Soko.

Pia hesabu zako zinapotosha kwa kuwa Vyuo na Shule haviendeshwi kwa ADA pekee. Kuna Ruzuku kutoka Serikalini na Vyanzo vingine. Nafikiri uchambuzi wako ni wa mtu aliyezidiwa na VIROBA. Shame![/QUOT

Hapa mwenzio kakuwekea gharama ambazo hubebwa(hulipwa/huchangiwa) na mwanafunzi/Mzazi moja kwa moja ambazo kwa Sera hii ya elimu bure kuanzia chekechea hadi Chuo kikuu, gharama zitabebwa na serikali!!

Sasa wewe unaongelea ruzuku. Tangu lini ruzuku ikawa inachomolewa kwenye mifuko ya wazazi na kupelekwa mashuleni/vyuoni?

Hii haiwezi kuingia huku kwa sababu tangu awali lipo fungu ambalo linatoka moja kwa moja serikalini kwenda kwenye shule/vyuo hivi ambalo hata usipoileta Sera hii lenyewe lipo tu!!

Siku nyingine jifunze kujibizana na watu kwa hoja na si kutumia lugha chafu na ya matusi!!

Kwa nini umwambie mwenzie kanywa viroba? Kwa nini umwambie mwenzio "shame on you?"

Ina maana ungezungumza tu kwa lugha ya kawaida yenye staha usingeeleweka eeh!!??
 
Acha kutokwa na mapovu. Hiyo Ruzuku yenyewe hutolewa kwa kiwango kidogo mpaka mwaka unaisha!. Shule na Vyuo huponea hizo karo za wanafunzi! Sasa wakifuta si itakuwa balaa. Usidanganyike na Siasa Uchwara wewe!
 
Nitapngeza gharama za Ruzuku za serikali.Mwaka 2010 tuliposema inawezekana hadi Sekondari mlikataa tukaleta Hesabu.Nyerere alisomesha watoto wa Kitanzania kwa Kahawa na Katani tu,Leo kuna kuna Dhahabu,Almasi na Gesi imebuliwa.

Kwa mwaka Mmoja tu Sekta ya Madini inapoteza Trilioni 2.5 kwa mujibu wa Ripoti ya IMF na PAC bungeni

Wakati wa Mabadiliko ni Sasa,Mabadiliko nje ya CCM.

Ben Saanane
 
Hujanisoma rafiki, sijakataa umuhimu wa elimu, wala sijalinganisha Tanzania na nchi za dunia ya kwanza, nilichokuwa najaribu kuelezea ni kuwa kwa kuwa nchi yetu ni tegemezi, misaada itakuja na mashariti ya uchangiaji na ushilikishwaji wa wananchi. Na hapo ndo elimu ya bure inatagonga kisiki. Mimi nasapoti elimu ya bure, ila anayeiahidi anatakiwa atupe maelezo ya kutosha juu ya jinsi atakavyo-implement, isije ikawa tunadanganywa.

Miaka ya nyuma tulishawahi kuwa na sera ya elimu bure na matibabu bure. Unafikiri ni nini kilitubadilisha? Ni IMF na WB, waligoma kutoa misaada mpaka nchi iweke utaratibu wa kuchangia. Utetezi wao ni kwamba mtu anajituma zaidi na anaweka thamani zaidi kwa kitu alichokilipia (Hii niliisikia mwenyewe katika moja ya speech ya Vice President mmoja wa WB alipotembelea TZ). Kama bado tunahitaji pesa za IMF na WB ni vigumu kuongelea elimu ya bure.

Na umeongelea swala la watawala kuuwa shule za umma na kupeleka watoto nje; unafikili hili litakomeshwa na elimu ya bure?

mkuu tanzania ikiweza kutumia raslimali zake vizuri hatuhitaji kutegemea misaada yao
 
Elimu bure kwa wote inawezekana.

Mbona tunatumia sana kuliko tunachopata/zalisha/kusanya?

Kama ni kukopa IMF, WB, wana sera zao nasi lazima tuwe na seranzuri zenye kulea utu wetu siyo zinazotweza utu wetu kisa tunataka mikiopo.Mbona sera za ushoga umezikataa? Si mngepata mabilioni? Kama una uwezo wakukopa kwa nini usikopesheke? Ukinyimwa ujue huna vigezo, utakopaje na kutumiavibaya hadi unashindwa kurejesha mkopo? Matumizi sahihi ya mkopo ni nyenzomuhimu kufikia malengo ya kukopa. Issue unatumiaje mkopo?

Unaomba mkopo uongeze mke? Akili hiyo?

Tatizo la Midanganyika siku hizi haitumii hata bongo zao kufikiri,uwezo wa kufikiri kutumia masaburi ni njanga kwa walio wengi aidha awe ananufaika na mfumo au ni uchizi wake na mahaba kwa kile anacho aminishwa!

Haiingii akilini mtu leo una unda serikali kubwa na unaendeleakuteua viongozi na huna uwezo wa kutosheleza mahitaji muhimu ya kijamii.Huhitaji hata elimu ya cheti kujua hilo. Kila kukicha misafara ya makumi kwamaelfu kusafiri nje na mbaya zaidi hakuna la maana wanalo jifunza huko majuu,wakirudi mambo ni yale yale wawe watalaam au wanasiasa. Hii inaishiakutafsiliwa kama ku-justify trip/allowance tu. Na hakuna anaye jali matumizihaya yana matunda gani, ni vipaumbele au siyo vipaumbele vya Taifa etc.

Mmejiuliza serikali ina nunua magari mangapi ya wanasiasa kilabaada ya miaka 5? Mmejiuliza serikali inatumia fedha kiasi gani kila baada yamiaka mitano kunununua magari yakifahali ya wakuu wa vitengo / viongozi umma? Mmeijiuliza Serikali inanunuamaVx ngapi kwa mwaka? Je serikali inatumia gharama (service /maintenance charges)kiasi gani kwa mwaka kwa magari hayo?

Mbaya zaidi tunachopata hatukitumii kwa maslahi ya wananchi wote. Sehemukubwa ya fedha inayokusanywa au hata kukopa hutumika kwa maslahi ya wachache,kwa ufupi kiasi kikubwa ndicho HUPIGWA na kijisehemu kiduchu ndicho huepelekwakwenye halimashauri zenu japo nancho hipiwa vile vile.

Sasa hivi mbunge aliye staafu baada ya miaka mitano ya siasaanapata kiasi gani? Je Mwalimu wa shule ya Msingi aliye fanya kazi kwa mfano miaka 30 katika maisha yake amelipyakiinua mgogo shilingapi ngapi hadi 2015? Sitaki kwenda kwenye details Zaidikwamba kiinua mgongo cha mbunge anaweza kulipa walimu wangapi? Je hiyo ndiyokuagawana keki ya Taifa kwa usawa? Serikali inakopa ili ipate kuwalipawanasiasa na vigogo mishahara/kiinua mgogo kikubwa, akili hiyo?

Serikali ikope na kuwekeza kwenye vitu vinavyo leta tija kwa maendeleoya Taifa. Mmejiuliza katika bajeti ya Serikali kwa mwaka ni asilimia ngapihutengwa kwa ajili ya maendeleo? Je, unategemea nini kama unaweka nguvu kidogo kuendeshagurudumu la maendeleo, utasogea/utapiga hatua? Unatumia zaidi kuliko kuwekaakiba uataendelea?

Ukiwekeza katika elimu utaendelea! Taifa likwekeza katika elimu,litaendelea!
 
jamani haina haja ya kubishana magufuli mwenyewe alishasema nchi hii ni tajiri sana tatizo liko kwenye matumizi.
 
jamani haina haja ya kubishana magufuli mwenyewe alishasema nchi hii ni tajiri sana tatizo liko kwenye matumizi.

maccm yanabisha tu,kwani milioni 50 kwa kila kijiji kama inawezekana kwao kwao kwa nini elimu bure haiwezekani?
Ccm wanawaza kupiga hela kwenye matamasha tu
 
Tukiwa na viongozi makini upo uwezekano wa kutoa elimu bure kwa watanzania na kuwatafutia vibarua ili babdaye wawe wazalishaji wa Taifa katika kulipa kodi.

Ili mtanzania aelewe hili lazima awe na akili ya kutosha vinginevyo kuelewa hili kirahisi ni ngumu na hasa kwa washabiki wa ccm ambao wengi wanakataa kwa kuwa wananufaika na mfumo wa sasa.
 
Haujapigia mishahara ya walimu na waadhiri ambayo ilikuwa inatokana na hizo ada za wanafuzi, kwa mfano tu udsm ina jumla ya wafanyakazi 700 kunawanao chukua hadi mshahara wa million 7 kwa mwezi
 
Swala la kutokuwezekana kwa elimu ya bure halipo kwenye mapato, nchi za ulimwengu wa kwanza zina mapato makubwa sana, lakini elimu siyo bure.

Kwa bajeti zetu zilivyo tegemezi unafikiri nchi za kipepari zitakubali kukupa msaada ili ufanye kitu ambacho wao wanaamini ni kinyume na principles zao? Kwa principle za kibepari ni kwamba mtu huthamini kitu alichokigarimia, ndo maana hata shopping bags (za plastic kwenye supermarkets) serikali za kibepari huwa zilalazimisha ziuzwe ili mtu asiitupe ovyo.

Jambo la muhimu hapa ni kuweka garama wanazomudu watu, na kuweka utaratibu wa kuwasaidia wale wasiokuwa na uwezo kabisa.

Hujanisoma rafiki, sijakataa umuhimu wa elimu, wala sijalinganisha Tanzania na nchi za dunia ya kwanza, nilichokuwa najaribu kuelezea ni kuwa kwa kuwa nchi yetu ni tegemezi, misaada itakuja na mashariti ya uchangiaji na ushilikishwaji wa wananchi. Na hapo ndo elimu ya bure inatagonga kisiki. Mimi nasapoti elimu ya bure, ila anayeiahidi anatakiwa atupe maelezo ya kutosha juu ya jinsi atakavyo-implement, isije ikawa tunadanganywa.

Miaka ya nyuma tulishawahi kuwa na sera ya elimu bure na matibabu bure. Unafikiri ni nini kilitubadilisha? Ni IMF na WB, waligoma kutoa misaada mpaka nchi iweke utaratibu wa kuchangia. Utetezi wao ni kwamba mtu anajituma zaidi na anaweka thamani zaidi kwa kitu alichokilipia (Hii niliisikia mwenyewe katika moja ya speech ya Vice President mmoja wa WB alipotembelea TZ). Kama bado tunahitaji pesa za IMF na WB ni vigumu kuongelea elimu ya bure.

Na umeongelea swala la watawala kuuwa shule za umma na kupeleka watoto nje; unafikili hili litakomeshwa na elimu ya bure?

Nitapngeza gharama za Ruzuku za serikali.Mwaka 2010 tuliposema inawezekana hadi Sekondari mlikataa tukaleta Hesabu.Nyerere alisomesha watoto wa Kitanzania kwa Kahawa na Katani tu,Leo kuna kuna Dhahabu,Almasi na Gesi imebuliwa.

Kwa mwaka Mmoja tu Sekta ya Madini inapoteza Trilioni 2.5 kwa mujibu wa Ripoti ya IMF na PAC bungeni

Wakati wa Mabadiliko ni Sasa,Mabadiliko nje ya CCM.

Ben Saanane

Mkuu TKNL nadhani Ndugu Ben Saanane amejibu hoja yako hapo juu.

Kimsingi elimu ya bure Tanzania inawezekana.

Pesa zipo nyingi sana, tatizo ni kwamba hatuna vipaumbele vyenye mantiki.
 
Last edited by a moderator:
Swala la kutokuwezekana kwa elimu ya bure halipo kwenye mapato, nchi za ulimwengu wa kwanza zina mapato makubwa sana, lakini elimu siyo bure.

Kwa bajeti zetu zilivyo tegemezi unafikiri nchi za kipepari zitakubali kukupa msaada ili ufanye kitu ambacho wao wanaamini ni kinyume na principles zao? Kwa principle za kibepari ni kwamba mtu huthamini kitu alichokigarimia, ndo maana hata shopping bags (za plastic kwenye supermarkets) serikali za kibepari huwa zilalazimisha ziuzwe ili mtu asiitupe ovyo.

Jambo la muhimu hapa ni kuweka garama wanazomudu watu, na kuweka utaratibu wa kuwasaidia wale wasiokuwa na uwezo kabisa.

Hatuzungumzii shopping bags hapa habari ni hiyo analysis kuwa ELIMU bure inawezekana Mkuu
 
Haujapigia mishahara ya walimu na waadhiri ambayo ilikuwa inatokana na hizo ada za wanafuzi, kwa mfano tu udsm ina jumla ya wafanyakazi 700 kunawanao chukua hadi mshahara wa million 7 kwa mwezi

Mkuu hivi idadi ya hao watumishi na wanafunzi zinalingana? Na hapo ameutumia mlima Kilimanjaro hivi akiweka Bandari ya Dar es salaam akiongeza na madini....uwezo wa kujitegemea tunao hebu tuondoe hizo impossibilities
 
Uloi nga mâché68;13922711 said:
Inaonekana wewe umezaliwa miaka ya 2000. Elimu bure mpaka Vyuo Vikuu Sera hiyo haipo popote duniani kwenye Uchumi wa Soko.

Pia hesabu zako zinapotosha kwa kuwa Vyuo na Shule haviendeshwi kwa ADA pekee. Kuna Ruzuku kutoka Serikalini na Vyanzo vingine. Nafikiri uchambuzi wako ni wa mtu aliyezidiwa na VIROBA. Shame!
Haya basi haiwezekani, umefurahi Mkuu? watu wengine huwa mnawaza kutokuweza tu kama sifa vile
 
Lowasa ndio Wa kutuvusha hapa tulipo kuelekea kwenye neema
 
elimu bure inawezekana ila elimu itakayotolewa haita kuwa bora elimu ambayo itatuwezesha kuwa na ushindani ndani ya soko la ajira kwasababu kwasasa elimu mzazi anachangia lakini elimu yetu ni mbovu sasa ikitolewa bure itakuwaje?
 
Tangu Mgombea Urais wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa atangaze Elimu bure, kuna watu wamekuwa wakiona huo kama muujiza. Kwa kifupi zipo njia nyingi sana zinazoweza kufanya Elimu kuwa bure kuanzia Shule ya msingi hadi Chuo Kikuu. Leo ngoja niongelee 'alternative' moja. Kwa mujibu wa TAMISEMI Tanzania ina jumla ya shule za msingi 16,343 zenye wanafunzi 8.3 mil.

Kwa upande wa sekondari shule zimeongezeka kutoka 531 mwaka 2005 hadi 4,576 mwaka 2014. Idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804,056 mwaka huu. Kwa upande wa elimu ya juu, idadi ya vyuo imeongezeka kutoka 26 hadi 54 kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2014 na kufanya idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iongezeke kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 200,986 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Hotuba ya bajeti ya wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014/2015, wanafunzi wa shule za msingi wanakadiriwa kugharamia kiasi cha Sh.10,000/= hadi 15,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa wanafunzi wote wa shule za msingi Tanzania wanahitaji Bilioni 80 waweze kusoma BURE. Shule za Sekondari za Serikali zinakadiriwa kuwa 2,446 zikiwa na jumla ya wanafunzi 1,004,071.

Kati yao wanafunzi 185,652 ni wa Shule za Kulala (Boarding), na wanafunzi 818,419 ni wa shule za kutwa (Day). Wanafunzi wa Shule za kutwa wanalipa ada TZS 20,000 kwa mwaka. So ukichukua 20,000 × 818,000 utapata Bilioni 16.3. Wanafunzi wa shule za Bweni wanalipa ada TZS 70,000/= kwa mwaka. So ukichukua 70,000 × 185,652 utapata Bilioni 11.2. Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu wa vyuo vya Serikal na vya binafsi wapo 200,986.

Kati yao wanafunzi 162,987 wanasoma Course za 'Social Science, Law, Humanities, Education etc' ambao ada zao hazizidi Mil.2 kwa mwaka. So chukua 162,989 × 2000,000/= utapata Bilioni 325. Wanafunzi 37,997 wanasoma course za "Science" kama Engineering, Udaktari etc na ada zao ni zaidi ya Mil.3 kwa mwaka. So hawa watahitaji Bil 113.5 kulipa ada ya mwaka mzima.

Fedha ya kujikimu pamoja na chakula (Meals & Accomodation) inayotolewa kwa sasa ni TZS 7,000 kwa siku kwa mwanafunzi mmoja. Hivyo basi mwanafunzi mmoja anapata Jumla ya Shilingi 1,680,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu ambao ni 200,986 wanahitaji Bil 337. Fedha ya Utafiti (Research), Mafunzo kwa njia ya vitendo (Field) na vitabu (Stationeries) hutolewa jumla ya Shilingi 735,000/= kwa mwaka ambayo hugawanywa kulingana na asilimia ya mkopo ya mwanafunzi.

Hivyo basi wanafunzi wote wanahitaji Bil 147 kwa mwaka. Ukijumlisha gharama zote hapo juu utapata jumla ya Shilingi Bilioni 934 tu. Kwa lugha rahisi ni kuwa ili kila mwanafunzi nchini asome bure kuanzia Elimu ya msingi, sekondari na akifika Chuo Kikuu alipiwe gharama zote bure kwa asilimia 100%, serikali inahitaji kutoa Shilingi Bilioni 934 tu kila mwaka.

Swali, Je hizi Bilioni 934 zinapatikanaje? Ukisoma hotuba ya Bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2014 utagundua kuwa Mlima Kilimanjaro peke yake unachangia karibu Bil.800 kwenye pato la Taifa (Gross National Income of $350 Milion). Kwa lugha Rahisi ni kuwa tunahitaji Mlima Kilimanjaro mmoja tu ili watoto wetu wasome bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu.

Yani tukiamua mapato yote ya Mlima Kilimanjaro tuyapeleke kwenye sekta ya Elimu bila kuchakachua, tutakua na uhakika wa kusoma bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo kikuu. Je hatuwezi? Hapo hatujagusa Mbuga za wanyama, hatujagusa Bandari, Madini, Gesi, Mazao ya misitu, Uvuvi, Kilimo, Viwanda, etc. Tumegusa mlima Kilimanjaro peke yake. Tuwapeni kura zetu UKAWA ili watoto wetu wafaidi matunda ya Uhuru wetu.Chini ya Rais LOWASA

Hili la kusoma bure linawezekana.
 
Kwanini isiwezekane jamani?! Sema hawa viongozi wa Ccm ulafi wao unawasahaulisha kwamba hii ninchi na inawananchi.

Wao wamezaliwa vijijini kamamimi nawenzangu, wakasomeshwa bule mpk hapa walipo. Sasawamesahau wanasema kusoma bule haiwezekani.

Swala lakujiuliza ni je, hiyo serikali ya Mwl. Nyerere na Mzee Mwinyi zilikuwa navyanzogani vya mapato mpk zikaweza kusomesha watoto bule, zikigawa madaftari nakalamu kwa wanafunzi wote nchi nzima. Hivyo vyanzo tuambiwe vilipotelea wapi?
Mimi naamini kwa Neema iliyoko nchi hii watoto wanaweza kusoma bule mpk hata PhD. Tatizo tulilonalo kwasasa nikukosa viongozi wakusimamia lasilimali zetu.

Delete Ccm tuokoe hii nchi.
 
Back
Top Bottom