Lowassa: Elimu bure inawezekana Tanzania

Lowassa: Elimu bure inawezekana Tanzania

LOWASSA na ELIMU YA BURE CHUO KIKUU inawezekana kwa kufanya yafuatayo

Published By (Helly Tasha Jr, 2015).

1. Elimu ya BURE inawezekana kwa kuachana na mbio za MWENGE za kila mwaka zinazogharimu Trillion 1.5 na zaidi

2. Elimu ya bure Inawezekana kwa SERIKALI YA LOWASSA ambayo imepanga kufuta MSAMAHA mirahaba ya KODI YA MADINI inayofikia kiwango cha Trion 4.5 kwa Mwaka ambayo serikali ya CCM imekalia kimya coz ni washirika Wa mikataba hiyo.

3. ELIMU ya bure inawezekana kwa kuongeza suala zima la mawasiliano na uchukuzi ili UTALII uongezeke nchini

4. ELIMU ya bure inawezekana kwa Serikali kuwekeza katka katika VICOBA mijini na vijijin vyenye wastani Wa kuingiza zaid ya trion 1.5 kwa mwaka

5. ELIMU ya bure inawezekana kwa kufuta KODI KAMPUNI KUBWA kama vile Mitandao ya Simu na hotel kubwa like( HOLIDAY TAX) ambapo serikali ya CCM hupoteza zaidi ya billion 950 kila mwaka

6. ELIMU bure chini ya LOWASSA inawezekana kwa Kuharakisha kuendesha kesi mahakamani na kutoweka gerezani kwa muda mrefu MAHABUSU ambao hugharimu zaidi ya billion 690 kila mwaka.

7. ELIMU bure inawezekana kwa kupunguza idadi ya BARAZA LA MAWAZIRI NA MASHANGINGI kama LOWASSA alivyosema awali ambao chini ya serial I hii ya CCM hugharimu zaidi ya bilion 896 kwa mwaka chini ya CCM.

8. ELIMU bure inawezekana kwa kupunguza safari za RAIS kwenda kuomba misaada nje ambazo hugharimu zaid ya bilioni 300 kwa mwaka.

Elimu ya bure inawezekana kwa kukusanya ushuru Wa FORODHA ipasavyo ambapo serikali hupoteza zaidi ya billion 900 kila mwaka.
YOTE 09,

10. ELIMU ya BURE inawezekana kwa kumchagua LOWASSA kuwa RAIS WA TANZANIA 2015-2020

Na kuhusu HOTUBA,kama RAIS NI KUONGEA basi kuanzia Awamu ya kwanza hadi ya nneTANZANIA ingekuwa kama MAREKANI.

LOWASSA ---> MABADILIKO

MABADILIKO NA LOWASSA.

Source: (Joyce Kiria, 2015)

Nyota ya Ufalme iko mabegani mwake, yeye ni mtawala yeye ndiye atakaye chunga Kondoo wa taifa hili, atatangulia nasi tutamfata nyuma hakuna neno wala nguvu chini ya Mbingu ya taifa hili itakayo mwangusha Lowassa, bali yeye ni jiwe lenye nguvu jiwe lililokataliwa na wajenzi, tazama limekuwa jiwe kuu la PEMBENI naye atakaye jaribu kushinda nalo litamwangusha chini na kumsaga TIKI TIKI..... tazama nalimwona aking'aa kama NYOTA.
 
Kwakweli hoja zinaeleweka nadhani vyama vingine vitaiba hoja hizi soon

Ziibe mara ngapi Mkuu wakati tayari gufuli limeshaiba ya kuwalipa wakulima na kutoa pembejeo bure! Ujenzi wa reli ya kati, kufufua general tyres! kazi wanayo!
 
Tatizo la watanzania wameminywa akili na kulazimishwa kufikiri kiCCM CCM .Pale mtu anapokuwa nje ya CCM anapata mwanga mpya na ana unleash potential na kuanza kuwaza na kufanya mambo kwa njia tofauti. Ndio maana watu kutoka CCM wanashindwa kumwelewa Lowassa lakini UKAWA wanamwelewa.
 
Ziibe mara ngapi Mkuu wakati tayari gufuli limeshaiba ya kuwalipa wakulima na kutoa pembejeo bure! Ujenzi wa reli ya kati, kufufua general tyres! kazi wanayo!

Ndio maana kila siku kazi ninkusikiliza Lowassa atasema nini
 
Lowassa ndio maana alikuwa tishio kwa JK
 
Lowassa ndo kila kitu katika kuileta tanzania mpya, swala la kudandia reli ya kati kwa ccm wacha waitumie. Ila kwao tunajua haiwezekani sababu ya wengi wenye makampuni ya usafirishahi kwa njia ya malori, ndo viongozi walioko ccm hawawezi achia mradi uende kwa kasi na ndo waliotumika kuihujumu hii miundombinu kwa maslahi yao.
 
Huku duniani wapo watu wa aina 3.

1. Watu wanaojua kupiga bla bla nyingi alaf matendo/utekelezaji hakuna.

2. Kuna watendaji wazuri. Hawa hawaongei sana ni kazi mwanzo mwisho and often huleta pleasing results i.e. John P. Magufuli.

3. Alaf kuna master architects and strategists, hawa wako fit sanaaa kwenye ku plan mambo makubwa and assigning key individuals, making things happen given different resources around them. Often hawako fixed wanabadilika badilika with a given situation. i.e. Edward N. Lowassa.

Mtu anaye jua kutumia ubongo wake vizuri in terms of planning schemes of executing things, muogope sanaa.

You are very right Senior Boss. Lowassa is much like Deng Xiaoping - the sole brain behind the transformation of China from a giant impoverished nation to a global economic super power in less than one generation. Like Deng, Lowassa is a great strategist who embrases this philosophy: "A LITTLE LESS TALK AND A LOT MORE ACTION".
 
Baada ya kum tathmini kwa karibu yule mzee ndipo nikamuelewa sanaa. Ndio umri umeenda, he isn't strong like a 30 year old man. Kikubwa cha kuangalia ni madini aliyonayo kichwani na nguvu na uwezo alionao ku make things happen ndio vime badilisha msimamo wangu kwa kiwango kikubwa.

If only ingetokea Lowassa (President) & Magufuli (Prime Minister) were to work together...wangefanya mambo ya ajabu na kushangaza sanaa. Hvyo basi kwa kua Magufuli yuko on tha other side....anayefaa ku collaborate na Lowassa ni Mbowe (na vichwa vingine kama Lisu).

#MtazamoTu.
 
Leo ngoja niwasaidie jamaa zangu wa CCM ambao wengi wao hawajui Hesabu. Tangu Mgombea Urais wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa atangaze Elimu bure, kuna watu wamekuwa wakiona huo kama muujiza.

Kwa kifupi zipo njia nyingi sana zinazoweza kufanya Elimu kuwa bure kuanzia Shule ya msingi hadi Chuo Kikuu. Leo ngoja niongelee 'alternative' moja.

Kwa mujibu wa TAMISEMI Tanzania ina jumla ya shule za msingi 16,343 zenye wanafunzi 8.3 mil. Kwa upande wa sekondari shule zimeongezeka kutoka 531 mwaka 2005 hadi 4,576 mwaka 2014. Idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804,056 mwaka huu.

Kwa upande wa elimu ya juu, idadi ya vyuo imeongezeka kutoka 26 hadi 54 kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2014 na kufanya idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iongezeke kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 200,986 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Hotuba ya bajeti ya wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014/2015, wanafunzi wa shule za msingi wanakadiriwa kugharamia kiasi cha Sh.10,000/= hadi 15,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa wanafunzi wote wa shule za msingi Tanzania wanahitaji Bilioni 80 waweze kusoma BURE.

Shule za Sekondari za Serikali zinakadiriwa kuwa 2,446 zikiwa na jumla ya wanafunzi 1,004,071. Kati yao wanafunzi 185,652 ni wa Shule za Kulala (Boarding), na wanafunzi 818,419 ni wa shule za kutwa (Day).

Wanafunzi wa Shule za kutwa wanalipa ada TZS 20,000 kwa mwaka. So ukichukua 20,000 × 818,000 utapata Bilioni 16.3. Wanafunzi wa shule za Bweni wanalipa ada TZS 70,000/= kwa mwaka. So ukichukua 70,000 × 185,652 utapata Bilioni 11.2.

Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu wa vyuo vya Serikal na vya binafsi wapo 200,986. Kati yao wanafunzi 162,987 wanasoma Course za 'Social Science, Law, Humanities, Education etc' ambao ada zao hazizidi Mil.2 kwa mwaka. So chukua 162,989 × 2000,000/= utapata Bilioni 325.
Wanafunzi 37,997 wanasoma course za "Science" kama Engineering, Udaktari etc na ada zao ni zaidi ya Mil.3 kwa mwaka. So hawa watahitaji Bil 113.5 kulipa ada ya mwaka mzima.

Fedha ya kujikimu pamoja na chakula (Meals & Accomodation) inayotolewa kwa sasa ni TZS 7,000 kwa siku kwa mwanafunzi mmoja. Hivyo basi mwanafunzi mmoja anapata Jumla ya Shilingi 1,680,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu ambao ni 200,986 wanahitaji Bil 337.

Fedha ya Utafiti (Research), Mafunzo kwa njia ya vitendo (Field) na vitabu (Stationeries) hutolewa jumla ya Shilingi 735,000/= kwa mwaka ambayo hugawanywa kulingana na asilimia ya mkopo ya mwanafunzi. Hivyo basi wanafunzi wote wanahitaji Bil 147 kwa mwaka.

Ukijumlisha gharama zote hapo juu utapata jumla ya Shilingi Bilioni 934 tu. Kwa lugha rahisi ni kuwa ili kila mwanafunzi nchini asome bure kuanzia Elimu ya msingi, sekondari na akifika Chuo Kikuu alipiwe gharama zote bure kwa asilimia 100%, serikali inahitaji kutoa Shilingi Bilioni 934 tu kila mwaka.
Swali, Je hizi Bilioni 934 zinapatikanaje?

Ukisoma hotuba ya Bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2014 utagundua kuwa Mlima Kilimanjaro peke yake unachangia karibu Bil.800 kwenye pato la Taifa (Gross National Income of $350 Milion).

Kwa lugha Rahisi ni kuwa tunahitaji Mlima Kilimanjaro mmoja tu ili watoto wetu wasome bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu. Yani tukiamua mapato yote ya Mlima Kilimanjaro tuyapeleke kwenye sekta ya Elimu bila kuchakachua, tutakua na uhakika wa kusoma bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo kikuu. Je hatuwezi??

Hapo hatujagusa Mbuga za wanyama, hatujagusa Bandari, Madini, Gesi, Mazao ya misitu, Uvuvi, Kilimo, Viwanda, etc. Tumegusa mlima Kilimanjaro peke yake. Kwakuwa CCM hawawezi tunawaweka pembeni tunaoweza tufanye.!
 
Swala la kutokuwezekana kwa elimu ya bure halipo kwenye mapato, nchi za ulimwengu wa kwanza zina mapato makubwa sana, lakini elimu siyo bure.

Kwa bajeti zetu zilivyo tegemezi unafikiri nchi za kipepari zitakubali kukupa msaada ili ufanye kitu ambacho wao wanaamini ni kinyume na principles zao? Kwa principle za kibepari ni kwamba mtu huthamini kitu alichokigarimia, ndo maana hata shopping bags (za plastic kwenye supermarkets) serikali za kibepari huwa zilalazimisha ziuzwe ili mtu asiitupe ovyo.

Jambo la muhimu hapa ni kuweka garama wanazomudu watu, na kuweka utaratibu wa kuwasaidia wale wasiokuwa na uwezo kabisa.
 
Mkuu TKNL unanishangaza sana.

Sasa unataka kulinganisha nchi za ulimwengu wa kwanza na sisi?

Unadhani kwa nini makampuni makubwa duniani hayaji africa kuwekeza? Unadhani ni bahati mbaya?

Wachina hawakufika hapo hivi hivi!!! Waliseomesha watu wao...

Haya tuliyofanyiwa ndo maana yanatufanya tuone umbali wa pua zetu mambo muhimu katika mustakabali wa maisha yetu na vizazi vyetu...

Amka ndugu shule ndo kila kitu....

Hayo majamaaa yanaua shule za umma makusudi halafu watoto wao wanawapeleka nje, ili vivazi vyao viendelee kuwa watawalaaaa...

Amkma mazee....
 
Last edited by a moderator:
Inaonekana wewe umezaliwa miaka ya 2000. Elimu bure mpaka Vyuo Vikuu Sera hiyo haipo popote duniani kwenye Uchumi wa Soko.

Pia hesabu zako zinapotosha kwa kuwa Vyuo na Shule haviendeshwi kwa ADA pekee. Kuna Ruzuku kutoka Serikalini na Vyanzo vingine. Nafikiri uchambuzi wako ni wa mtu aliyezidiwa na VIROBA. Shame!

Swala la kutokuwezekana kwa elimu ya bure halipo kwenye mapato, nchi za ulimwengu wa kwanza zina mapato makubwa sana, lakini elimu siyo bure.

Kwa bajeti zetu zilivyo tegemezi unafikiri nchi za kipepari zitakubali kukupa msaada ili ufanye kitu ambacho wao wanaamini ni kinyume na principles zao? Kwa principle za kibepari ni kwamba mtu huthamini kitu alichokigarimia, ndo maana hata shopping bags (za plastic kwenye supermarkets) serikali za kibepari huwa zilalazimisha ziuzwe ili mtu asiitupe ovyo.

Jambo la muhimu hapa ni kuweka garama wanazomudu watu, na kuweka utaratibu wa kuwasaidia wale wasiokuwa na uwezo kabisa.
 
Tanzania elimu bure inawezekana acheni kumpuuza mtoa mada.
Mbona amewafafanulia vizuri sana.
Sisi wananchi tunasema inawezekana na Lowasa ndiye rais wenu.
 
Mkuu TKNL unanishangaza sana.

Sasa unataka kulinganisha nchi za ulimwengu wa kwanza na sisi?

Unadhani kwa nini makampuni makubwa duniani hayaji africa kuwekeza? Unadhani ni bahati mbaya?

Wachina hawakufika hapo hivi hivi!!! Waliseomesha watu wao...

Haya tuliyofanyiwa ndo maana yanatufanya tuone umbali wa pua zetu mambo muhimu katika mustakabali wa maisha yetu na vizazi vyetu...

Amka ndugu shule ndo kila kitu....

Hayo majamaaa yanaua shule za umma makusudi halafu watoto wao wanawapeleka nje, ili vivazi vyao viendelee kuwa watawalaaaa...

Amkma mazee....

Hujanisoma rafiki, sijakataa umuhimu wa elimu, wala sijalinganisha Tanzania na nchi za dunia ya kwanza, nilichokuwa najaribu kuelezea ni kuwa kwa kuwa nchi yetu ni tegemezi, misaada itakuja na mashariti ya uchangiaji na ushilikishwaji wa wananchi. Na hapo ndo elimu ya bure inatagonga kisiki. Mimi nasapoti elimu ya bure, ila anayeiahidi anatakiwa atupe maelezo ya kutosha juu ya jinsi atakavyo-implement, isije ikawa tunadanganywa.

Miaka ya nyuma tulishawahi kuwa na sera ya elimu bure na matibabu bure. Unafikiri ni nini kilitubadilisha? Ni IMF na WB, waligoma kutoa misaada mpaka nchi iweke utaratibu wa kuchangia. Utetezi wao ni kwamba mtu anajituma zaidi na anaweka thamani zaidi kwa kitu alichokilipia (Hii niliisikia mwenyewe katika moja ya speech ya Vice President mmoja wa WB alipotembelea TZ). Kama bado tunahitaji pesa za IMF na WB ni vigumu kuongelea elimu ya bure.

Na umeongelea swala la watawala kuuwa shule za umma na kupeleka watoto nje; unafikili hili litakomeshwa na elimu ya bure?
 
Elimu bure inawezekana Kodi wanazo samehe na magari ya kifahari tukiamua kupunguza matumizi yasiyo ya lazima gharama za sikukuu za kitaifa
 
Tanzania elimu bure inawezekana acheni kumpuuza mtoa mada.
Mbona amewafafanulia vizuri sana.
Sisi wananchi tunasema inawezekana na Lowasa ndiye rais wenu.

inawezekana ndio kwa upande wa ada serikali ikagharamia, ila kwa vyuo vp kuhusu pesa za accomodation na wale watakao chaguliwa vyuo vya private?
 
Hujanisoma rafiki, sijakataa umuhimu wa elimu, wala sijalinganisha Tanzania na nchi za dunia ya kwanza, nilichokuwa najaribu kuelezea ni kuwa kwa kuwa nchi yetu ni tegemezi, misaada itakuja na mashariti ya uchangiaji na ushilikishwaji wa wananchi. Na hapo ndo elimu ya bure inatagonga kisiki. Mimi nasapoti elimu ya bure, ila anayeiahidi anatakiwa atupe maelezo ya kutosha juu ya jinsi atakavyo-implement, isije ikawa tunadanganywa.

Miaka ya nyuma tulishawahi kuwa na sera ya elimu bure na matibabu bure. Unafikiri ni nini kilitubadilisha? Ni IMF na WB, waligoma kutoa misaada mpaka nchi iweke utaratibu wa kuchangia. Utetezi wao ni kwamba mtu anajituma zaidi na anaweka thamani zaidi kwa kitu alichokilipia (Hii niliisikia mwenyewe katika moja ya speech ya Vice President mmoja wa WB alipotembelea TZ). Kama bado tunahitaji pesa za IMF na WB ni vigumu kuongelea elimu ya bure.

Na umeongelea swala la watawala kuuwa shule za umma na kupeleka watoto nje; unafikili hili litakomeshwa na elimu ya bure?

Pesa nchi hii zipo...wewe ndo hujui kabisaaa.

Hayo masera ya IMF na WB hapa ndo mahala pake, najua.

Ukiua utegemezi wa nje unafanya utakavyo, sisi na CCM yetu utgemezi haujawahi kupungua unaongezeka, wanchokifanya wanaleta bajeti za kisaniii tu, bajeti wanayojua kabisaa kuwa haitekelezeki...

Nilitaka ujue, si bahati mbaya kuua elimu ya umma, ni mkakati. Usidhani JK hakuwahi kuwa na nia njema y akusaidia wananchi, alkiingia na kasi na ari ya kusaidia, mfumo umeoza na kujawa na walafi wasiotaka kutoka.

Endeleeni kudanganywa, na mnaingia fulu na sijui hapa makazi tu sijui ni nini!!! Kuua mfumo lazima janga la kijani litoke...
 
Swala la kutokuwezekana kwa elimu ya bure halipo kwenye mapato, nchi za ulimwengu wa kwanza zina mapato makubwa sana, lakini elimu siyo bure.

Kwa bajeti zetu zilivyo tegemezi unafikiri nchi za kipepari zitakubali kukupa msaada ili ufanye kitu ambacho wao wanaamini ni kinyume na principles zao? Kwa principle za kibepari ni kwamba mtu huthamini kitu alichokigarimia, ndo maana hata shopping bags (za plastic kwenye supermarkets) serikali za kibepari huwa zilalazimisha ziuzwe ili mtu asiitupe ovyo.

Jambo la muhimu hapa ni kuweka garama wanazomudu watu, na kuweka utaratibu wa kuwasaidia wale wasiokuwa na uwezo kabisa.

wanajifanya hawaelewi
 
Back
Top Bottom