Lowassa azungumzia afya yake, Rushwa katika Chaguzi za CCM...

Kwa wale mliotaka kujua kama Lowassa akiwa Rais atakuja kukemea rushwa, Mzee huyu amewasikieni, hapa ni maelezo yake kuhusu Rushwa kwenye chaguzi za CCM kama alivyonukuliwa leo Jumanne na Gazeti la Mwananchi.

"Ninaendelea na matibabu mazuri katika jicho langu moja ambalo nilifanyiwa upasuaji miaka miwili iliyopita hapahapa, (Ujerumani), ninatarajia kurejea nyumbani wakati wowote kuanzia sasa kuungana na Watanzania wenzangu katika kulijenga taifa letu."
.......

Haya maneno yamekuwa yakijirudia sana bila vitendo,ccm ni janga la kitaifa litatumaliza yaani wao ndio wameshikilia rungu lakini bado wanalialia na rushwa kana kwamba wala rushwa wamegeuka upepo hawaonekani!!!

Acheni kutupumbaza wananchi kwa ngonjera zenu za kila siku,kiongozi makini ni yule anaezungumza kupitia vitendo tu..Sumaye nae wimbo ni ule ule/Jakaaya nae vivyo hivyo mmetuchosha.
 
yeye ndo bingwa wa rushwa kuna jamma mmoja alikuwa anagombea udiwanai kwa chadema monduli mjini mwaka 2005 akamhonga laki tano ili ajitoe mana alikuwa anakubalika kweli na angeshinda....sasa sijui anajiambia yeye au.....na alivowatuma TAKUKURU Awashike wabunge wawili arusha lekule ana elisa ili mtu wake agombee peke yake uenyekiti wa chama mkoa arusha....hii ni seinema tuu isiyo na director....
 
Ha ha ha ha ha,ha ha haha...jamani nnji hii balaa....ha ha ha ha ha ha....wajinga ndio waliwao....ha ha ha ha...ila sisi wabongo nao tumezidi uboga...tunadanganywa danganywa tuuuu tuuuu
 
Imemchukua miaka mingapi kugundua kuwa kuna tatizo la rushwa na kuwa TAKUKURU inahitaji kupewa meno zaidi. Well, kwa vile anamvuto sana natumaini akirudi ataleta mswada wa kuifanyia marekebisho TAKUKURU ili iwe na meno kweli ya kumuuma hata yeye......

Nadhani dhana ya 'Vita dhidi ya rushwa' itakuwa imebadilika kwa kupata maana mpya, ndio maana akapata mawazo haya leo
.
 
Duh! huyu ni sawa na ukishajisaidia na kukimbia kinyesi chako,yeye awe cardinal wa kugawa rushwa alafu ahikane rushwa?
 
Lowassa have nothing to offer on the war of fighting corruption he is a big manipulator, elusive, evasive and coercive person who is ready to do anything even taking someone life who stands his way to presidency. Lowassa is a kingpin of corruption in Tanzania.....

Lowasa ni janga kwa watanzania!!!! Ee Mungu tuepushe watanzania na huyu Belzebul
 
EL akichukua nchi kama president nitachulua uraia wa nchi nyingine kuliko kumuona mwizi huyu akipigiwa salute na mizinga 21.
 
Nchi ya kunung'unika na kulalamika.

Dhambi ya kunung'unika ni mbaya sana kuliko kuuwa.

Poleni sana
 
Ni kauli nyepesi ambayo ingeweza kutolewa na mtu yeyote. Haionyeshi hata kidogo dhamira ya dhati ya kupambana na rushwa. CCM bila rushwa haiwezekani. Dawa ni kuiondoa kwanza CCM au kuondoka CCM.
 
Kwa wale mliotaka kujua kama Lowassa akiwa Rais atakuja kukemea rushwa, Mzee huyu amewasikieni, hapa ni maelezo yake kuhusu Rushwa kwenye chaguzi za CCM kama alivyonukuliwa leo Jumanne na Gazeti la Mwananchi.

Lowassa azungumzia rushwa.........

Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ambaye kwa sasa yuko Ujerumani kuchunguzwa afya yake, ameeleza kusononeshwa kwake na habari za rushwa zilizokithiri ndani ya CCM.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Lowassa alisema: “Nikiwa mwanaCCM na Mtanzania, ninasononeshwa sana na taarifa za kukithiri kwa vitendo vya rushwa ndani ya chama chetu, serikalini na katika taasisi mbalimbali.

“Ni kweli kwamba, rushwa ni tatizo. Ni kansa ambayo kama taifa, hatuna budi kulitafutia ufumbuzi wa kimfumo badala ya kuendelea kufikiri kwamba linaweza kumalizwa kwa njia ya kulalamika, kulaumiana na kupakana matope.

“Tunao wajibu wa kuhakikisha kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inapewa meno na kuimarishwa zaidi katika kukabiliana na vitendo hivi vya ukiukwaji wa maadili.”

Akizungumzia afya yake Lowassa alisema: “Ninamshukuru Mungu siha yangu ni imara na kwamba madaktari walionifanyia uchunguzi wamejiridhisha pasi na shaka kwamba afya yangu ni njema.

“Ninaendelea na matibabu mazuri katika jicho langu moja ambalo nilifanyiwa upasuaji miaka miwili iliyopita hapahapa, (Ujerumani), ninatarajia kurejea nyumbani wakati wowote kuanzia sasa kuungana na Watanzania wenzangu katika kulijenga taifa letu.”

Kwenye RED. I predict another good attempt by Edward Lowassa to rejuvenate. Is he going to make it again after systematical series of come backs and winnings in his party? I can now see the real Lowassa bearing CCM's presidential flag after JK in 2015 by hidding his traits.

Anasisitiza tuhuma zote za ruswa dhidi yake ni uongo, majungu na fitina.Anataka kuzipiga teke na kwa kweli chini ya nguvu aliyonayo sasa kwa Wahariri wa vyombo vya habari kupitia Editors' forum ya akina Absalom Kibanda na Neville Meena hakika ataweza, atashinda.

Ili kudhibitisha 'anaichukia' rushwa, anataka aone TAKUKURU ikipewa meno zaidi kuliko ilivyo sasa.Nani sasa Msafi ndani ya CCM apindue mtumbwi 'Salama' anaotaka kuupanda Lowassa kuelekea kilele cha URAIS? Atavuka tena kama alivyoruka viunzi vingi zaidi ndani ya CCM tangu adondoshwe na RICHMOND mwaka 2008? Another strategy hidden in prevarication.
 
Katika hii taarifa sijaona sehemu aliysema kuwa yeye hatoi rushwa. Mtu anaweza kuwa kinara wa kutoa rushwa lakini akawa anasikitika kuwa analazimika kutoa rushwa ili apate anachokitaka...
 
Hivi tunahitaji mtu ambaye hatoi au kupokea rushwa ili aje akemee rushwa ndani ya Nchi. yupo kweli sina uhakika.

Rushwa Tanzania ni mfumo ambao uko ndani ya CCM na ili kuudhoofisha ni kujitoa CCM au Kuiondoa CCM madarakani. Hakuna mwanaccm ambaye anaweza kukemea rushwa akiwa ndani ya CCM huo ni unafiki.
 
Wana JF, huyu jamaa aliyeandika hizi comment za Low has juu ya rushwa ndani ya ccm, ukweli ni kwamba ni kibaraka wa lowassa, halafu ni maiti anayetembea, mimi binafsi naona kwamba ni mpumbavu hapa JF huwezi kutudanganya aendelee tu kumuosha fisadi/lowassa miguu na kula matapishi yake.
MY INTAKE: Lowassa ndo kiongozi pekee ambaye kila mtu anamfahamu kwamba kila alikofanyia kazi amedhuluma umma wa Tz angalia AICC ARUSHA, Alipokuwa waziri wa Ardhi na alipokuwa pm halafu angalia alipowauza wamasai kwa kuwahonga pombe,nyama za pori na kuwafundisha namna ya kufitina watu na kugawa hongo kwa wamasai, pia angalia alivyowatengeneza waandishi uchwara wa kumpamba kama maiti,pia angalia chaguzi zote za cmm kwa mwaka huu amegawa mabilioni ya pesa ili mtandao/wafuasi wake wapite.
Halafu jamaa ana kikundi cha wamafya za kuwamaliza wapinzani wake hebu waulizeni watu monduli wanavyojuta/kutabika kwa kumchagua huyu mwizi mkuu wa raslimali za umma.
KILA WAKATI WANA ELEZA HUYU JAMAA LOW HAS HAFAI KWA LOLOTE KTK UONGOZI NA ACHENI NDOTO ZA KUONGOZWA NA WEZI, TUMKATAE KWA HALI ZOTE.
yeye ndiye kamanda mkuu wa ugawaji rushwa Tz.
......

Mkuu hapo umeonyesha chuki zilizpitiliza dhidi ya EL mpaka kumwita maiti mtarajiwa,hapo kubali umeteleza mkuu.

H
akuna mwenye mkataba na Mungu pengine hata wewe unaweza tangulia kufa kuliko huyo unayemchulia kifo,hata kama unahongwa kumchafua mtu lkn utoe hoja za msingi zinazokubalika na siyo kutokwa povu hovyo.
nawasilisha
 
Kweli siasa ni mchezo mchafu, nimeamini siasa bila unafiki na uongo haiendi hasa bongo! Yaani lowassa hata aibu hana! Lowassa ni moja ya wanasiasa wanaoamini katika ushindani wa rushwa/fedha kwenye chaguzi.

Ni mzee huyuhuyu aliyehamisha watu kwa mabasi toka monduli mjini kwenda mto wa mbu mkoani Arusha ili wasimsikilize dk slaa wakati wa kampeni 2010, huku akiwapa pesa,wali na nyama! Hiyo haikuwa rushwa?,.vip uchaguzi wa kumpata sioi ndani ya ccm kule arumeru mashariki? Watanzania!watanzania! Tusipokuwa makini tutavuna mabua.

Kweli katika nimeamini msemo wa 'if u cant beat them, join them'. Haa haaa.

Nadhani ukijijua sio mnafiki basi bora usiingie katika siasa

Ukijiona wewe ni mkweli sana na uongo huuwezi, usiingie kwenye siasa
 
Back
Top Bottom