Rais Samia: Wanasiasa, Polisi, Ofisi za Umma waongoza kwa rushwa

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,753
15,227
Jeshi la Polisi, ofisi za umma, Mahakama, wafanyabiashara na taasisi za elimu ya juu ni miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kuwa na vitendo vya rushwa.

Arusha. Rais Samia Suluhu Hassan ametaja maeneo yanayoongoza kwa rushwa nchini kuwa ni wanasiasa, Jeshi la Polisi, ofisi za umma, Mahakama na kuzitaka mamlaka zinazohusika kufuatilia taasisi hizo.

Makundi mengine yanayoguswa ni pamoja na wafanyabiashara na taasisi za elimu ya juu.

Ameyasema hayo leo Julai 11, 2023 jijini Arusha katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kupambana na rushwa barani Afrika yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 tangu kusainiwa mkataba wa Umoja wa Afrika wa kupambana na rushwa.

“Rushwa inaadhoofisha mifumo ya kitaasisi na kuathiri mipango, vitendo vya rushwa haviiishii kwenye mipaka ya kitaifa kwa kutambua hili ni muhimu kwa nchi za Afrika kushirikiana katika mapambano haya kwa kupeana misaada ya kisheria pamoja na ushirikiano wa kiufundi.

“Wala rushwa wanapaswa kufahamu kuwa nchi zetu si vichaka vya kuficha fedha zinazotokana na rushwa au kufuga wala rushwa, tunataka dunia nzima ifahmu kwamba Afrika si mahali salama kwa wala rushwa na hilo lionekane kwa vitendo kupitia hatua tunazozichukua na si mikutano, makongamano na maneno peke yake,” amesema.

Aidha amesema kuwa, Serikali inaendelea kuimarisha Taasisi ya rushwa kwa upande wa bajeti na mifumo ili kuleta ufanisi katika mapambano dhidi ya rushwa.

Ameongeza kuwa, Tanzania ilisaini mkataba huo Novemba 5, 2003 na kuridhia Febuari 22, 2005 na mkataba kuanza kutumika rasmi Agosti 5, 2006.

Amesema Tanzania ni moja ya 48 miongoni mwa nchi 55 zilizosaini na kuridhia mkataba huo.

Akizungumza awali kwenye mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, George Simbachawene amesema katika maadhimisho hayo mamlaka za kupambana na rushwa zilikuwa na majadiliano yaliyolenga kujitathmini katika utekelezaji wa majukumu yao
 
Mimi ningefuta kabisa mishahara kwa hii idara ya Polisi ili wajilipe na hizo rushwa wanazokula
 
Kama vipi watafute muwekezaji kwenye Jeshi La Polisi, kama walivotafuta mwekezaji bandarini.
Juzi nilikwenda kula kwenye kijiwe flani hivi Cha ma afisa wa police, kweli nikajiunga nao kwenye meza yao,Sasa kwenye ma story yao ya town wakawa wanawalaumu sana Watumishi wa Mahakama za mwanzo kua ni wapenda Rushwa sana,na wanaangalia mwenye pesa ndiyo wanampa ushindi na wakazidi kusema Mahakama za mwanzo hakuna haki! Na wakati huo na wao kuna issue za Rushwa nao wako wanasikilizia!!
 
Back
Top Bottom