Lowassa awapasha akina Nape na Mangula...

Nimependa hiyo kuwa wana mgombea wao na ameshajaza form anasubiri siku ya kurudisha. ..

Mkuu,

hivi Visebengo vya Lumumba vipo CCM-EL,CCM-Sitta,CCM-Migigro ama CCM-Membe?
 
Kama Zitto alinunuliwa na CCM, basi Lowassa anaweza kununua mtu yeyote kuwa kwenye kambi yake. Na anaweza akaununua na Urais pia. Lowassa ni janga la kitaifa..mtu gani asiyejali na kuogopa mamlaka zilizo juu yake? Je yeye mwenyewe akiwa ndio mamlaka...kuna atakayemgusa kweli?
 
Lowassa ni Rais wa Tanzania 2015 - 2025...! Kama hutaki kajizike...!
 
mini kilimzuia kutokea kwenye kikao cha msasani ili akasafishwe kama alivyoomba,hadi akasababisha mzee wetu kuunganishwa naye,wote wakahitwa wapumbavu nakutakiwa kuacha upumbavu wao?

mama yako ndiye aliyemzuia
 

Kivp mkuu Lowassa na Ttcl kuna uhusiano gani?
 
Lowasa anafaa sana kua Rais wa Tanganyika,hata huku ndani ccm viongozi wakuu wengi wao wanapenda Edo ashika nchi,tatizo linalowafanya wanapata woga kidogo ni roho yake ya ULIPIZAJI KIISASI, sasa wanadhani akishika madaraka atawalipiza maba
ya wale wote walio kua wabaya wake.
 
Sijuhi huyu mzee akitemwa na kamati kuu ya CCM katika mchujo wa awali wa wagombea Urais atakuwaje? pressure na kisukali zitapanda sana!
 
kumbe ukiwa unamfukuza mwizi kwa kitendo chake kiovu cha kupora,alafu ukakutana na kiibaka mwingine anakwapua unaacha kuukemea wizi na unaushangilia?

Imagine, mko wawili mnamkimbiza mwizi, unakuja kujua kuwa huyu unayesaidiana naye kukimbiza mwizi amepata mgao kwenye wizi uliofanywa na yule mnayemkimbiza, unafanyaje?

1. Utaendelea kumkimbiza yule mwizi kwa kusaidiana na mtu ambaye tayari ana mgao?

2. Utamwambia huyu we baki kwa sababu ni mmoja wao, then umkimbize yule kwanza halafu baadae urudi kumkimbiza huyu uliyekuwa unasaidiana naye?

3. Utamkamata huyu wa karibu, then urudi kumkimbiza yule mwizi wa mwanzo?
 
Lowasa akishika nafasi katika serikali Nape itabidi aishi india
 
Utabiri wa mtoto wa marehemu Shekhe Yahaya unaonyesha kuna nguli wa siasa atatemwa na chama chake na kisha kufariki. Bila shaka mwanasiasa huyu ni E. Lowasa ama Zitto.
Kwahiyo acha Lowasa atapetape maana mfa maji haachi kufanya hivo.
 
Endelea kupaka rangi kwenye upepo...EL ni maarufu anakubalika zaidi ya CCM na WanaCCM kwa umoja wao x 1000... I'm afraid so far CCM haina option nyingine zaidi ya EL... Kubali kata ujinyonge ...
 
Utabiri wa mtoto wa marehemu Shekhe Yahaya unaonyesha kuna nguli wa siasa atatemwa na chama chake na kisha kufariki. Bila shaka mwanasiasa huyu ni E. Lowasa ama Zitto.
Kwahiyo acha Lowasa atapetape maana mfa maji haachi kufanya hivo.

mtaanza kufa ww na huyo mumeo mtabiri,na mshindwe mlegeee hadi ---- washirikina wakubwa nyie
 
Ndugu zangu, Mh Lowasa aachane na siasa mwambie asije akajikuta anakufa kwa presha. Serikali haitompa ruhusa luwa Rais huu ndio ukwel. Watamdhohofisha kwakweli niliwah sema nauona mwisho wa Lowasa

Kama kweli Edward Ngoyayi Lowassa atateuliwa na CCM kama mgombea wa Urahisi kwa mwaka 2015 basi itakuwa ni kudhihirisha tu kuwa nchi hii inaweza kuongozwa na Juha yeyote!!!

Hivi huyu Lowassa si ndiye aliyepatikana na kashfa au tuhuma za Ufisadi wa Richmond(Richard wa Monduli) na kwa hiari yake kabisa tena bila kulazimishwa akajiuzulu Uwaziri Mkuu???Kama Uwaziri Mkuu tu ulimshinda akamwaga manyanga iweje leo atushawishi kuwa anaweza kukalia kiti cha Ikulu the Highest Office in our Country???

Haya ni matusi kwa Watanzania wote. Hatutakubali FISADI aingie Ikulu asilani. Kama tu kwenye Uwaziri Mkuu alifanya ufisadi itakuwaje huyu bwana akipewa Ikulu?? Believe me huyu jamaa atauza nchi yote. Hivi watu wanafikiri hii pesa anazowahonga Maaskofu na Mapdre makanisani na hao Masheikh na Maustazi kwenye miskiti anazitoa wapi???Jueni kuna mahali anaziiba na akiingia Ikulu lazima arudishe kwa kupitia nyie Wananchi!!!

Mimi naomba CCM waharakishe kumteua kuwa mgombea wao wa Urahisi kwa 2015. CCM ndipo wataijua Tanzania ya sasa na siyo ile ya zidumu fikra sahihi na mbovu za Mwenyekiti. CHADEMA itakuwa imepata tiketi ya moja kwa moja kwenda Ikulu bila mpinzani kutoka CCM. Lowassa hawezi kuwa Rais wa nchi hii,hafai na hakubaliki kama Malaria!!!

Tafakari
 
Sijuhi huyu mzee akitemwa na kamati kuu ya CCM katika mchujo wa awali wa wagombea Urais atakuwaje? pressure na kisukali zitapanda sana!

Nani wa kumtema? yeye ndo mwenye uwezo wa kuwatema kama alivyofanya majaribio kwenye kura za marohani baada ya kupata mafanikio sana alitoa suluhisho la kusitisha uasi na ukafanikiwa !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…