Mimi simtetei Lowassa wala Nape au Mangula lakini nataka niwakumbushe watanzania.
Jamani ebu kumbukeni mwaka 1995, walijitokeza wagombea urais kutoka ndani ya CCM kama 9 hivi. kuna mgombea mmoja alihojiwa hivi na Nyerere " Mwenzetu umepataje utajiri huu kwenye nchi maskini ". alishindwa kujibu na hajajibu mpaka leo.
Sasa hivi ndani ya CCM kuna watu wameanza kujitangaza kupitia makanisani na misikitini wakitoa pesa kwa njia ya harambee. Mmoja ameulizwa mwenzetu hizi fedha nyingi unazochangisha umezitoa wapi? Nimesikia amejibu yeye hana fedha ila anachangiwa na marafiki zake. Lakini nimeambiwa huyu anayechangisha ni yule yule ambaye Nyerere alimhoji . Kama ni yeye basi awaambie watanzania alifirisika lini?. Lakini pia naambiwa ni yeye yule yule kwa namna fulani alihusika na ufisadi wa Richmond. Lakini naona watanzania kama wamesahau. Jambo moja niliseme: Mimi naona mtu akiingia madarakani kwa kutoa hela yake kuwashawishi watu ni afadhali kuliko yule anayechangiwa fedha na matajiri kwani akipewa madarka watamsakama wakidai riba kwa fedha walizo mchangishia hivyo ataliweka taifa rehani. huyu anayetoa fedha zake ni hatari lakini ni nafuu kwani yeye atataka arudishe hela yake tu. Huyu anayechangiwa hafai kabisa kwani baadae ataiuza nchi kwa marafiki waliomchangia. Kumbukeni awamu ya nne ilivyoingia madarakani na misukosuko ya Richmond, EPA, na meremeta. Halafu aliyetakiwa ajivue gamba ni nani eti?
Nawasihi watanzania tukumbuke historia tunapofanya maamuzi.
Halafu mimi sijui pesa zinazotolewa makanisani na miskitini na wanasiasa wanaotaka urais zinakubalika kama sadaka mbele ya Mungu. Nakumbuka kwenye maandiko matakatifu juu ya mama aliyetoa senti moja na mafarsayo matajiri yaliyotoa maelfu lakini imeelezwa sadaka iliyokubalika ni ile senti ya mama maskini siyo zile fedha nyingi zilizotolewa?!. Haya makuhani na mashehe angalieni changamoto hiyo.
Halafu naomba mtafakari falsafa ya moja inayosema:mtu anayetaka sana kuwa kiongozi hadi anunue watu hafai kabisa kuwa kiongozi. Kiongozi atkayefaa ni yule jamii inamtafuta siye anayetumia vishawishi kama rushwa. niishie hapa leo.