Lowassa atoa mpya..............

Lowassa atoa mpya..............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,504
Reaction score
911,249
Lowassa awaonya vigogo wanaojali matumbo yao

na Violet Tillya, Arusha

amka2.gif
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametoa wito kwa wabunge na madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita kuhakikisha wanafanya kila liwezekanalo kubadilisha hali ya maisha ya wananchi wao kiuchumi. Kadhalika amewataka viongozi hao kuweka kipaumbele katika kujali matumbo ya wapigakura wao ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kuwakopesha ili waweze kuanzisha miradi ya kujikwamua kiuchumi kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi wengi hapa nchini.
Lowassa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Manyire, Kata ya Mlangarini, wilayani Arumeru alipokuwa akizungumza katika sherehe za kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kumchagua diwani wao Mathias Manga (CCM).
"Wakati umefika kwa viongozi katika maeneo mbalimbali hapa nchini kubadilika na kuacha tabia na mazoea ya kujinufaisha wao wenyewe na familia na jamaa zao na kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi kuwatumikia wananchi hususan kujali wanakula nini"� alisema Lowassa.
Pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uamuzi wake wa kukubali mabadiliko ya Katiba na kutoa wito kwa wananchi kuhakikisha kuwa wakati ukifika wajitokeze kwa wingi kutoa maoni yao.
 
kweli nyani haoni kundule.......yaani huyu Lowassa sasa amekuwa ni mtu wa kuhimiza maadili ambayo yeye mwenyewe wala hayafuati.................Is this not a case of preaching water while swilling wine when nobody is watching?
 
It is a mark of an educated mind to be able to entertain a thought without accepting it

kweli nyani haoni kundule.......yaani huyu Lowassa sasa amekuwa ni mtu wa kuhimiza maadili ambayo yeye mwenyewe wala hayafuati.................Is this not a case of preaching water while swilling wine when nobody is watching?

monkey-back-22.3.jpg
 
Mnashangaa nn wakati ninyi mnaomwona mmbaya ndo ninyininyi mnaompa kura?
BTW anajiandaa kwa 2015!
 
Kwani kama baba yako akiwa na tabia ya ulevi wa kupindukia,hawezi kukuambia mwanangu usinywe pombe fanya moja,mbili,tatu........???Hii inaonyesha anajua lile lililo sahihi na wanalostahili kufanyiwa wananchi na ndo anachohamasisha.........wachungaji wangapi wanatuambia tusizini nao wana wanawake nje ya ndoa zao?????????????Mwenzenu kaliona........................anafanya na kuhamasisha wenzake.........LOL
 
Kwani kulewa sawa na wizi?....walevi wanafungwa?
 
kweli nyani haoni kundule.......yaani huyu Lowassa sasa amekuwa ni mtu wa kuhimiza maadili ambayo yeye mwenyewe wala hayafuati.................Is this not a case of preaching water while swilling wine when nobody is watching?

Kwa jinsi wadanganyika tulivyo vishoka/ wasahaulifu huyu 2015 atakuwa tayari mtakatifu na anachukua nchi.
 
lakini ka mtu haka kanachukua urais hivi hivi kimchezo mchezo

ha ha ha kweli bongo si nchi
 
Kwani kulewa sawa na wizi?....walevi wanafungwa?
i love this one...

Aanze kwa mfano tu, arudishe japo asilimia 50% aliyochuma kuneemesha tumbo lake kwanza na pia atusaidie kujua dowans ni ya nani
 
Kwani kama baba yako akiwa na tabia ya ulevi wa kupindukia,hawezi kukuambia mwanangu usinywe pombe fanya moja,mbili,tatu........???Hii inaonyesha anajua lile lililo sahihi na wanalostahili kufanyiwa wananchi na ndo anachohamasisha.........wachungaji wangapi wanatuambia tusizini nao wana wanawake nje ya ndoa zao?????????????Mwenzenu kaliona........................anafanya na kuhamasisha wenzake.........LOL
Lakini nae atataka aonje ajue ladha yake kwanini baba yeye anywe halafu mimi anikataze kama ni mbaya mbona haachi...........Yeye ndio alitakiwa atoe mfano wa uongozi bora ndio awaelekeze na wengine. Anasubiri gawio la bil. 189 Dowans halafu anawaambia watu wafuate maadili ya uongozi, wawatumikie wananchi na wasijiangalie matumbo yao?

Angalizo langu ni kuwa huyu bwana anajisafisha na ndio Rais ajaye wanaempandikiza maana kwasasa amekuwa mstari wa mbele kuonya mabaya (narejea kauli yake aliyosema wiki chache zilizopita wakati wa mbio za umeya kuwa vyama vya siasa ccm/ chadema visijaribu kutibua amani iliyoko Arusha pamoja na hii ya leo kuwataka viongozi wasijali matumbo yao bali wawatumikie wananchi). Amini nakwambia Wadanganyika tutamchagua tu huyu 2015 kama akipitishwa.
 
Lowasa huyuhuyu naye anaweza kutoa ushauri?.........watu wengine km lowasa na rostamu wangeendelea kukaa kimya tu km wafanyavyo wakiwa bungeni na waendelee kuongoza majimbo yao ya watu vipofu
 
Aanze yeye kuonyesha mfano!Huwezi kumwambia mtu asiibe wakati wewe mkono wako uko kwenye mfuko wa mtu mwingine tayari!!
 
Kwani kama baba yako akiwa na tabia ya ulevi wa kupindukia,hawezi kukuambia mwanangu usinywe pombe fanya moja,mbili,tatu........???Hii inaonyesha anajua lile lililo sahihi na wanalostahili kufanyiwa wananchi na ndo anachohamasisha.........wachungaji wangapi wanatuambia tusizini nao wana wanawake nje ya ndoa zao?????????????Mwenzenu kaliona........................anafanya na kuhamasisha wenzake.........LOL

Ni vizuri akianza kwa kusema kwanini yeye anafanya ambacho hataki wengine wafanye, anatakiwa kuwa wa mfano. Sio kuwaambia watu wafanye alichoshindwa kufanya.
 
Kwani kama baba yako akiwa na tabia ya ulevi wa kupindukia,hawezi kukuambia mwanangu usinywe pombe fanya moja,mbili,tatu........???Hii inaonyesha anajua lile lililo sahihi na wanalostahili kufanyiwa wananchi na ndo anachohamasisha.........wachungaji wangapi wanatuambia tusizini nao wana wanawake nje ya ndoa zao?????????????Mwenzenu kaliona........................anafanya na kuhamasisha wenzake.........LOL

Katika Biblia Takatifu kuna kuna mstari unasema, "Toa kibanzi/boriti katika jicho lako ndipo uweze kuona kibanzi/boriti katika jicho la mwenzio"
 
Back
Top Bottom