Lowassa aponda nguvu ya umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa aponda nguvu ya umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SINGOGO, Jan 11, 2012.

 1. S

  SINGOGO Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  BOOKMARK THIS PAGE

  [​IMG]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"] Lowassa aponda nguvu ya umma [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 10 January 2012 21:07 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  Anthony Kayanda, Kigoma
  WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ameibuka na kukemea matumizi ya nguvu ya umma, yanayoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa nchini kushinikiza mambo mbalimbali, akisema hayalifikishi taifa popote.

  Akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Sekondari ya Kanisa la FPCT Bigabiro, mkoani Kigoma, Lowassa alisema nguvu wanazotumia wanasiasa kuhamasisha nguvu ya umma, ingefaa kutumika kushiriki kazi za maendeleo ili kuliletea taifa maendeleo endelevu.
  Ingawa Lowassa hakutaja chama cha siasa kwa jina, lakini Chadema ndicho ambacho kimekuwa kikitumia kauli mbiu ya Nguvu ya Umma (Peoples Power) kushinikiza mambo mbalimbali.

  "Badala ya kuonekana wakihamasika kufanya maandamano ya kupambana na Serikali, jambo ambalo halitasaidia taifa kuondokana na umasikini, nguvu hiyo ingetumika kushiriki kazi za maendeleo," alisema Lowassa.

  Alisema miradi mingi ya maendeleo imekuwa ikikwama kutokana na wananchi kukataa kushiriki kujitolea nguvu zao kwa kufanya kazi, badala yake, wanataka kulipwa fedha kutekeleza miradi maeneo yao.

  “Nguvu ya umma tunayoshuhudia kwenye maandamano ya baadhi ya vyama vyetu, ingekuwa inatumika kwa kiwango kilekile kufanya kazi za kujitolea kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa sekondari zetu, hakika taifa lingepiga hatua kubwa ya maendeleo, lakini linapokuja suala la kufanya kazi nguvu ya umma hutoweka,” alisisitiza Lowassa.


  Harambee
  Katika harambee hiyo, Lowassa na rafiki zake walichangia Sh60.5milioni taslim na kufanya michango yote kufikia Sh125 zikiwamo ahadi.

  Lowassa alisema elimu ikitiliwa umuhimu ni wazi taifa litajikomboa kutoka kwenye hali duni kwa kuwa litakuwa na watu wenye uelewa wa kutosha juu ya mabadiliko na mifumo mbalimbali ya dunia, kiasi kwamba itakuwa rahisi kufundishwa na kuelekezwa mambo muhimu.
  “Baada ya kubaini hakuna usawa katika taifa, tulilazimika kutembea nchi nzima kuhamasisha ujenzi wa sekondari za kata ili kila eneo watoto wasome. Watoto wa Kigoma wawe kama wenzao wa Kilimanjaro au mikoa mingine iliyopata mwanga wa elimu mapema, ndiyo maana angalau watoto wengi wanafika kidato cha nne sasa ikilinganishwa na miaka ya nyuma,” alisema Lowassa.

  Ajira
  Lowassa alitumia harambee hiyo kurejea kauli yake kuhusu tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini, ambao wamehitimu masomo yao ngazi mbalimbali lakini wanaishia mitaani bila kupata kazi zinazoeleweka.
  Alisema tatizo la ajira kwa vijana ni bomu linaloweza kulipuka wakati wowote na kuleta shida kwa taifa, kwa vile ndiyo nguvu kazi inayohitajika zaidi kujenga uchumi imara wa nchi, hivyo kusaidia kuondokana na umaskini, mfumko wa bei na hata kudorora kwa uchumi.

  “Nimekuwa nikilisemea sana suala hili la ukosefu wa ajira kwa vijana, kiasi kwamba kuna watu walinibatiza jina la Yohana Mbatizaji, lakini bado natoa mwito kama jamii tutafakari kwa makini jambo hili,” Lowassa alirejea kauli hiyo na kuongeza:
  “Kila tunapokutana kwenye semina na makongamano tulijadili kwa kina, vinginevyo tutakuja kujilaumu siku moja kwa sababu hata wanaohitimu vyuo vikuu, wanaopata ajira ni asilimia tano tu kwa mwaka.”

  Alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali mstaafu Issa Machibya, kusaidiana na kanisa hilo kuwashawishi watu wanaomiliki eneo inapojengwa sekondari hiyo, wapunguze gharama za fidia ya ardhi na mazao yao ya kudumu, inayofikia Sh75milioni kwa madai kwamba ni nyingi ikilinganishwa na thamani ya mradi unaotekelezwa.

  Mchungaji
  Awali, katika risala yao iliyosomwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo la FPCT Bigabiro, David Nkone, alisema wameamua kujenga sekondari ya kidato cha kwanza hadi sita kutokana na uhaba mkubwa wa sekondari za ngazi hiyo mkoani Kigoma, hususan zenye michepuo ya sayansi.

  Mchungaji Nkone aisema Chuo cha Theolojia cha FPCT Bigabiro kinachotoa mafunzo ngazi ya stashahada pia kinakusudiwa kupanuliwa na kufikia kutoa Shahada, hivyo kuongeza fursa za elimu na ajira kwa baadhi ya Watanzania.

  Kanisa hilo lilimteua Lowassa kuwa mlezi wa sekondari hiyo aliyowekea jiwe la msingi ambayo kwa sasa ina madarasa matatu yaliyofikia hatua ya rinta, lengo likiwa ni kujenga madarasa ya kidato cha kwanza hadi sita.

  Katika hatua nyingine, mjumbe wa Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM Mkoa wa Kigoma, Muhsin Abdallah Sheni, aliahidi kuchangia Sh10 milioni na kompyuta mbili, huku Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba akiahidi Sh3 milioni, Mbunge wa Viti Maalumu, Josephine Ngenzabuke aliahidi kutoa Sh2 milioni na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Machibya akiahidi Sh2.5 milioni.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. J

  John W. Mlacha Verified User

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  huyu fisadi tusipoangalia ataingia magogoni.
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  CHADEMA mmemsikia lowassa lakini...hakafu kuna watu wanataka hyu jamaa awe rais wetu,akiingia ikulu maandamano ya amani marufuku,jamii forum marufuku,nchi nzima magazeti yatakuwa matatu tu,uhuru,mzalendo na daily newz!huyu jamaa ni dikteta bandugu!
   
 4. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  wewe ndiyo unajua saa hizi mkuu umechelewa sana..
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  sasa hivi nasikia kuna kundi linajiita marafiki wa lowassa(friends of lowassa)ndio linalowezesha hayo mamilioni kila mzee anapotia mguu kupiga harambee,ndio mana kawa kivutio cha makanisa uchwara,si vinginevyo!
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nitoke vipi?
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwani nyie hamjui kuwa......Lowassa ana nguvu zaidi ya Umma?.........nyie endeleeni tu na "pipooz pawa!"
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hahahahaaa, ukickia m2 anaogopa NGUVU YA UMMA ujue ni fisadi anaogopa kunyongwa!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Yeye si kiongozi wa chama chake? Kama kweli anaamini katika kujitolea nguvu ngazi kunaweza kusababisha mabadiliko kwa nini yeye anajitolea fedha? Au kwa nini hahamasishi wana CCM kujitolea hizo nguvu kazi?
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tatizo siyo Lowassa tatizo ni wanaopokea na kumualika kwenye shughuli za kuchangisha tena kanisani??

  Makanisa na viongozi wao ndio wanamdekeza huyu kiumbe fisadi
   
 11. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  amepata kila kitu duniani isipokuwa kimoja tu.
  Na hataingia kaburini bila kutimiza malego yake.
  Just a matter of time.
   
 12. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Makanisa na viongozi wao are reclaiming back their money........
  I would have done the same.
   
 13. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Pliticians are very fun. Doing things they do not believe in. Imagine, yeye angekuwa opposition leader angefanyaje kama kila kitu kimepinda: sukari bei juu, mafuta bei juu, haki za wafanyakazi zinaminywa MAKUSUDI KABISA, kura zinaibiwa and end less problems? Angewaambia wananchi watumie nguvu hizo kwa maendeleo?

  Wanasiasa !!!!. Hivi unategemea wananchi wanaweza kutumia nguvu zao kwa maendeleo wakati hawako satisfied na mambo mengi sana kutoka kwenye serikali yao? Wana njaa, hawajalipwa bei za mazao yao na huduma mbali mbali lazime watoe rushwa? Hivi wanasiasa wanaweza kweli kusimama majukwaani na njaa? Ningetegemea an intelligent politician would ask "why and how" wananchi wanachukua NGUVU ya UMA???

  Ujanja wa wanasiasa wanasoma kwanza hali ya hewa na audience yao kabla ya kuongea
   
 14. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Huyo ndiye Lowasa ambae kwa sasa uenda anatamani awe yohana Mbatizaji,du patamu waumini ama kweli ukishangaa ya ..........utastaajabu ya ................!!!!!!!. Hakika Mungu ndiye jibu kuna wakati sisi kama binadamu uwezo wetu unafika mwisho.Manake hata Makanisa ambayo ndiyo sehemu ya mwisho tunayoamini kuwa haki inaweza kutetewa mpaka kifo kama mashahidi wa Yesu wa Uganda.Lakini imekuwa sio ila Mungu wetu anasikia
   
 15. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Watumie nguvu zao kufanya kazi ipi ya maendeleo wakati nguvu walizotumia kufanya kazi zao binafsi na kulipa kodi kubwa isiyo na kipimo hiyo kodi ndio anaifisadi Lowasa na team yake na badala waipangie miradi ya maendeleo na badala yake mwanachi analipa bei juu ya umeme, mafuta, chakula nk
   
 16. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Acha arudishe pesa alizoiba kupitia maarambee yake na urais hapati ng'o.
   
 17. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Acha arudishe pesa alizowaibia watanzania kupitia maarambee yake na urais hapati ng'o.
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Natamani hata leo EL awe rais ili awawajibishe viongozi wazembe.
   
 19. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Lowassa anakuja kwa nguvu urais mtamu!
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,676
  Trophy Points: 280
  Mnajua principle za kuua nyoka? Huyu fisadi atabakia hadithi! Kwa namna anavyoutaka Urais imekuwa zaidi ya nia na sasa ni UHAINI!
   
Loading...