Lowassa apanda chati kuelekea uchaguzi mkuu 2015

wanabodi,

wakati mchakato wa uchaguzi ndani ya chama cha mapinduzi ccm unaendelea kuanzia ngazi ya shina hadi taifa. Mbunge wa monduli edward lowassa anaonekana kupanda chati kwa kasi ya ajabu na kuonekana ana nafasi kubwa katika mbio za urais 2015.

Uchambuzi wa kisiasa unaonesha karibu kila kona ya nchi hii, katika watanzania 10 utakaowahoji kuhusu ni nani hasa anayefaa kumrithi rais wa sasa kikwete, saba kati yao wanamtaja lowassa wakidai ni "jembe" linalopigania haki na maendeleo ya kila mtanzania.

Makundi makubwa yanayotajwa katika mnyukanakano huo ni pamoja na kundi la lowassa, samwel sitta, na bernad membe. Kila mmoja anapambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba wanaingiza watu wao muhimu katika vikao vya (nec) na ndani ya jumuiya za chama hicho, uvccm, uwt, na wazazi, katika makundi yote hayo lowassa anaonekana kuwa ni mtu makini ana nafasi kubwa ya kupenya na kupererusha bendera ya chama hicho.

Kusimama kwa lowassa kama mgombea urais ni pigo kubwa kwa vyama vya siasa hasa chadema, cuf na nccr mageuzi. Kutokana na rekodi ya lowassa, ni mtu wa kufuatilia kila jambo analoamini katika dhamira yake kwamba linafaa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni mwenye hulka ya kusaidia na kuchangia shughuli za kijamii bila kujali itikadi za kisiasa wala dini, tofauti na viongozi wengine wa kisiasa amekuwa mtu tegemeo katika shughuli za kijamii iwe za kanisani au msikitini.

Ukitaka kumjua lowassa ni kiongozi wa namna gani, tembelea jimboni kwake monduli ukaone namna alivyowezesha makundi ya vijana na wazee kiuchumi.

kwenu jembe kwetu mtaji
 
Ndugu usilete porojo huo utafiti umeufanyia wapi? na hiyo sample ilikuwa ni akina nani na wapi? nchi hii kwa sasa CCM haipendwi na imepoteza mvuto na hakuna atakaye simama kuiokoa hapo 2015.
Na wewe utafiti wako umeufanyia wapi? naona na wewe unaleta porojo
 
Here is a man who knows which side of his bread is buttered! Ama! Na wewe umeingia kwenye bandwagon ya Lowassa!!!??
 
Kwanini wewe usiende kumfungulia kesi kama ushahidi unao. Kwanini usubiri mkuu wa nchi amkamate wakati hata wewe unayo haki ya kumshitaki?

Ndio maana unampigia kampeni kwakuwa mimi sijaenda kumshtaki? Kha!!

Jaji si kateuliwa na huyo huyo rafiki yake...?ambaye ni mwenzenu. Ni kumkataa tu kama ninavyofanya...hafai!!

bado kumzomea tu atakapojitokeza rasmi kama yule mwenzake....
 
Ndio maana unampigia kampeni kwakuwa mimi sijaenda kumshtaki? Kha!!

Jaji si kateuliwa na huyo huyo rafiki yake...?ambaye ni mwenzenu. Ni kumkataa tu kama ninavyofanya...hafai!!

bado kumzomea tu atakapojitokeza rasmi kama yule mwenzake....
Wewe unasema ni mwizi, leta ushahidi basi sio unaleta stori za vijiweni. Hivi wewe unamjua Lowassa vizuri au ndio unamuona kwenye gazeti, hata hao viongozi wenu kina Slaa wanamsujudia.
 
Tunakumbuka wakati Lowassa baada ya kuhamishwa kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kupelekwa Wizara ya Ardhi na Maliasili alikuta madudu mengi na kuanza kupambana nayo kwa ujasiri mkubwa wa ajabu.

Kulikuwa na wajanja wachache ndani ya halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walitaka kuuza viwanja vya Mnazi Mmoja kwa mfanyabiashara mmoja maarufu, Lowassa alitoa tamko la serikali akiwa bungeni Dodoma akitaka mfanyabiashara huyo aondoke haraka eneo hilo kwa kuondoa uzio alikuwa ameujenga na ndipo wananchi wakavamia na kuchukuwa mapati yote.

Watanzania wanamuitaji "jembe" Lowassa.
 
Sina tatizo na Lowasa, ninatatizo na Msimamo wa Mwalimu Nyerere Kuhusu yeye na Uongozi. Nina wasiwasi na namna watu wanavyomuhusisha na UFISADI. Kuwa ana mali nyingi sana (siwezi thibitisha), kuwa ana tamaa sana ya mali na kumiliki kila kitu. Kuwa ni mtu wa kumwogopa. Nadhani, jinsi haya yatakavyowekwa sawa, kuthibitishwa itatusaidia sisi tusiyo ta ukhibitisho. Siasa wakati mwingine zina fitna, hata hivyo naona kama muda si rafiki kuyaweka sawa ninayoyafikiri.
 
Vipi tena Jembe Zitto Kabwe ndio mnalikana bado mapema namna hii? Zitto angalia hawa ndio mashabiki wako wanaokujazaga ujinga kwamba wewe ndio Jembe lao, waangalie ukiwapa kisogo matendo yao.
Sasa wewe ulita Zitto asisifiwe? Kweli ni Jembe na hakuna atakae weza kumfikia ndani ya chama chenu.

Zitto vs Lowassa 2015 ndio utakua mpambano wa kweli lakini vikaragosi wengine wenu kina Slaa na Mbowe ni kupoteza muda wa uchaguzi tu.
 
Pasco anaweza kuandika kupitia kwa member mwingine? Hii ni kuzima uhuru wa mawazo ya mtu mmoja mmoja.
 
Sasa wewe ulita Zitto asisifiwe? Kweli ni Jembe na hakuna atakae weza kumfikia ndani ya chama chenu.

Zitto vs Lowassa 2015 ndio utakua mpambano wa kweli lakini vikaragosi wengine wenu kina Slaa na Mbowe ni kupoteza muda wa uchaguzi tu.
Hivi kuna mshindani yeyote asiyependa kukutana mshindani dhaifu!? kumbuka hapa ni Home of Great thinker. watu wanasoma between the line, Zitto is dead & buried kuhusu Urais.
 
Wanabodi,

Wakati mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM unaendelea kuanzia ngazi ya shina hadi taifa. Mbunge wa Monduli Edward Lowassa anaonekana kupanda chati kwa kasi ya ajabu na kuonekana ana nafasi kubwa katika mbio za urais 2015.

Uchambuzi wa kisiasa unaonesha karibu kila kona ya nchi hii, katika watanzania 10 utakaowahoji kuhusu ni nani hasa anayefaa kumrithi Rais wa sasa Kikwete, saba kati yao wanamtaja Lowassa wakidai ni "Jembe" linalopigania haki na maendeleo ya kila Mtanzania.

Makundi makubwa yanayotajwa katika mnyukanakano huo ni pamoja na kundi la Lowassa, Samwel Sitta, na Bernad Membe. Kila mmoja anapambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba wanaingiza watu wao muhimu katika vikao vya (NEC) na ndani ya Jumuiya za chama hicho, UVCCM, UWT, na Wazazi, katika makundi yote hayo Lowassa anaonekana kuwa ni mtu makini ana nafasi kubwa ya kupenya na kupererusha bendera ya chama hicho.

Kusimama kwa Lowassa kama mgombea Urais ni pigo kubwa kwa vyama vya siasa hasa Chadema, CUF na NCCR Mageuzi. Kutokana na rekodi ya Lowassa, ni mtu wa kufuatilia kila jambo analoamini katika dhamira yake kwamba linafaa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni mwenye hulka ya kusaidia na kuchangia shughuli za kijamii bila kujali itikadi za kisiasa wala dini, tofauti na viongozi wengine wa kisiasa amekuwa mtu tegemeo katika shughuli za kijamii iwe za kanisani au msikitini.

Ukitaka kumjua Lowassa ni kiongozi wa namna gani, tembelea jimboni kwake Monduli ukaone namna alivyowezesha makundi ya vijana na wazee kiuchumi.
Ungesema kati ya watanzania wana CCM 10 siyo kati ya Watanzania 10. Hiyo ratio ya kimagamba haiapply kwa watanzania wote wenye vyama tofautitofauti na wasio na vyama.
 
Hivi kuna mshindani yeyote asiyependa kukutana mshindani dhaifu!? kumbuka hapa ni Home of Great thinker. watu wanasoma between the line, Zitto is dead & buried kuhusu Urais.
Haya ni mawazo yako au Ya Slaa? Hivi nyie vijana, pamoja na ugreat thinker wenu lini mtaacha kutumika?
 
Back
Top Bottom