Lowassa anaruhusiwa kusaini Petition ya Zitto?

Lowassa anaruhusiwa kusaini Petition ya Zitto?

Nimeona wabunge wa CCM (8) waliosaini kwenye ombi la Zitto atakaloliwasilisha kesho kutaka Waziri Mkuu wa Tanzania apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye, wanapongezwa.

Swali langu kwa wana jamvi wenzangu na Lowassa naye akisaini ataonekana shujaa au ataonekana mlipa Kisasi? Na Zitto amruhusu Lowassa kusaini au asimruhusu? Kwa sababu baadhi ya wabunge waliosaini na kuonekana mashujaa ni walewale miezi kadhaa iliyopita tulikuwa tunawacharura humu ndani kwamba ni "wezi" "mafisadi" na watu wanaolipwa fedha zetu bila ya kufanya kinachotakiwa.

Kila siku tunasema kwamba ndani ya CCM hakuna msafi hata mmoja wote ni mafisadi, Leo inakuwaje Filikudnjombe awe shujaa wakati anatoka CCM?
Kigarama, na mimi naomba nikuulize maswali kadhaa ninayodhani ukiweza kuyajibu, utaweza kutambua hoja yako isivyo na mshiko.

  1. Je, Lowassa, kama hataweka sahihi, utamkubali kwa kuwa msimamo wake ni sawa na wabunge wengi wa CCM ukiondoa hao wanane waliothubutu?
  2. Je Lowassa, kutoweka kwake sahihi, kunamtofautisha vipi na hao wabunge wenzake ambao, kama yeye, wameamua not to walk the talk?
  3. Je Lowassa, kama hataweka sahihi, mwana CCM yeyote ana haki gani ya kutompongeza kama mwanachama mwenzao kwa kuwa na msimamo sawa na wenziwe wengi?
  4. Kila tunaposema CCM wote ni wachafu, wewe na wengine huwa mnapinga kwa kudai si wote, kwa nini basi wanapojitokeza watu kama Mkono, mna"panic"?
  5. Kati ya wale mnaodai ni wapiganaji ndani ya CCM (nina hakika listi unayo) hakuna hata moja aliyethubutu, je na hao mbona huwasemi?
  6. Wako waliokuwa wana CCM lakini wakaamua kwa hiari yao kujitoa na kujiunga na Upinzani, walikuwa vipofu na sasa wanaona, kwa nini wasipongezwe?
 
Tukumbuke kuwa yaliyojitokeza sasa ni yale yale yanayotaka kujirudia yaliyojitokeza kwa Lowasa mpaka leo si PM tena. Kuoneana aibu kunawagharimu wengine kuonekana wachafu wakati ukweli unaonesha kuwa LOWASA hakuhusika na zile kashfa. Ila alikuwa ni mbuzi wa KAFARA TU. Leo hii hawa Mawaziri ambao wanaambiwa kwa MADUDU NA HASARA MLIO ISABABISHIA NCHI HII mnatakiwa mjiuzuru lakini MKUU WA NCHI anawatetea unadhani PINDA ATAKUWA NI NANI KAMA SI MBUZI WA KAFARA?

Akipigiwa kura ya kutokuwa na Imani nae itakuwa ni Historia mbaya sana, aibu kubwa sana kwa PINDA kuanzia kwa familia yake mpaka Tanzania nzima.

Badala ya kufikiria kusign hili karatasi la MH. ZITTO nadhani sisi tungekomaa kutafuta namna gani huyu anayewasababishia wenzake AIBU Afanywe nini na si mwingine bali ni JK.

Mtazamo wangu ni kwamba kwa maana ya saini ni sawa na kura tu kwa hiyo kama ni saini za wabunge tu hata LOWASA ana haki ya kupiga maana kama wewe unasema kakosa MVUTO WA KISIASA ni wewe tu lakini MONDULI huyu ni Mbunge wao na hata kesho ukiweka NANI (TAJA YEYOTE UNAYEMDHANI ANA MVUTO KISIASA) akisimama na LOWASA atapigwa chini vibaya sana.

Tusichanganyane mada hapa, la msingi hawa MAFISADI walioonekana MAWAZIRI waondoke au JK aondoke. SIPO tayari kumwona PINDA AKISULIBIWA KWA KOSA ASILOLITENDA, FIKIRI KAMA UNGEKUWA NI WEWE!!!!!!!!😱hwell:
 
QUOTE=Mag3;3764739][Kigarama, na mimi naomba nikuulize maswali kadhaa ninayodhani ukiweza kuyajibu, utaweza kutambua hoja yako isivyo na mshiko.[/QUOTE]

Mimi sidhani kwa wewe kutokubaliana na hoja yangu basi ndiyo inakuwa haina mashiko. kwanza hii hoja nimetumia mantiki wala sijatumia nini nakipenda au nakiamni. Tatizo wengi wetu tunaamini kwamba kila jambo likisemwa kinyume na vile tunavyofikiri au kulijua basi halina mashiko.

  1. Je, Lowassa, kama hataweka sahihi, utamkubali kwa kuwa msimamo wake ni sawa na wabunge wengi wa CCM ukiondoa hao wanane waliothubutu?

  1. Swali langu haliko kwenye kumkulbali au kutomkubali Lowassa. Bali hoja yangu ilikuja baada ya Filikudnjombe kusifiwa na kuonekana shujaa wakati wengine tunaomfahamu kwa undani tunajua si "mpiganaji" kama wengi wetu tunavyompigia chapuo. Kama Lowassa asiposaini itakuwa ni jambo lake na wapiga kura wake wa Monduli. Kwa nini tunafikiri kusaini ni "kuthubutu" yaani mambo ya kawaida kabisa tunayaita ni kuthubutu!!??
  1. Je Lowassa, kutoweka kwake sahihi, kunamtofautisha vipi na hao wabunge wenzake ambao, kama yeye, wameamua not to walk the talk?

  1. Tofauti yao nadhani hao waliosaini wanaamini matatizo ya nchi yetu yatatatuliwa kwa kumpigia kura ya kutokuwa na Imani waziri Mkuu, lakini inawezekana (simsemei Lowassa) yeye anaamini suluhu ya tatizo liliopo si hili alilolipendekeza Zitto.
  1. Je Lowassa, kama hataweka sahihi, mwana CCM yeyote ana haki gani ya kutompongeza kama mwanachama mwenzao kwa kuwa na msimamo sawa na wenziwe wengi?


  1. Apongezwe kwa lipi? Hata hao waliotia saini wanatakiwa kushutumiwa kwa kosa gani?
  1. Kila tunaposema CCM wote ni wachafu, wewe na wengine huwa mnapinga kwa kudai si wote, kwa nini basi wanapojitokeza watu kama Mkono, mna"panic"?

  1. Mimi sijapanic kwani ni mmoja kati ya watu nisiokubaliana na staili ya uongozi wa Mkono. Staili ya kuleta "maendeleo" kwa kutumia fedha za mfukoni mwake. Pia nikusahihishe kwamba mimi sina "wenzangu" bali hoja zangu nazisimamia mwenyewe. Hivi Mkono Kusaini nimepanic, kivipi nimepanic?

  1. Kati ya wale mnaodai ni wapiganaji ndani ya CCM (nina hakika listi unayo) hakuna hata moja aliyethubutu, je na hao mbona huwasemi?

  1. Tafuta post zangu ambazo nilishawaita wanafiki tangu zamani. Huwezi kutumia mbinu za uvuvi kuendeshea shamba la mahindi. Kama ambavyo siwakubali wajaza jazba walioko CHADEMA na hawa "wapiganaji" ni watu nisiowakubali kabisa.

  1. Wako waliokuwa wana CCM lakini wakaamua kwa hiari yao kujitoa na kujiunga na Upinzani, walikuwa vipofu na sasa wanaona, kwa nini wasipongezwe?
Hoja yangu ni kwamba ni lazima tujuzane kama tatizo ni watu au mfumo na ndiyo maana nikatolea mfano wa Lowassa. Kama leo Lowassa akijiunga na CHADEMA atasafishika kwa kujiunga tu na CHADEMA!!
 
Sitajibu hoja zako zote kwa sababu naamini katika hii vita iliyo mbele yetu kama taifa hatutakiwi kuwa watazamaji, hatutakiwi kuwa wasindikizaji na hatutakiwi kuwa wanafiki. Kama uliona michango ya wabunge wa CCM kabla hawajalikacha bunge na kwenda kujifungia kwenye kikao kama cha wanywa kahawa utanielewa. Wapo waliokuwa wanatoka povu utadhani wako tayari kumpigia Raisi kura ya kutokuwa na imani naye, kumbe...! Mheshimiwa Zitto kawapa njia nyepesi ya kutokea, nayo ni ya kumwajibisha Waziri Mkuu, kiongozi pekee wa serikali ambaye walishiriki katika uteuzi wake kama wabunge. Ghafla, tofauti na ilivyotegemewa na wengi, wakajitokeza katika rangi yao halisi ya la kinafiki, eti kuwalazimisha mawaziri kujiuzulu...! kwani bunge linawateua mawaziri?

Tofauti yao nadhani hao waliosaini wanaamini matatizo ya nchi yetu yatatatuliwa kwa kumpigia kura ya kutokuwa na Imani waziri Mkuu, lakini inawezekana (simsemei Lowassa) yeye anaamini suluhu ya tatizo liliopo si hili alilolipendekeza Zitto. Hoja yangu ni kwamba ni lazima tujuzane kama tatizo ni watu au mfumo na ndiyo maana nikatolea mfano wa Lowassa. Kama leo Lowassa akijiunga na CHADEMA atasafishika kwa kujiunga tu na CHADEMA!!
Tatizo kuu linalotukabili kama taifa ni mfumo lakini huo mfumo ni kwa sababu unasimamiwa na watu ambao wako tayari kuutetea kwa kila hali kwani wanafaidika nao. Kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni hatua mojawapo ya mwanzo na muhimu sana katika kuufikisha ujumbe kuwa pamoja na yote, mfumo haukubaliki. Hapa ndipo panatakiwa watu wa kusimama ili wahesabiwe na kwa mbunge wa CCM, ukubali usikubali, ni ujasiri usio wa kawaida unaohitaji kupongezwa. Haijalishi mtu alikuwa mtuhumiwa, ingawa na hilo linaweza kuzusha swali la kwa nini mtu huyo, pamoja na tuhuma zote hizo, bado yupo hapo alipo bila kuwajibishwa! Kigarama, ungekuwa mbunge, je ungemwaga sahihi kwenye hoja?
 
Last edited by a moderator:
Kigarama, ungekuwa mbunge, je ungemwaga sahihi kwenye hoja?
Definetly nisingesaini kwani najua tatizo si Waziri Mkuu bali ni yule aliyemteua yeye na hao mawaziri wenzake. Kama watu tuko makini hata kesho tukitaka kufanya mabadiliko ni lazima tuongelee kumuondoa Rais Madarakani na CCM yake. natofautiana na wengi kwa kudhani kuiondoa CCM madarakani ni kuwashawishi "wapiganaji' waliioko CCM kujiunga na CHADEMA kama vile walioko CHADEMA hawatoshelezi kuleta mapinduzi ya kweli nchini. Wala siamini kuiondoa CCM ni kusema sema bila kufanya kazi ya ziada kuelimisha (siyo kwa mikutano ya hadhara) wananchi wa kawaida nchini.

Napingana na wote wenye mawazo kwamba CCM haikubaliki kwa sababu haina wasomi au CHADEMA inakubalika kwa sababu wana wasomi wengi. CCM haitaondoka kwa kusema maovu yake bali kwa kuyathibitisha kwa wananchi na kutoa njia za kuondokana na maovu hayo.
 
Back
Top Bottom