Lowassa anaruhusiwa kusaini Petition ya Zitto? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa anaruhusiwa kusaini Petition ya Zitto?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Apr 22, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nimeona wabunge wa CCM (8) waliosaini kwenye ombi la Zitto atakaloliwasilisha kesho kutaka Waziri Mkuu wa Tanzania apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye, wanapongezwa.

  Swali langu kwa wana jamvi wenzangu na Lowassa naye akisaini ataonekana shujaa au ataonekana mlipa Kisasi? Na Zitto amruhusu Lowassa kusaini au asimruhusu? Kwa sababu baadhi ya wabunge waliosaini na kuonekana mashujaa ni walewale miezi kadhaa iliyopita tulikuwa tunawacharura humu ndani kwamba ni "wezi" "mafisadi" na watu wanaolipwa fedha zetu bila ya kufanya kinachotakiwa.

  Kila siku tunasema kwamba ndani ya CCM hakuna msafi hata mmoja wote ni mafisadi, Leo inakuwaje Filikudnjombe awe shujaa wakati anatoka CCM?
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  .. and I have that feeling that he is going to do it soon .. anybody to challenge him ?
   
 3. mazeea1

  mazeea1 Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 24, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  pole sana sana! CCM wote mafisadi? basi ukiwa nje ya nchiunaweza sema watanzania wote ni wezi! ufikirie kabla ya kuandika jaman! mambo hayani mazito... yanaeda mbali kuliko uanachama wa kisiasa, ni mambo ya kitaifa!
   
 4. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Umetumia hisia (emotion) kujibu hoja yangu. Humu kila siku tunasema CCM ni mafisadi lakini leo tunawapongeza wana CCM waliosaini hoja ya Zitto, na ndiyo hoja yangu inapokuja kama na Lowassa naye anaruhusiwa kusaini na jee Zitto amruhusu kusaini kwa niaba ya wananchi wa Monduli?
   
 5. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  kwani yeye sio Mbunge..?, hata Pinda mwenyewe akitaka, Ruksa
   
 6. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Kisheria Lowassa anaweza kusign. Issue ya ataonekana analipa kisasi sidhani km itaonekana hivyo kwani si Pinda aliyesababisha ajiuzulu. Ni tuhuma alizokuwa nazo
   
 7. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tunakumbuka mabilioni aliyolipwa Mkono kwenye ile issue Valambhia? Tunajua kwamba Filikundjombe alimhujumu mgombea wa CHADEMA 2010. Hoja ya usafi wa wabunge wa CCM imekufa?
   
 8. N

  Njangula Senior Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utaifa kwanza ndugu yangu. Naishi jimbo la Filikunjombe kikazi, matumainh ya wananchi juu yake yameongezeka kwani alikuwa ktk probation. Kutokana na mkwara wa Lukuvi, ni vema kumwita shujaa mbunge yeyote wa CCM aliyethubutu kusaini.
   
 9. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kigarama,
  Swali lako ni zito na lenye mantiki sana.
  Ninachokiona hapa ni kutokana na utamaduni wa bunge wa kupiga kura ya sema ndiyo au hapana.
  Inapofikia hapo ni ngumu sana kujua nani amesimama wapi. Watu wanajificha nyuma ya sauti za ndiyo na hapana.

  Karatasi hii inaweka wazi nani yupo wapi katika masuala yanayoligusa taifa hili na hasa umasikini.
  Wale wanaosaini haina maana ni mashujaa, la hasha! ila wao wamejiweka wazi wapi wanasimama.Wala haina maana kuwa wapo sahihi, hata wale waliokataa kusaini wapo sahihi. Kwa mfano, January Makamba amesema hii ni ' ngazi ya kisiasa' kwa hiyo hata saini.

  Maana yake ni kuwa yeye ameweka siasa mbele kuliko masilahi ya umma. January Makamba amesahau kuwa alipotoa hoja ya kuwabana wenye nyumba wasitoze kodi kwa mwaka ilikuwa ni ngazi ya kisiasa. Anafahamu kuwa sheria pekee hazizuii uhalifu. Jambo zuri basi tumemjua yupo wapi ukilinganisha na Anne Kilango ambaye kimsingi anapinga ufujaji na ubadhirifu(patachimbika hapa bungeni) lakini kwa hili hatujui anakubaliana nalo au hakubalini. Hatujui anamwonea huruma PM kwa urafiki w kisiasa au anaona kuna tatizo. All in all watu wa aina hii ndiyo tunatka tuwajue tu!

  Kinachotakiwa hapa ni mtu kuhubiri kile anachosfanya. Ule usainii wa kuwa mkali na mwisho kusema naunga hoja mkono ndiyo unafiki kama wa akina January. Sasa ni wakati 'walk the talk'
  Karatasi itasaidia sana kujua wanafiki. Mnafiki ni yule tusiyejua ima ni mnyama au ni ndege (popo).
  Narudia hata asiyesaini yupo sahihi, ila atoke na kusema sikusaini. Kinachotafutwa ni kundi la 'tatu' yaani kundi la wanafiki hili ndilo tunataka tulijue. Ukisaini au usiposaini tukakujua wewe huna tatizo. Tatizo kama hutujui upo wapi.

  Kuhusu Lowassa, ningekuwa mshauri wake ningesmshauri asisogelee hiyo karatasi. Lowassa ana haki kama mbunge though! tatizo ni kuwa EL amechafuka sana na kwamba hakuna atakachokifanya umma umwelewe au umwamini.
  Hana moral authority yoyote ya kusema hiki ni kizuri kile ni kibaya. Amepoteza public trust kiasi kwamba umma unaona akishika dhahabu itageuka kuwa mavumba, akipewa keki ghafla itakuwa samadi.
  Lowassa has nothing to lose on this, he is a loser ab initio hence he doesn't need to spark the fire.
   
 10. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nguruvi3 nimeupenda uchambuzi wako siyo wale wamezoea kujibu hoja kishabiki. Kiukweli Lowassa amepoteza imani sana kwa wananchi kiasi kwamba hakuna atakachokifanya kikaonekana chema. Nimeipenda hoja ya kutafuta wabunge wa kundi la tatu ambao hawajulikani wamesimamia wapi kwenye hoja hii.
   
 11. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Mkuu kutokana na mfano wako kama nimekuelewa yaani mfano nyumba inaungua moto, na watu wote wapo ndani does it mean utakataza baadhi ya watu wasizime moto sababu ndio walioanzisha moto..? (huoni kwamba huko kutakuwa ni kujiua wote ?)

  As the case of Ushujaa hapa hakuna Shujaa they are doing their jobs (which has been long overdue), tena nashangaa walikuwa wapi miaka yote (anyway better late than never). Hata kama motives zao ni mbaya, kama wanatenda jambo zuri hatuwezi kuwakataza sababu ya their ill-motives
   
 12. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  unajua kuwa upo jukwaa la siasa?
  This is purely a political move.Lowasa haitaji kusaini, hakubaliki.
   
 13. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hoja iliyoko ni ya wabunge kuchukua upande!hata mbunge wa CDM asingeweka sahihi tusingehukumu chama chake!
   
 14. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Agenda ya Zitto inahitaji saini. Sidhani kama itakuwa busara kubagua, hata Pinda akitaka atapewa asaini haina tatizo. unapoanzisha vita una kuwa na shabaha kwa adui mmoja, hujengi maadui wapya, ndio dhamira ya zito kupata saini. Kumbuka kuwa mwisho wa siku atahitaji kura ya kila mmoja ukimtenga sasa atasusia. Nadhani zitto analijua hilo
   
 15. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nguruvi3 mimi napingana na wewe kuhusu lowasa,mi maoni yangu ni kwamba,licha ya lowasa kuchafuka,tena si kuchafuka bali kujichafua lakina anakila sababu ya kusogerea karatasi.kwanini nasema hivyo,...kwa kua lowasa ni mbunge anaye wakilisha watu natakiwa afate maslah ya umma,kama alivyo wajibika kujiuzuru (mwenyewe sikuizi anasema maamuzi magumu)na ndivyo anatakiwa awajibike sasa,kumbuka yupo pale kwa ajili ya wananchi waliomchagua,anawatumikia anawajibu tena wakusaini sio kusogelea tu.filikunjombe anasema sio mimi niliosain bali wanaludewa,afanze maamuzi mazito ya kusaini ambayo kwangu ni maamuzi sahihi,na kama ajasaini inatakiwa wananchi wa jimbo lake wamuhoji tena haraka
   
 16. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kobelo kumbuka lowasa ni mbunge,ingawa haaminiki na hata mimi simkubali lakini lowasa anapaswa kusaini au atoe tamko kuwa hasaini kwa sababu frani,kwanini,kwakua pamoja na kutokuaminika kwake lakini ni mbunge huyu wa kundi flani/jimbo.na kanuni aziitaji kura za msafi au mchafu,inaitaji kura ya mbunge yoyote yule.sasa kama uchafu ni kigezo cha kutokupiga kura bas ajiuzuru hadi ubunge
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kama kasaini Mkono ambaye yumo kwenye" list of shame" kaitwa shujaa na watu wamesahau kama alipwa na BOT dola 998,000.

  Lowassa nae akisaini ataitwa shujaa kachagua upande wa historia.
   
 18. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ritz,wewe unapendekeza lowasa asaini au asisaini?na kama asaini au asisaini tueleze kwanini
   
 19. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  May I ask...,
  Hivi kinachotakiwa na sahihi za wabunge wasafi / mashujaa au sahihi za wabunge ?

  Nadhani hapa kinachotakiwa ni number na sio nani kasign, kila sahihi ina uzito sawa ingawa za wengine kutokana na convincing power yao zinaweza zikapelekea wengine wengi wasign (hence hizo ndio nzuri zaidi)
   
 20. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nasubiri majibu yako mkuu
   
Loading...