mwana wa mtu
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 220
- 53
Kwa upande wa Lowasa, naweza kusema ni mkakati mzuri hasa katika harakati zake za kuponya majeraha ya kutemeshwa uwaziri mkuu. Ni mchezo wa kisiasa, ni sehemu ya Propaganda, Propaganda siyo dhambi alimradi humshurutishi mtu.
Kwa upande wa CCM, hii ni dalili mbaya kutokana na kuwa inajidhihirisha kuwa Lowasa amepoteza matumaini na Mwenendo wa chama chake, na kama raia yeyote basi anaitumia haki yake ya kimsingi kujijengea mustakabali mzuri iwapo mambo yatakuwa mabaya CCM. Ni wajibu wa CCM kuliona hilo na kulifanyia kazi ilhali bado mapema. Wasipuuze.
Kwa upande wa CHADEMA, kama Lowasa ameamua kujipenyeza kwao, wasimfukuze, wamkaribishe hata kama anakuja kama mpelelezi. Wanachopaswa kufanya ni kujitengenezea namna watakayoweza kumtumia Lowasa indirectly ili ku-achieve malengo yao, ya muda mfupi na hata muda mrefu. Pia wakiwa na kitengo kizuri cha intelligence naamini kabisa yapo watakayoweza kujifunza kutoka kwa Lowasa, mradi wahakikishe hawampi nafasi ya kujipatia wafuasi wasio waaminifu. Ni juu ya CHADEMA na CCM kuwa makini namna ya kudeal naye. Agalau huo ni msimamo wangu kama kweli Lowasa anacheza mchezo huo...
Mimi nadhani Lowassa ana plan B. Anajua asipopata kupitia CCM na ikiwa CHADEMA watachukua dola kutakuwepo na vilio vya kutaka asulubiwe kwa ufisadi wake. Sasa hapa lazima viongozi wa Chadema wawe be careful kwa sababu huyu anaweza kuwa compromise ili asichukuliwe hatua zozote ikiwa kutakuwepo mabadiliko ya utawala. Nisingepokea msaada wake au urafiki wake.Issue hapa siyo hiyo unayosema wewe. Huyu mtu ni sumu kubwa kwa watanzania, popote atakapohamia. Siyo mtaji wowote wa kisiasa kwa vile yeye ndiye chanzo cha matatizo yote haya ambayo yanatukabili na kujivua gamba lake ili awahadae watanzania kwamba yeye ni safi ndicho tunachokikataa. Yeye ndiye anayehusika na shida za watanzania ambao leo anajifanya kuwakimbilia na kuwatetea au kuwaonea huruma. Hii ni dalili mojawapo ya mnafiki.
Wana JF,
Kuna habari zinaendelea kunong'onwa chini kwa chini kwamba Edward Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa lazima hivi sasa anatoa support kwa pande kuu mbili zinazopingana kisiasa CCM- ianyoongoza serikali rasmi na CHADEMA inayoongoza serikali nje ya ofisi.
Taarifa zilizopo zinajikita katika hoja zifuatazo;
1. Kwa kipindi kirefu Lowassa amejionesha, na anaendelea kujionesha kuwa bado ana nia ya dhati ya kuja kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais, na kwa kuwa kwa sasa inaadaiwa anapima upepo, ameanza kutoa support kote kuwili ili kuweza kujenga future yake-hata kama si kwa urais.
2. Wanadai hivyo wanasema pia kuwa kwa kipindi kirefu haijanukuliwa au kusikika Lowassa akiwashambulia CHADEMA waziwazi, na hata kwa uficho, ukiachia mbali Chadema waliweka mgombea wa ubunge kwenye jimbo lae, lakini hajawahi kuwa-deal uongozi wa juu wa Chadema kuhusu hilo...
3. Ukiachia mbali kuwa kwa sasa amekuwa akitoa matamko mengi yanayokinzana na misimamo ya CCM, ingawa yaweza kutazamwa kama uleule mkakati wake wa kurejea kwenye safu na kujipanga, lakini mengi ya matamko haya yanadaiwa kuwa kwa namna moja ama nyingine kwenda sambamba na misimamo ya CDM; mfano suala la katiba, tahadhari kuhusu Arusha kabla ya maandamano, jana kaibuka na suala la mishahara ya wafanyakazi..na mengine kama mnakumbuka..
Ni kwasababu ya hizo hoja, inadaiwa kuwa kumekuwa na juhudi fulani anazifanya ama zimeshafanyika, za kutoa support kwa CDM katika shughuli zake, bila kusahau kuwa bado yuko kwenye chama chake CCM akiwa damu damu na huku akiungwa mkono na wengi sana kwenye vikao vikuu na ambao ndio tumaini lake hapo baadae.
Maswali ni je, kama habari hizi ni za kweli, kuna athari gani kwa pande zote mbili,..na hasa CHADEMA ambako mtu kama huyu itakuwa ni maajabu kuwa na 'link'...tafadhali tujadiliane hili.
Kuna haya maneno niliyoya bold hapa chini:
ni wakina nani wapo nyuma ya hizi bold nlizoweka..???:thinking::thinking::thinking:

Watanzania wenye nia, nguvu, uadilifu na elimu ya kutosha, mtazamo chanya, wenye kupenda wanachi, kumuogopa Mungu watakapoisha, au kugoma kugombea urais, nitampa kura yangu Lowasa!!