mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
UKIWAAMBIA wanasiasa kuwa siasa ni uongo hakuna mwanasiasa atayekukubalia na watakachokuambia ni kuwa siasa si uongo ila wanasiasa ndio waongo, lakini tunaachaje kusema siasa ni uongo wakati yatokayo vinywani mwa wanasiasa wengi huwa ni uongo?
Kipindi cha kampeni tulisikia mambo mengi lakini moja lililosikikika sana ni kuwa “MsimchagueLowassamaanani fisadi” zilitumika propaganda nyingi kuelezea ufisadi wa Lowassa na sikushangaa kwa nini CCM walikuja na ajenda ya Mahakama ya Mafisadi hii yote ilikuwa ni katika kujaribu kuelezea kuwa Lowassa ni fisadi na hafai.
Wakati kampeni zinaendelea watu mbalimbali ama kwa utashi wao au kutumika walizunguka kwenye vituo mbalimbali vya habari kuelezea kwa nini Lowassa hafai, wapo walioonekana wametumwa na chama na wapo walioonekana kujitolea lakini hatuwezi kuthibitisha hili.
Sasa ni mwaka na miezi kadhaa tangu Serikali hii iingie madarakani sasa naomba kuwauliza ufisadi wa Lowassa umekwisha? Siku za nyuma hapa nilisikia kauli ya kushtua kidogo kutoka kwa mheshimiwa mmoja kuwa Mahakama ya Mafisadi imekosa kesi maana tangu Serikali hii iingie madarakani wizi umepungua.
Kila ninapokumbuka masuala kama haya siachi kusema siasa ni uongo, maana yake chama chochote na wanachama wake wote wanamsahau vipi mtuhumiwa mmoja? Ina maana pamoja na kutumbua kote majipu wamemsahau Lowassa waliyemtaja kama fisadi kwa zaidi ya siku hamsini, haikutosha hata wakati Rais Magufuli anakabidhiwa uenyekiti wa chama Mzee Makamba alizungumza tena kuhusu Lowassa ina maana wanasahau au wanajisahuulisha? Au ndio tuseme Lowassa huwa fisadi kipindi cha uchaguzi tu ukishaisha anakuwa msafi?
Katika kumbukumbu zangu sijawahi kuona mtuhumiwa au mshukiwa wa kashfa kubwa kama Richmond akawa na jeuri, maana mara zote alizokuwa akituhumiwa aliwaambia wanaomtuhumu kama wanao ushahidi kuhusu wizi wake waende mahakamani na sijamuona mtu yeyote awe kiongozi wa nchi au wananchi wa kawaida akienda mahakamani, hii ni sawa na kusema Lowassa hahusiki na Richmond na si kashfa hiyo tu bali na nyingine zote hivyo jina lake hutumika kisiasa kumchafua huku wao wakinufaika kisiasa na si fisadi bali anakuwa fisadi inapofika kipindi cha uchaguzi.