Lowassa anakera, Tambwe ni pigo kubwa kwa CCM

Lowassa anakera, Tambwe ni pigo kubwa kwa CCM

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kuna mambo mawili yananikereketa wakati kampeni zikiendelea. Mambo hayo mawili yanawahusu wanasiasa wawili: Edward Lowassa na Hiza Tambwe. Lowassa amekuwa akitukera CCM kwelikweli. Hachokozeki. Anarushiwa dongo, anakwepa. Anakashfiwa, ananyamaza kimya. Hahami kwenye hoja zake. Anakera kweli yaani. Hata timu ya kampeni sasa inapoteza dira. Ilipanga kujibizana naye.

Anavyonyamaza, anawakosesha wanatimu cha kusema ili kuendeleza kilichopangwa. Huyo ni wa kwanza. Wa pili ni Hiza Tambwe. Tulimpokea Tambwe humu chamani, CCM, na kuwa naye kwa miaka tisa. Tulimsajili toka CUF. Hiza Tambwe, kutokana na uzoefu wake wa kisiasa, hasa kusema maneno yanayochoma, aliaminiwa haraka CCM. Akawekwa kwenye Kitengo cha Propaganda.

Hata timu ya Vijana wapambanaji mitandaoni, luningani na magazetini, katika utetezi wa chama ilikuwa chini yake. Tambwe alikuwa mbunifu wa mambo mbalimbali ya kipropaganda kukilinda na kukisafisha chama. Tambwe amefanya kazi ya kutukuka ndani ya CCM. Kuondoka kwake kwenda UKAWA ni pigo kubwa kwa CCM. Tambwe ni Master of propaganda. Ametuacha wakati mbaya sana. Hatukutegemea.

Lowassa anakera, Tambwe amekwenda kuongeza na kutangaza sera. Mwaka huu tukitoboza, tutakuwa 'watakatifu'!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Shida ya UKAWA hawajui namna ya kumtumia huyo Tambwe. Tambwe sio wa kumshirikisha vikao vya ndani, ananunulika.... lakini ni wa kumpa vya kuongea hasa majukwaani, anaweza kuwafanya watu wamsikilize
 
11953220_917545874971987_919564406648940005_n.jpg11951820_917545884971986_7987352058551855363_n.jpg
hapa naona wanahutubiana wenyewe kwa wenyewe
 
hahahahaaaaa VUTA-NKUVUTE kumbe ndio ilikuwa mipango yenu....yaani aseme na njie mmwagiike?? SASA tumepata mtu wa kutusemea hayo ya Serikalini............................SUMAYE, ye yuko special kujibu hayo.
 
Last edited by a moderator:
..aisee poleni sn hamna jinsi,kwani huko kwenu hamkuwa na sera? sera yenu ilikua lowasa lowasa lowasa hahaa mmeula wa chuya!
 
..mnaweza kutuboza ila sipati picha hayo makovu mtakayo toka nayo,sijui km sura zenu zitatazamika tena!
 
Watu nafikiri HAKUNA sehemu Sumaye alisema ""LOWASA AKIPITISHWA NA CCM"" hakuna...ila alisema "CCM ikimpitisha mla Rushwa yeye angejuiondoa""

Na kweli amejiondoa CCM...kajiunga UKAWA na Lowasa, sasa jiulize, nani MLA RUSHWA kati ya Lowasa na Magufuli ambaye Sumaye alikuwa anamzungumzia.
 
Last edited by a moderator:
Ama kweli ulimi ni kiungo kidogo tu ila kina weza kukugharimu.
Mpango wa kuiondoa Ccm madarakani ulianza kitambo na hao unaowaona tulianza kuwatumia toka wakiwa ndani ya Ccm, Kwahyo hayo uliyoyaona ni moja kati ya mbinu tuliyoitumia na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwavuruga
 
Shida ya UKAWA hawajui namna ya kumtumia huyo Tambwe. Tambwe sio wa kumshirikisha vikao vya ndani, ananunulika....lakini ni wa kumpa vya kuongea hasa majukwaani anaweza kuwafanya watu wamsikilize
Mkuu tumekusikia.
Tunalifanyia kazi.
Ntalifikisha mahala husika hili suala
 
Na huyu unamjua?

Mkuu Watu, pale hotelini wakati Sumaye anatangaza nia mimi nilikuwepo. Hakumtaja Lowassa hata mara moja. Huu ni upotoshaji wa makusudi wa taarifa na habari. Kama makada,wakati huu tuuepuke uzushi na upotoshaji

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom