Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 781
Chama cha Wananchi CUF, kipo kwenye mgogoro mkubwa wa kiutawala uliosababishwa na kurudi kwa prof Lipumba kwenye uenyekiti wa chama hicho.
Prof Lipumba alijihudhuru nafasi ya Uenyekiti kwenye Chama cha wananchi CUF mnapo tarehe 5/8/2015 kwa madai kuwa dhamira yake inamsuta kushirikiana na mheshimawa Edward Lowassa katika uchaguzi wa 2015, Hivyo ameamua kuachia ngazi na yeye angebaki kama mwanachama wa kawaida,uchaguzi wa 2015 hakufanya kampeni hata chembe.
Prof lipumba ametumia mapungufu ya kikatiba yaliyofanywa na Aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Maalim seif na kamati ya uongozi wa muda chini ya mwenyekiti Julius Mtatiro kutopeleka mabadiliko kwa msajiri mkuu wa vyama vya siasa pamoja na barua yake kutojadiliwa na kamati kuu kijirudishia nafasi yake ya kuwa mwenyekiti tena wa chama hicho.
Kurudi kwa mara nyingine kwa prof Lipumba kumeleta mpasuko mkubwa kwenye chama hicho, ikiwepo kumwondoa Aliyekuwa Katibu mkuu Mheshimwa Maalim Seif na kumteua mbunge Magdelina sakaya kuwa katibu mkuu mpya kitu kinachoongeza mpasuko mkubwa na kuna dalili zote za chama hicho kukosa ushirikiano baina ya wanachama wake wa bara na wa zanzibar.
Mgogoro huu wa Cuf unamadhara mawili juu ya maendeleo ya ukawa. Kwanza kuna kila dalili ya chama cha CUF kuweza kujiondoa ndani ya Ukawa, hii inatokana na prof Lipumba kutoona faida ya ukawa kwa Cuf, pili ukawa kukosa makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja mmoja kwa kila jimbo ili kutoa nafasi kwa wao kuchukua majimbo mengi kama tulivyoshuhudia uchaguzi wa 2015, hivyo kutapelekea Wapinzani kupoteza baadhi ya majimbo.
Mgogoro huu ni pigo kubwa kwa wapinzani unatakiwa utatuliwe, kukimbia mazungumzo au kumsusia Lipumba chama ni kujihatarishia ushindi katika ngazi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao. Wapinzani wajikite kuutafutia ufumbuzi kuliko kurushiana vijembe kwenye vyombo vya habari. Mgogoro na kuvunjika kwa Ukawa furaha kwa CCM