Lowassa amtwisha zigo Waziri Nundu

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
Lowassa amtwisha zigo Waziri Nundu


Patricia Kimelemeta

KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, imemtaka Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu, kuwasilisha barua ya kupinga ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa eneo la Taveta, Kenya kwa sababu umekiuka mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Hatua hiyo imefikiwa baada kamati hiyo jijini Dar es Salaam jana, kujadili suala la Ulinzi na Usalama kupitia Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, alisema kitendo cha Kenya kujenga kiwanja hicho karibu na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), ni kwenda kinyume na mkataba wa EAC na Tanzania haijatendewa haki.

“Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, namtaka Waziri wa Uchukuzi, kuwasilisha pingamizi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki kupinga ujenzi wa kiwanja cha ndege, kwa sababu umekiuka sheria na taratibu za makubaliano,” alisema Lowassa. Aliongeza kuwa eneo hilo kuna kiwanja cha Kia, hivyo huwezi kufanya uwekezaji wa aina moja eneo hilo na kwamba, hiyo sawa na kuvunja makubaliano hayo suala linaloweza kuzusha mgogoro.

Lowassa alisema kutokana na hali hiyo, waziri anatakiwa kuwasilisha taarifa yake kwenye kamati hiyo atakapotekeleza agizo hilo, ili wajumbe wa kamati na wabunge wa EAC waweze kupata taarifa.

Kutokana na hali hiyo, kamati hiyo inatakiwa kusubiri taarifa kutoka kwa waziri nwenye dhamana ili kuendelea na hatua stahiki ya pingamizi hilo. Akichangia hoja, Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa, John Shibuda, alisema serikali isipokuwa makini kwenye suala hilo, Tanzania itakuwa jamvi la wageni.

“Tanzania ni jamvi la wageni sasa, watu wanatoka huko waliko na kukimbilia huku, niwaambie laiti hayati Mwalimu Julius Nyerere angekuwa hai, angetuchapa viboko kwa sababu sisi ndio tunaotetea maslahi ya wananchi wetu, lakini ndio wa kwanza kukubali mambo kama haya,” alisema Shibuda.

Hata hivyo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alisema wizara yake inatengewa bajeti ndogo ambayo inafanya washindwe kutekeleza majukumu hayo ipasavyo. “Bajeti iliyopita ya wizara ni Sh3 bilioni, ambazo huwezi kufanya shughuli yoyote ile ikilinganishwa na wizara yenyewe ni nyeti, kutokana hali hiyo tunaomba serikali kupitia kamati hii iweze kutuongezea fungu,” alisema Sitta. Mwisho
 
are you serious!!! budget 3billion, yani hata Chenge anaweza aka subsdize hii wizara kwa miaka nane (25,000,000,000/3 = 8 years
 
boresheni kia, shusheni gharama za kutua ndege na muwaambie bodi ya utalii ifanye kazi ya kutangaza nchi na sio viini macho vya kubandika picha kwenye basi moja london na kusimama mbele ya hilo basi na kupiga picha kisha mnaweka kwenye michuzi na kusema mnatangaza utalii.
wenzetu kenya wanaweka matangazo kwenye mainstream tv stations tena prime time
 
this is the point. Lowaa you are talking though hutakuwa rais

hata aongee nini hastahiri kuwa raisi,this is not a perfume to make him smell like an angel!

It's too late hata hivo,wanajua uwanja umefikia wapi sasa?

Walikuwa wapi wakati kenya wako hatua za mwanzo kujenga kiwanja hiko?

Wanadhani kenya ni wajinga kukubali kupoteza hela kibao walizo kwisha tumia kujenga kiwanja leo hii?

na bado,tutakuja gundua kenyans are feeding on us tukiwa tumebaki mifupa
 
Mh Lowassa watu walishaongea sana Kuhusu KIA lakini umekaa kimya. Sasa hivi unakuja na strategy ambao ni late counter attack. Kwa maana kwamba maandalizi yote ya uwanja wa TAVETA ulishaanza kujengwa.

Ina maana viongozi wote hapa Tanzania ni vipofu?? Walikuwa hawasikii TATO, KIATO na watu wanasema Tariffs za KIA sishushwe ili kumudu ushindani na Jommo Kenyatta Airport.

Kwanza hata kabla hiyo TAVETA haijajengwa, Jommo Kenyatta Airport ya Nairobi imeshateka soko la Africa Mashariki.

Kama 80% (let say) ya watalii wanaokuja Tanzania kupitia Arusha au kupanda mlima wanapitia Kenya halafu wana connect to Tanzania via Bus Shuttles na Kenya Airways/PW.

Mfano kuna shuttles kama Riverside Shuttle, Davanu, Impala Shuttle, Rainbow,Bobby Shuttle na nyingine hao wote wanapiga biashara ya kusomba watalii Jomo Kenyatta Airport kuwaleta Tanzania.

Nawashauri Lowassa, Sitta na Omari Nundu wafanye haya Kwanza kabla ya kuwa atack kenya. Maana kenya waliona tumelala ndo maana wanaanza kujenga Airport TAVETA.

- Kuwashauri wizara ya Fedha, Wizara ya uchukuzi na Wizara ya mali asili/utalii kuboresha uendeshaji wa KIA, Kushusha landing tarrifs ili ndege nyingi zaidi kutua KIA. Kushusha bei ya mafuta ya ndege. n.k

Kwa hiyo naomba kama kuna mtu anaweza kuwafikishia huu ujumbe ili hao waheshimiwa waanze na kuboresha KIA Kwanza.

Uwanja wa KIA ungekuwa na vivutio na uendeshaji mzuri then hao wakenya wasingepata wazo.

Hey Tanzania wake up...!!!
 
Lowasa alikuwa wapi siku zote?Hili suala la huu uwanja tumeshalijadili sana.Hebu mods unganisheni hii thread na ile ya zamani tuliojadili kule kwenye jukwaa la kimataifa
Uwanja wa ndege Taveta,means KIA itakufa.Kenya watajinufaisha kupitia raslimali zetu,it's against Intergration spirit
 
kuboresha airport pamoja na barabara. I think it is high time we have two lane roads frm KIA To ARUSHA-MOSHI. Tuone umuhimu wa kuboresha arusha kwa kuwa na miundo mbinu ya barabara ama sivyo tutakuwa tunalalamika tu siku zote bila kujua ni kwa nini tunapoteza kwenye ushindani
 
kuboresha airport pamoja na barabara. I think it is high time we have two lane roads frm KIA To ARUSHA-MOSHI. Tuone umuhimu wa kuboresha arusha kwa kuwa na miundo mbinu ya barabara ama sivyo tutakuwa tunalalamika tu siku zote bila kujua ni kwa nini tunapoteza kwenye ushindani

Nadhani unamaanisha dual carriage way maana hiyo barabara tayari ina two lanes. Kwani traffic volume ipo kubwa ivyo mpaka kuhitaji dual carriage way!
 
Lowasa na kamati yako acheni kufanya maamuzi ya kijima. Hivi hata kama mko kwenye Jumuiya ya A. mashariki ina maana ninyi kama Tanzania mkiamua kujenga uwanja mwingine wa kimataifa Mwanza, Dodoma, Kigoma, Mbeya au Mtwara mnahitaji kukubaliwa na nchi nyingine? Kenya ni nchi huru na ni haki yake kuongeza huduma hizo za usafiri ili kuwarahisishia wananchi wake na pia kuvuta wageni kutembelea Kenya na hivyo kuongeza pato la nchi. Tanzania mmelala tu mnatarajia na wenzenu walale? Hivi uwanja wa KIA unaweza kuuita ni wa Kimataifa? Acheni porojo kwenye mambo ya maendeleo. mmekalia kuwekeza kwenye mifuko ya mafisadi badala ya kuwekeza kwenye miundo mbinu kama wanavyofanya jirani zetu Kenya.
 
Lowassa amtwisha zigo Waziri Nundu
Mwenyekiti wa kamati hiyo, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, alisema kitendo cha Kenya kujenga kiwanja hicho karibu na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), ni kwenda kinyume na mkataba wa EAC na Tanzania haijatendewa haki. [/QUOTE]

Kama kuna makubalioano hayo katika EA treaty, basi huu umoja haufai kabisa na hakuna haja ya kuendelea nao. Yaani Wakenya eti wasiendeleze Kenya yao kwasababu sisi Watanzania tumelala? (read tumeshindwa kuendeshakwa ufanisi KIA kibiashara, tumeshindwa kujenga Uwanja wa ndege wa kimataifa Mwanza as a gate away for north-western corridor.

Haya ndiyo yale yale eti kutumia maji za Lake Victoria kwaajili ya watanzania tuombe kibali Egypt. Kama tunakataa hilo la Waegypt kwanini tunataka kuwakata Wakenya kujenga uwanja ktk ardhi yao TAVETA. haya ni makubaliano ya kijinga kama ya Nile basin treaty, hayatakiwa kuwa enterntained tuache double standard.

Go go Kenya, build a mondern airport in TAVETA to seize the opportunity while Tanzanians are still in deep sleep.

Mkimaliza TAVETA jengeni tena international airport Kisumu to seize opportunity of tourism for north-western corridor. After that you'll be ruling east africa, wajinga ndiyo tuliwao kwasababu hao watawala ni sisi ndio tunaowake madarakani.
 
Back
Top Bottom