RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Aliyekuwa mgombea wa kiti cha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, leo Machi 11, 2016 amemtembelea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, MMaalim Seif Sharif Hamad kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Maalim Seif kwa sasa anajipumzisha kwenye Hoteli hiyo baada ya kupata nafuu kufuatia kulzazwa kwenye Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam siku tatu zilizopita baada ya kuugua wakati anasafiri kutoka Zanzibar kuja Dar.