Emma.
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 19,932
- 5,560
Viongozi wakuu wa UKAWA wakiongozwa na aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA aliyekuwa anaungwa mkono na muungano wa vyama CHADEMA, CUF, NLD na NCCR (UKAWA ) Edward Lowasa leo amefanya mazungumzo na aliyekuwa mgombea uraisi kupitia CUF Maalim Seif kuhusu mgogoro unaendelea huko Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amekutana na viongozi Ukawa jijini Dar es Salaam kujadiliana nini cha kufanya baada ya mazungumzo yao na CCM Zanzibar kuonekana kukwama.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu ambaye alikuwa mmoja wa viongozi waliokutana na Maalim Seif, alisema mazungumzo hayo ni ya kupeana mawazo ya hatua gani wachukue kuhusiana na suala la Zanzibar.
“Mgogoro wa Zanzibar ni mkubwa, kwa hiyo tumejadiliana kujua tuendelee wapi katika kutatua mgogoro huo,” alisema Profesa Baregu.
Alisema katika kikao chao hakuna makubaliano rasmi ambayo wamefikia jana lakini taarifa nyingine zilizopatikana baadaye zimesema watakwenda Dodoma kuzungumza na wabunge.
Kikao hicho kilihudhuriwa na mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Twaha Taslima.