mshilakule
JF-Expert Member
- Jul 13, 2015
- 280
- 227
Source ya habari ni tanzania daima ambalo kila siku lnaelezea kukubarka kwa lowasa tangu alipo jiunga na cdm maana yake hamna jipya hapo just kumweka kwenye political sphere ili asisahaulike haraka
Hatimae wananchi wameanza kukiri heri wangemchagua Lowassa kuwa rais huenda angewahurumia katika bomoabomoa inayoendelea.
Wadau hii maana yake nini?
Chanzo: Tanzania Daima
Jamaa kaandika kama muandishi mwenye "elimu ya hapa na pale"yaan umeandika mengiii ila pumba tupu, hiv umesoma kwanza kabla ya kupost?? umekuwa kama una kimbizwa,,,
Source ya habari ni tanzania daima ambalo kila siku lnaelezea kukubarka kwa lowasa tangu alipo jiunga na cdm maana yake hamna jipya hapo just kumweka kwenye political sphere ili asisahaulike haraka
Jangwani ni eneo la njia/mkondo wa maji,wengine wanasema ni sehemu ya 'kupumulia' bahari....granted. Kile kituo cha magari hayo mapya ya nanihii pale kimejengwa mlimani siyo jangwani pale! Tena yale mafuriko yaliyopita yalikipiga chini chali kabisa ikabidi waanze kujenga upya. Watakibomoa lini? Na wale waliojaza udongo pale pembeni, na walionyanyua lile eneo la upande wa pili yalipo mabanda ya wamachinga hawajatatiza huo mkondo wa maji? Kwa harakati zile hakuna madhara kwa eneo lile na maeneo jirani? Walioruhusu/zembea hadi shughuli hizo zikafanyika lini watachukuliwa hatua?!
Jamaa kaandika kama muandishi mwenye "elimu ya hapa na pale"
1000digits kuna wimbo mmoja Bushoke Junior anasema wanayataka mapinduzi na mapinduzi hawayawezi....tafuta hiyo nyimbo, ujumbe wake ni mmoja tu, hakuna mabadiliko yasiyokuwa na gharama. Umeandika meeengi sana lakini tambua ukweli mmoja tu, haiwezekani watu waishi kwa kuzingatia taratibu za kizamani halafu wakapata maendeleo ya kisasa. Mtanzania hawezi kuishi kwa tamaduni zake, kwa hulka zake halafu akayafikia maendeleo waliyonayo wengine. Hakuna kitu kama hicho, machungu lazima yatukute ili tuweze kuvuka kipindi hiki. Inauma mtu anabomolewa nyumba aliyoijenga kwa jasho, lakini ni lazima tufike mahali kwa ujumla wetu tukubali kurudi katika njia iliyonyooka.
Hivi unahabari kuna watu walipewa viwanja mabwepande wakaviuza wakarejea tena jangwani.Leo hawana hata pakwenda. Watu kama hao wasaidiweje.Tatizo ni mahaba ya watu waliyo nayo kwa Magufuli.
Kuna majipu humu ndani ambayo yanataka kupoteza malengo kwa kusifia kila kitu.
Wanataka kuaminisha watu kuwa umaskini wa watanzania umesababishwa na ujenzi wa mabondeni bila kujua kwamba kujenga mabondeni kumesababishwa na umaskini wa watu.
Hawa magamba kazi yao ni kusifia kila kitu kama magaidi yanayoamini kila wanachosoma kwenye vitabu vya dini na kuua kila mwenye imani tofauti na wao.
Mtu anayependa sana na kuamini kila kitu ni hatari sana na anaweza kuwa gaidi muda wowote.
Magufuli sio Mungu hata asikosolewe kwa kukiuka utu na heshma ya wazee ,wakina mama na watoto maskini kwa makosa yaliyofanywa na serikali yake iliyokua dhaifu kwa miaka 50 tangu uhuru.
Hata Mwenyezi Mungu kwa Mujibu wa biblia alijikosoa mwenyewe japo mwanzoni aliona kila kitu alikifanya sawa.
Ifahamike tu kuwa mimi sipingi watu kuhamishwa toka mabondeni.
Ninachokataa ni kuwaacha wale wazee waliobomolewa bila kupewa makazi.
Magufuli huyu huyu ndiye aliyekuwa amewapa Makada na viongozi wenzake nyumba bora zilizokua zinamilikiwa na serikali tena kwa bei sawa na bure japokuwa walikua na majumba na mapesa mengi ya kujenga nyumba popote. Tuliaminishwa kuwa viongozi wa serikali hawakuwa na uwezo wa kujenga nyumba na wengi wanakaribia kustaafu hivyo wananchi tusilalamike na kukosoa uamuzi wa serikali kuwauzia nyumba kwa bei ya choo cha shimo.
Leo hii serikali hiyo hiyo chini ya mtu yule yule aliyesema mawaziri na viongozi wakuu wa serikali hawakua na uwezo wa kujenga nyumba anawaacha wazee bila makazi baada ya kuvunja nyumba zao.
Kwa nini huruma iliyokuwa imeonyeshwa kwa viongozi wa serikali wakati wa kuuza nyumba za umma kwa kusema kuwa wapewe tu kwa kuwa hawana uwezo isitunike kwa wazee maskini wa mabondeni kujengewa nyumba za kawaida wakapewa kwa kukatwa kodi kwa miaka hata 20 theni wamilkishwe ?
Nimetoa wazo la kutumia majeshi yetu kuwajengea nyumba kwa gharama nafuu?
Msimamo wangu miaka yote ni wizara ya ardhi kupima viwanja na kutenga maeneo ya makazi salama kwa wananchi wote. Hiyo ndiyo kazi ya serikali. Ndio maana watu wanalipwa kwa kazi hiyo.
Sasa linapokuja suala la uzembe wa muda mrefu wa serikali halafu ikabidi hatua kubwa na ya lazima ifanyike kwa kuhamisha watu toka makazi yao basi kwa taifa lolote lenye kujali watu wake ni lazima libebe mzigo ili kupunguza machungu ya wananchi wake wasio na hatia.
Haifai na haikubaliki kwa serikali kuwabomolea watu makazi yao halafu ikawaacha kila mmoja aende kujenga nyumba holela tena huko pembezoni mwa mji. Baada ya muda hawa waliobomolewa na wengi wao kukosa viwanja na nyumba watafuatwa tena na serikali hii hii ya CCM na kuambiwa kuwa wamejenga bila ramani.
Unafiki utaacha lini, kwanini usianze Na JkJamani mwacheni Lowassa aende kuchunga ng'ombe wake huko Monduli.
Hii dhana ya kumjaza ujinga eti bado anapendwa na wananchi wanamkumbuka ili mzidi kumkamua pesa zake za kifisadi mtakuja kupambana na karma law mbele ya safari ya kisiasa.
Mbowe naomba umuonee Lowassa huruma! Let him go, please!
Lowassa is finished! There is no way back for him!
malalamiko hayasaidii, miaka ya 80 na 90 katika maeneo yote ya mabondeni hakukuwa na watu, tatizo la serikali ni kuwa iliiacha rushwa ikaota mizizi, mwananchi wa hali ya chini akakosa mtetezi. maafisa ardhi wakaota mapembe, wakaanza kuwadharau vijana mpaka wazee, lakini sheria na ramani za miji zilikuwepo, kutokutumika kwa sheria hakumaanishi kuwa sheria hazipo, kutokuzijua sheria pia hakumaanishi kuwa sheria hazipo, inasikitisha kuona watu wakikosa makazi baada ya nyumba kubomolewa lakini haya maumivu na mateso ni mambo ya kupita, huwezi kujenga Tanzania mpya kwa kutegemea tamaduni zile zile za zamani.Tatizo ni mahaba ya watu waliyo nayo kwa Magufuli.
Kuna majipu humu ndani ambayo yanataka kupoteza malengo kwa kusifia kila kitu.
Wanataka kuaminisha watu kuwa umaskini wa watanzania umesababishwa na ujenzi wa mabondeni bila kujua kwamba kujenga mabondeni kumesababishwa na umaskini wa watu.
Hawa magamba kazi yao ni kusifia kila kitu kama magaidi yanayoamini kila wanachosoma kwenye vitabu vya dini na kuua kila mwenye imani tofauti na wao.
Mtu anayependa sana na kuamini kila kitu ni hatari sana na anaweza kuwa gaidi muda wowote.
Magufuli sio Mungu hata asikosolewe kwa kukiuka utu na heshma ya wazee ,wakina mama na watoto maskini kwa makosa yaliyofanywa na serikali yake iliyokua dhaifu kwa miaka 50 tangu uhuru.
Hata Mwenyezi Mungu kwa Mujibu wa biblia alijikosoa mwenyewe japo mwanzoni aliona kila kitu alikifanya sawa.
Ifahamike tu kuwa mimi sipingi watu kuhamishwa toka mabondeni.
Ninachokataa ni kuwaacha wale wazee waliobomolewa bila kupewa makazi.
Magufuli huyu huyu ndiye aliyekuwa amewapa Makada na viongozi wenzake nyumba bora zilizokua zinamilikiwa na serikali tena kwa bei sawa na bure japokuwa walikua na majumba na mapesa mengi ya kujenga nyumba popote. Tuliaminishwa kuwa viongozi wa serikali hawakuwa na uwezo wa kujenga nyumba na wengi wanakaribia kustaafu hivyo wananchi tusilalamike na kukosoa uamuzi wa serikali kuwauzia nyumba kwa bei ya choo cha shimo.
Leo hii serikali hiyo hiyo chini ya mtu yule yule aliyesema mawaziri na viongozi wakuu wa serikali hawakua na uwezo wa kujenga nyumba anawaacha wazee bila makazi baada ya kuvunja nyumba zao.
Kwa nini huruma iliyokuwa imeonyeshwa kwa viongozi wa serikali wakati wa kuuza nyumba za umma kwa kusema kuwa wapewe tu kwa kuwa hawana uwezo isitunike kwa wazee maskini wa mabondeni kujengewa nyumba za kawaida wakapewa kwa kukatwa kodi kwa miaka hata 20 theni wamilkishwe ?
Nimetoa wazo la kutumia majeshi yetu kuwajengea nyumba kwa gharama nafuu?
Msimamo wangu miaka yote ni wizara ya ardhi kupima viwanja na kutenga maeneo ya makazi salama kwa wananchi wote. Hiyo ndiyo kazi ya serikali. Ndio maana watu wanalipwa kwa kazi hiyo.
Sasa linapokuja suala la uzembe wa muda mrefu wa serikali halafu ikabidi hatua kubwa na ya lazima ifanyike kwa kuhamisha watu toka makazi yao basi kwa taifa lolote lenye kujali watu wake ni lazima libebe mzigo ili kupunguza machungu ya wananchi wake wasio na hatia.
Haifai na haikubaliki kwa serikali kuwabomolea watu makazi yao halafu ikawaacha kila mmoja aende kujenga nyumba holela tena huko pembezoni mwa mji. Baada ya muda hawa waliobomolewa na wengi wao kukosa viwanja na nyumba watafuatwa tena na serikali hii hii ya CCM na kuambiwa kuwa wamejenga bila ramani.
Wanaomkumbuka Lowasa ni waovu na mafisadi
Hakuna atakayemkumbuka mwizi Lowasa baada ya mda mchache mtamjua magufuli anacholenga watu wote watamwelewa tu.
umesahau usafiri wa umma. mojawapo ya sababu za kuanza kuzorota huduma ya UDA miaka ile ya 80 ni kuendelea kwa kasi ya ujenzi ovyo wa makazi hivyo huduma ya usafiri wa uda kushindwa kuwafikia wakazi. laki kadha hadi wengi wa watu wa dsm wakawa wanaishi kwenye skwata. mabasi makubwa yanayofaa mijini yakawa hayawezi kupita kwenye vichochoro kuwafuata watu.
Wewe ni ndezi kabisaManaake wanajua Lowassa ni kama JK tu kuchekea ujinga ndio kazi yake