John Magufuli anaangalia mbali sana, nadhani hakukosea kutojenga urafiki wa wafanyabiashara kipindi kile CCM inafanya kampeni. Hakutaka kuiangalia Tanzania yenye kuwafaidisha wachache na kuwasahau walio wengi. Hata ile jeuri ya kuwaambia watu hakuna kwenda nje ya nchi, imetokana na yeye mwenyewe kujiamini katika uadilifu alionao. Rais tajiri mwenye hisa nyingi kwenye mabenki na makampuni makubwa ya kimataifa atapata wapi jeuri ya kuwaambia watu wasiende nje ya nchi?. JPM mpaka sasa keshaweza kuzidhibiti tamaa binafsi za utajiri, kwake walio wengi wanaporidhika basi wale wachache hawawezi kumnyima usingizi.
Hivi Magufuli ametaja mali zake?
Mana hatutaki unafiki na visasi tunataka dhamira ya kweli.
Ni jambo baya sana kushangilia udhalimu wanaofanyiwa wazee na watoto wa watanzania wenzetu ambao wengi wao ni maskini wakutupwa wanaobomolewa nyumba zao na kuachwa wakilala nje.
Ni laana kubwa kuwafanyia unyama wazee na akinamama na watoto eti wamejenga mabondeni.
Je ni kwa nini mji mzima wa Dsm usibomolewe kwa kuwa ni maeneo karibu yote yamejengwa bila kupimwa.
Serikali ya CCM ilikua wapi?
Na je CCM wote walikua ni mataaira isipokua Magufuli peke yake ndio amekuja kuwazindua?
Au kwa sababu maeneo mengi ya jiji ccm ilikosa kura mwaka jana?
Ni kwa nini wazee wanaotaabika kwa kuvunjiwa nyumba wasingeheshimiwa kama watu dhaifu?
Ndio maana CCM na serikali yake ilishindwa kudhibiti mauaji ya albino kwa sababu ya kukosa huruma!
Kuna ugumu gani kwa serikali ya CCM kutumia pesa inazokusudia kuinyang'anya CUF ushindi wake kwa kurudia uchaguzi uliofanyika na kumalizika kwa amani kwa kuzitumia kwenye kuwasaidia wazee wetu kwa kuwajengea nyumba hata vyumba viwili kwenye eneo lililopimwa na kisha kuwatoza kodi ndogo ya nyumba,hata sh. 5000 tu kwa mwezi ili waweze kuishi kama hao maprofesa wanaoonekana kuwa ndio binadamu ilihali ndio walitumika miaka nenda rudi kuihujumu nchi?
Je, hao waliojenga mabondeni wangejenga wapo wakati watu wachache waliowahi kushika madaraka kwenye serikali za CCM wamejimilikisha kila eneo zuri na nyumba za umma?
Je,ni kwa nini wasianze na ofisi za CCM ambazo zimejengwa bila kufuata ramani?
Hivi Serikali imeshindwa nini kutumia majeshi yetu, makuruta wa JKT na wafungwa kujenga nyumba hata laki moja kwa gharama ndogo sana kwa ajili ya wazee na wakina mama na watoto walioko mabondeni? Kisha wakalipa kodi ya sh. 5000 - 10,000/-?
Je, pangekua na vita ni sh.ngapi zingetumika?
Iweje tushindwe kutumia majeshi yetu kuhudumia jamii kwenye nchi ya amani kama TZ?
Au CCM inataka kinuke kule Zanzibar itumie mamilioni ya pesa kupeleka majeshi kule kuweka serikali kwa udhalimu wa kuua demokrisia. Je,itasaidia nini kumwona Shein yuko Madarakani kwa gharama za watanganyika wakati baba zetu na mama zetu na watoto wetu wanalala nje kwa ku unjiwa vijumba vyao tena kwa uzembe wa serikali wa kushindwa kutimiza wajibu wake wa kupima viwanja na kuweka wazi matumizi ya ardhi?
Kila sheria inayotungwa inapaswa kutekelezwa kwa kujali kwanza ustawi wa watu wake sio kuufanya wengine wafe kwa makosa na uzembe wa watawala na chama kile kile kilichosababisha uzembe huo.
CCM na Serikali yake walipaswa kwanza kuwaomba watanzania msamaha kwanza ndipo waanze kuwabomolea nyumba zao?
Kama Serikali ya Magufuli na CCM yake wameamua kuwaadhibu wote waliovunja sheria basi isiishie kwa wazee na akina mama na watoto waliojenga mabondeni kwa umaskini wao bali wawaadhibu wote mpaka wale waliofoji vyeti ambao wako kwenye ajira na wanaendelea kuhurumiwa na kutumbua mishahara ilihali masikini hawahurumiwi. Hatusikii mtu ndani ya CCM akiseme au kushauri kwamba wote waliodanganya kwenye ajira wavunjiwe ajira zao kama wazee wetu wa mabondeni!!
Hii inakuaje kujipatia umaarufu kwa kuwaadhibu na kutesa walalahoi na kuwaacha watu wanaokaa kwenye maofisi yenye viyoyozi kwa vyeti batili wakiendelea kutanua?
Kama busara inatumika basi itumike kwa wote.