Lowassa akitaka kuukata mzizi wa fitina achukue hatua hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa akitaka kuukata mzizi wa fitina achukue hatua hii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Dec 7, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  WanaJF

  Mie nadhani E. Lowassa angechukua hatua ya haraka ya kukata mzizi wa fitina unaomuandama kwa kufanya yafuatayo:

  Kwa kuwa tuhuma kubwa dhidi yake ni ufisadi wa Richmond/Dowans (nyingine hazijatajwa/hakuna) basi aombe kwa mama Rosemary Mwakitwange amwandalie mdahalo wa yeye kujieleza tuhuma zake kwa namna ya kujisafisha.

  Watafutwe watu wenye kulielewa vema sakata zima la Richmond/Dowans kama vile waandishi wa habari, na watu wengine kwa ujumla wa kumuuliza maswali na kuomba ufafanuzi kuhusu role yake katika kashfa hiyo.

  Najua mdajalo huo anaweza kuugharamia yeye mwenyewe kwani ni kwa faida yake kama kweli anataka kujisafisha.

  Vinginevyo mtu huyu anatuvuruga tu kwa kuleta utetezi wa kijuu juu. Mwezi uliopita aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na wengi walifikiri alikuwa anataka kujieleza kwa ufasaha kuhusu tuhuma dhidi yake, kumbe alitaka kuwatisha tu... kwamba wakimwandika mambo ya uongo atawashitaki.

  Sasa waandishi hawajui ukweli ni upi hasa – kwa hivyo ni bora akajitokeza na kusema yote anayoyaona ya kweli na akubali kuhojiwa katika kupata ufafanuzi. Kuanzia hapo wakimuandika uongo atakuwa na haki ya kuwashitaki.

  Over to you Mr EL …. KAZI NI KWAKO!!!

  Nawasilisha.


   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,386
  Likes Received: 22,266
  Trophy Points: 280
  pumbavu yule, hatakiwi kufundishwa namna ya kuoga, acha madhambi yake yamle hadi aoeze
   
 3. M

  Middle JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kweli bosi wangu
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Duh Mkuu Zak -- kweli naamini humpendi. Akifanya hivyo atakuwa ame-commit political suicide. Salama yake ni kutuchezea hivi hivi tu, kugusua gusia bila ya kwenda kwa undani katika tuhuma zinzomuelemea.
   
 5. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza aje mtu na tuhuma za moja kwa moja na zenye ushahidi juu ya Mh, Lowassa ndio nae atajieleza ni vipi hausiki na dowans na richmond.
  Sio hizi rumors tu akiwapa kisogo wananyoosha kidole kwa Lowassa akigeuka wanakipindisha, tena kwa kumchekea.
   
 6. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Na hao waulizaji maswali watapatikanaje?... Isije ikawa ni fursa ya sanaa nyingine kuwahadaa watanzania.

  Au umesahau watu walikua na mabango ya "kupinga" Rostam kujiuzulu, hata kabla hajatangaza kujiuzulu kule Igunga?
  Au umesahau watu waliolia na kusaga meno siku ile baadaye wakaonekana na vicheko kama si wao?
  Au umesahau watu walio"zimia" kwa mheshmiwa mbunge kujiuzulu? Na baadae wakaonekana Nzega wakiji"pongeza".
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwenye mdahalo watapatikana tu na sio lazima wawe wale adversaries wake kisiasa. Unataka kusema alijiuzulu kwa rumours tu?
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nakuhakikishia watakuwepo watu wenye ushahidi wa kimaandishi watakaokuja na makabrasha. Usianze kuweka obstacles za kumpa sababu akwepe mdahalo. Nakubali mdahalo utakata mizizi ya fitina, asiogope kuchukua hatua hii nzito ili irudi heshima yake mbele ya jamii.
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2011
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Zak Malang,

  Sikubaliani na pendekezo lako, hakuna ambaye anajua ukweli wa sakata zima la Richmond/Dowans zaidi ya Lowassa, JK, Karamagi, Dr. Msabaha na Dr. Mwakapugi. Wengine waliobakia wanajua nusu nusu tu.

  Waandishi wa habari nao wako gizani kama sisi, kwa hiyo hakuna mtu ambaye anaweza kumhoji Lowassa kwa undani kwa kuwa info nyingi za dubwasha hilo ilikuwa ni siri yao wao wenyewe.

  Kama unakumbuka Kamati Teule ya Dr. Mwakyembe iliomba file fulani kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Dr. Mwakapugi alimtuma mfanyakazi wa wizarani aende nalo na arudi nalo bila kuiachia Kamati Teule ipitie nyaraka zote zilizokuwa kwenye hilo file. Huyo aliyetumwa kazi yake ilikuwa ni kuwasomea tu kile ambacho wanauliza, ndipo alipoambiwa arudi na akamwambia Dr. Mwakapugi mwenyewe aende kuonana na Kamati Teule. Bado stori ilikuwa ni ile ile, Mwakapugi hakuwaachia file.

  Kwa hiyo kuna mengi sana ambayo hatuyajui na hata kama yapo ambayo wana habari wanayajua inawezekana wanaweza kuwa wanayajua nusu nusu, so, ili aweze kujitetea vizuri ahakikishe kwamba wanaomhoji wana-details zote na inaweza kuwa rahisi kumbana na maswali.

  Hitimisho ni kwamba Richmond/Dowans inagusa Ikulu na ndio maana imekuwa ikimpa jeuri EL. JK hayuko tayari hilo dubwana lieleweke kwa wananchi maana na yeye mwenyewe atajiweka kwenye kundi moja na EL na ilihali baadhi ya wananchi wanaamini kwamba JK ni msafi. Subiri JK atoke madarakani ndipo utapata nondo zote za Richmond/Dowans. Kwa sasa tubaki na sintofahamu kwa kuwa Ikulu haitaki tujue dili nzima! Mwakyembe alishasema kwamba Kamati Teule kuna mengine iliyaacha ili "kulinda heshima ya serikali". Je, ni serikali gani iliyokuwa inalindwa? Nani kiongozi wa hiyo serikali?
   
 10. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Akieleza juu ya mmliki halali wa kitu hiki "Rich Of Monduli" ndo nitamwamini.
   
 11. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Atakuwa anakata tawi alilokalia...hana ubavu!
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Umechambua kwa UMAKINI
  thanx
   
 13. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa kamati ya Mwakyembe haikumtendea haki.
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,607
  Likes Received: 3,900
  Trophy Points: 280
  asante sana , naona zak bado yuko ile dunia ya wanaishi kwa kuamini kila wanachoelezwa!

  ngau angesema mdahalo wa wahusika wote wa richmond...akiwemo wahusika wa ile kamatai ya bunge

  Mwisho kitu ambacho mtoa hoja amekiri ni kuwa...LEO HII WATANZANIA WENYE TUHUMA YA UFISADI WANATAKIWA KUANDAA MIDAHALO YA KUJISAFISHA....shame!

  yaani umeshindwa kusema kwa nini DPP, TAKUKURU , POLISI NA MAHAKAMA haijaweza kumshtaki Lowasa unasema kinyume chake...then tatizo si EL ni system!

  system ndio inamfanya EL awe jinsi alivyo!!

  soma signature
   
 15. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,812
  Likes Received: 36,903
  Trophy Points: 280
  Basi amalizie yale maelezo aliyoanza kuyatoa TVT kabla mitambo haijakatwa gafla kipindi kile baada ya kuachia ngazi.
   
 16. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Tanzania hamna viongozi wazuri period mmejaza walarushwa tu. Magufuli pekee ndiyo kiongozi atakaye safisha Tanzania wengine wa CCM ni vichekesho tu! vilevile upinzani watasafisha nchi!
   
 17. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #17
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Ukisoma makala baada ya makala hapa JF,utafikia uamuzi kwamba Lowassa ni fisadi sugu. Kama atakuwa Rais kwa hela zake,hilo ni jambo la Watanzania kuamua. Kwa sababu ukitazama biography za rais wa marekani utaona wengi wameingia kwa ufisadi. Bill Clinton,ufisadi wa gun-running,. Lyndon. Johnson,ukisoma biography sijui kama utaendelea kuuliza nani kamuua Kennedy. Kennedy pia nae kaingia madarakani kwa ufisadi na victory margin ya 120,000 votes. Hata. Barak. Obama akishang'atuka labda tutaambiwa aliingia madarakani kwa ufisadi. Kuhusu alivyosema Lowassa jana kwamba "kama amefanya makosa,kwa nini hawajampeleka mahakamani. Watu wanatoa maoni yao. Wengine wanasema . Lowassa ni fisadi,wengine wanasema sio fisadi. Hii ni kama wakati wa. Lucifer. Lucifer alikuwa anawaasa watu wagome. Kila mmoja wao alikuwa anaombwa kujihusisha na huo. Kwa hiyo uamuzi haukutolewa juu ya Lucifer mpaka mtu wa mwisho anayeathirika na huo mgomo kwa njia moja au nyingine, kutoa uamuzi wake,for or against the rebellion. Meanwhile uamuzi ulipokuwa unachelewa Lucifer alikuwa anasema:". Tumegoma siku hizi zote,lakini hatukuchuliwa hatua yoyote. Inaonyesha kwamba hawana ubavu wa kutugusa kama tuklungana" . Lakini baada ya mtu wa mwisho kutoa uamuzi,uamuzi ulitolewa na. Lucifer alikamatwa na kuwekwa detention. Sasa nitaulizwa hizi habari nimezipata wapi. Nimesoma katika. Urantia. Book,kitabu ambacho lazima kisomwe kwa uangalifu, kwa sababu sijui watu waliokiandika walitumia meth amphetamine kiasi gani. Kile kitabu ni pure meth. Lakini utaona ukisoma katika Biblia au katika .Quraan,kwamba mgomo ulitokea duniani,wakati wa Adam na Hawa,wakati wa .Sodoma na Gomora,haya ndiyo mambo yanayosimuliwa.
   
 18. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  .........wanaotakiwa kufanya hivi ni wale wanaotishika na ama Lowassa mwenyewe au kivuli chake, hawalali, ili mradi tu wajue leo EL kafanya nini, namshauri awapuuze kwa sababu wao wameshindwa kumpuuza;
   
 19. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Pamoja na kashfa za miaka ya nyuma na Nyerere kumkataa,lakini EL kama akiweza kututhibitishia wabongo pasi shaka yoyote kuwa hakuhusika hata kidogo katika sakata zima la Richmond na akatutajia wahusika wote wa Richmond na kwamba yeye alijiuzuru ili tu kulinda heshima ya serikali yake,akigombea Urais 2015 kupitia chama chochote/independent,ana kura yangu tayari.
   
 20. L

  LowasaSupporter Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani watu tunajua ya kuwa ni ushabiki na chuki binafsi za akina Sita, Ninauye, Membe, Kikwete, Nyalandu na wengine wengi ambao wamezijenga kwa Lowassa. Na pia tukubali ya kuwa uwezo wa Lowassa kikazi unawapa taabu hawa jamaa. Yupi kati ya hawa ni msafi? Membe ambaye amechukua pesa kutoka kwa Quaddafi ili kujikuza kisiasa hapa Tanzania, Sitta ambaye anasafarisha magogo nje ya Tanzania, Kikwete ambaye anachakachua nchi kupitia kijana wake Ridhwani? Nyalandu ambaye amejenga jumba kwenye kiwanja kichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa dispensari? Yupi anaweza kumtupia mawe akisema mikono yake ni ya haki? Nadhani baadhi ya watanzania tumekuwa wanafiki sana, chuki hii kwa Lowassa imeanza kufifia na hakuna mwaka mmoja zaidi wimbo huu wa kumchafua Lowassa utakuwa unakubalika tena na watanzania. Yaliyopagwa na mungu binadamu hawezi kutegua, kama Mungu anataka Lowasa kuwa rais wa nchi hii atakuwa, wala siyo hao wenye kuvaa ngozi ya kondoo wakipita wakisema huyu hafai, huyu hivi, yule vile, kama ni fisadi toeni ushahidi. Msije mkakuta mnatoa hukumu pasipo haki....Msihukumu msije mkahukumiwa kwa kukosa kiongozi thabiti...Msidanganyike na hawa wenye hila binafsi akina Sitta, Membe na kundi lake?
   
Loading...