iArmaniAdamson
JF-Expert Member
- Jun 15, 2015
- 944
- 289
UTANGULIZI:
Kama inavyoeleweka vizuri kwa sasa, athari za maamuzi ya muda wa mwisho ya UKAWA kumteua mtu ambaye hawamfahamu vizuri, ni kwamba Lowassa ndani ya CCM alivunja kanuni akitaka achonganishe Mwenyekiti wa chama na wanachama wake kwa kutofuata itifaki za "kutangaza nia" huko CCM;
HISTORIA FUPI:
Athari za kumchagua mtu wa dharura ni kama ilivyo kwenye historia hii fupi.
Huko Malawi, Hayati Raisi Mutharika dakika za mwisho kabisa alichaguliwa kwa kipingamizi kikubwa kuwania uraisi (pamoja na kwamba alikuwa hata ajulikani na wanachama halisia) kwa tiketi ya chama cha zamani (UDF).
Baada ya uchaguzi, alipochaguliwa ilitokea akapishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama (aliyemuomba kuwania Uraisi). Mutharika akajivua uanachama wa chama cha UDF (kilichomchagua) na kuunda chama chake kipya cha DPP akiwa ndani ya uRaisi.
UTAFITI:-
Kuna mambo makuu matatu yanachangia hili:-
1. Lowassa amechaguliwa kwa dharura sana, baada ya machungu ya kukatwa (na ni kama amenunua chama, maana mipango yote ya kujitambulisha, kutangza mali na kujisafisha yaliwekwa pembeni alipotua CHADEMA);
2. Lowassa sio mtu wa kufuata kanuni au sheria za chama, kama ilivyoonekana ndani ya CCM (kufanya kampeni kabla ya muda uliopangwa na kuendelea kufanya hivyo hata baada ya kuonywa na uongozi wa chama chake kwamba asifanye hivyo);
3. Lowassa HAJAWAHI KUVAA GWANDA na SIJAMWONA NA GWANDA hii inasema vizuri moyo wake uko wapi au hauko wapi kisiasa na sidhani atakaa chadema milele, (mkumbuke CHADEMA sio baba yake na wala sio mama yake);
SWALI:-
Lowassa akiingia Ikulu na wakapishana mawazo na Mbowe kuhusiana na uendeshaji wa chama, ukizingatia hawafahamiani vizuri kama ilivyo kwa Mbowe na Slaa etc.
JE, Lowassa (akiwa Raisi na Amri Jeshi Mkuu) na Mbowe (akiwa Kiongozi na Mkuu wake kwenye chama alichochaguliwa) wakipishana, NINI KITAMZUIA LOWASSA ) KUTOKA UKAWA/CHADEMA, ii) kujiunga na ACT, iii) kuanzisha cham chake, au iv) hata KURUDI CCM chama anachojua vizuri na kwenye club ya marafiki zake wa zaidi ya miaka 38 / chama cha mapinzudi / CCM !