Mazingira
JF-Expert Member
- May 31, 2009
- 1,833
- 306
Kuna wakati najaribu kuwaza mwenyewe, hivi hawa akina Mbowe, Lema, Tundu Lissu, Mnyika, Msigwa etc wanajua anachowawazia Lowasa moyoni mwake? Maana walizunguka karibu nchi nzima wakimwita fisadi na leo hii ameingia kwao kawapa na pesa zake na wamempa nafasi ya kugombea cheo cha urais. Nahisi akipata anaweza kugeuka ghafala na kuwashughulikia hawa watu. Ukiangalia hata sasa hivi kwenye kampeni namuona angalau Mbowe lakini ameshasuka team yake ya wana CCM B (Sumaye, Mgeja na Masha) wenzake ndo anazunguka nao. Ngoja tusubiri tuone mwisho wake, lakini nahisi jamaa ana uchungu na fundo la sumu ambalo atawatemea mara baada ya uchaguzi. Na akishindwa kamwe si mtu wa kukijega chama kama alivyofanya Slaa na kitapoteza imani kwa wananchi kabisa.