Elections 2015 Lowassa akanusha tetesi za kuhamia CHADEMA

Nani sasa mchafuzi wa LOWASSA, CCM au CHADEMA waliomuita FISADI mwembeyanga? hebu nyoosha udaku wako basi angalau uonekane kuna kitu unataka kusema then tutaona kama pumba au la.

Tatizo lako unataka kujibu kila posting ndiyo maana huna muda wa kuzisoma ..................... rudia kusoma tena utaelewa!!
 
TAARIFA YA KUKANUSHA KUHAMIA CHADEMA SOURCE: Ofisi ya Mh.Lowassa (Mbunge

Kumeendelea kujitokeza taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii kuhusu Mh. Lowassa kuhamia chama cha Chadema.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mh. Lowassa amekabidhiwa kadi ya Chadema, ameshiriki uzinduzi wa tawi la Chadema na kwamba kutaandaliwa mkutano wa kumkaribisha katika viwanja vya jangwani.

Kwa mara nyingine tena, ofisi ya Mh. Lowassa inakanusha taarifa hizo kuwa sio za kweli na zenye kutaka kupotosha umma wa watanzania.

Imetolewa na ofisi ya Mh.Lowassa (Mbunge)

attachment.php
mimi kama gogo la shamba,tena ninaimani hata watu makini kama mimi.Luwasa atakuwa amefanya uamuzi wa busara sana kama atajitoa ccm na kujiunga na chama cha upinzani hasa chadema,tena wakati wa kujitoa ccm ni huu,
 
Hizo ni mbinu za washindani wenzake ndani ya ccm kutaka kuwaaminisha wananchi kwamba Lowasa siyo mtu mwenye msimamo.
 
Nini Lowassa ..hata Kikwete anayo Kadi ya Chadema ..amebaki nayo Kama kumbu kumbu ya kitendo chake cha kutaka kugombea Urais kwa Tiketi ya Chadema ..mwaka 1995... Wazee ..wakamsihii akubali Matokeo ( kukubali kwake Matokeo Ndio Kulimpa urais 2005 )

Sio AJABU kabisa mwaka 2015 mwanzoni au mwaka huu mwishoni tukaona mengi Kama Ataona chama chake hakimtendei haki.......mnaona Sasa kuna watu wanafanya kampeni kima mahala makanisani ....vyuoni..kila mahala lakini hawakemewi ...Kiasi inazusha maswali ....Kama Kweli karipio la chama lilikuwa genuine...wapo wanaenda kuzundua album hadi wanasema wametumwa na Rais na kampeni Za wazi ...yote hayaonekani
 
chadema wanaujua ukweli wa lowasa kutohusika na makashfa ,lowasa atakapofunguka na kusema ukweli uliopo watanzania wote watampenda kwa 80%.Kama huamini ngoja aje.You can not appreciate the importance of something until you loose it.
 
Miezi miwili na ushee iliyopita mgombea huyu aliulizwa na wahariri wa magazeti iwapo atahama CCM kama haitamchagua kugombea urais mwaka huu. Jibu lake lilikuwa kwamba hatahama CCM kamwe kwa sababu ilimlea, na kwamba huyo ambaye hamtaki ndani ya CCM ndiye ahame chama hicho!

Hata hivyo, kabla mwezi haujakatika mgombea huyu akakihama chama hicho na kujiunga na chama cha Upinzani, na chama hicho kikamteua kugombea urais, na sasa kuna -vijana wanamshabikia! Kimsingi aliongopa katika jibu lake lile na taswira aliyojijengea ni ya mtu asiyeaminika katika kile anachosema.

Ingekuwa ni Wazungu au sisi watu wenye kufikiri sawasawa, tusingemshabikia -katika mbio zake za urais kwa sababu ni mtu mwongo, kigeugeu na asiyeaminika, mtu asiyeweza kusimamia maneno yake mwenyewe.

Lakini kwa uwezo wetu mdogo wa kufikiri, baadhi yetu- tunamzawadia mgombea huyo kwa kumuunga mkono kwenye kampeni yake ya kuusaka urais kwa udi na uvumba!

Uongo na ukigeugeu kama huo pengine ungevumilika kama nafasi yenyewe anayowania si urais. Lakini urais ni kazi yenye heshima, utukufu, uadilifu nk. Ni kazi ambayo haimfai mtu mwongo na asiyesimamia maneno yake mwenyewe.

Vijana wetu hawajiulizi, kama huyu alidiriki kutudanganya jana, kwa nini asiendelee kutudanganya hata leo au hata baada ya kuingia Ikulu.

Tutamwamini vipi katika hayo anayodai kuwa atatutendea akiingia Ikulu kama huko nyuma aliwahi kutudanganya kwa kushindwa kusimamia maneno yake mwenyewe? TAFAKARI:
 
Hivi rais alisemaje kuhusu kura ya katiba mpya?
 
maisha ni tathmini... alijitathmini akaona amefungwa fikira yko. so alitumia uhuru na haki yke ya kisiasa.
 
Wapi kavunja katiba ?
Yeyote yule anahaki ya kubadisha uelekeo hata kama kauli alitolea juu ya paa !
Ni kabila tu ndiyo haibadilishiki .
 
Back
Top Bottom