Lowassa aiteka CC na NEC...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mambo hadharani, Edward Ngoyai Lowassa hatimaye amefanikiwa kupenyeza hoja yake ya CCJ ili kukwamisha hoja ya Kujivua Gamba. Habari za uhakika kutoka ndani ya vikao vya CC vinavyofanyika hapa Dodoma zinaeleza kuwa Lowassa, akipewa nguvu na Chiligati, Kinana na Mukama, amefanikiwa kumpa kigugumizi Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete kwa kuweka mezani hoja ya CCJ ambayo wachambuzi wanadai kuwa itawatia tunduni akina Samwel Sitta na Nape Nnauye.

Kutokana na hilo, hoja/mada juu ya kujivua gamba huenda isijadiliwe. Hadi nakwenda laptopuni jana, ajenda moja tu juu ya uchumi wa CCM ndiyo iliyojadiliwa hapa Dodoma. CC kikiwa ni kikao cha juu kabisa cha maamuzi kimeshindwa kumgusa kabisa Lowassa, Chenge na wafuasi wao. Wafuasi wa Lowassa wameapa kumpigania Mkuu wao hadi mwisho na kuhakikisha kuwa hagusiki.

Nimemnukuu mtu wa karibu wa Lowassa akitamba kuwa Lowassa hataguswa kamwe. Si mwingine ila ni Ole Millya, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha. Maji yanazidi unga....Mimi ni Vuta-Nkuvute kutoka Dodoma nikiripotia JamiiForums.
 
Watu walitaka anzisha ccj ili kuondokana na uchafu wa magamba, so it is not a big deal kwa watanzania.
Deal ni ufisadi na kujilimbikizia mali, huku ukiacha watanzania wakiteseka kwa magonjwa , umasikini ulikithiri na elimu duni.
CCJ si ishu inayo wasumbua wa TZ
 
Kila mbwa na siku yake ya kufa, hata siku ya Lowassa kufa kisiasa hakuna anayejua. Tatizo kubwa binadamu tuanishi kwa hisia
 
mo2.jpg


Sisasa ni mchezo mchafu, weledi wa kupanga hoja na kuzipangua ndio kufanikiwa.

Lowasa namwona ni mtu makini pekee katika serikali ya Kikwete ambaye pekee aliyethubutu kujivua gamba binafsi kwa kujiuzuru Uwaziri Mkuu baada ya kashfa ya Rishmond.

Wangapi wana kashfa nzito lakini Kikwete anakula nao sahani moja? Naweza sema Lowasa ni shujaa kwani viongozi wabovu wamejaa serikali ya Tanzania kuanzia na Mkulu mwenyewe lakini hakuna hata mmoja anayethubutu kujiuzuru au kuwajibishwa, badala yake wamejenga dhana ya kulindana.
 
CCM ingekuwa na UWEZO wa kumvua gamba EL ... wangekuwa tayari siku nyingi wameutumia UWEZO huo adimu ..kufanya mambo mengi ya Kijasiri na kimaendeleo kwa chama chao na jamii. Kwa kuwa hawana uwezo huo ..ni doto na ni upuuzi kusubiri CCM iliyo nyongonyea na kunyauka ..kufanya ..THE IMPOSSIBLE!! Na kumtikisa EL ... BAD FOR THIS COUNTRY!!
 

CCM ni chama makini kimepitia misukosuko mingi tu.. huu nao utapita tu... suluhu litapatikana watu wataekana sawa

 
WHAT DOES CCJ HAS TO DO WITH OUR BILLIONS OF MONEY GOT LOTS? COME ON JK DON'T FOOL YOUR SELF WITH CCJ ISSUE!

We would like to hear about those who misuse our resources and let CCM into bad shape!

Sorry I will be back soon!
 
Kila mbwa na siku yake ya kufa, hata siku ya Lowassa kufa kisiasa hakuna anayejua. Tatizo kubwa binadamu tuanishi kwa hisia

kuna watu wanajua fitina za siasa sio el aka mamvi, yeye najua kutumia pesa sio mdomo kama mnabisha tulia muone mambo yanavyokwenda!
 
Mbona hakukanusha tuhuma za Richmond, hana lolote ni papa tu !
 
Mbona hakukanusha tuhuma za Richmond, hana lolote ni papa tu !
Kujiuzuru kutokana na kashfa hizo ni jawabu la Lowaza kukubali kasoro katika uwajibikaji wake kama kiongozi, sasa jibu gani ulitegemea?
 
ni hivi ndugu zangu............EDWARD NGOYAI LOWASA haoindoki ccm.......
 
unajidanganya,rais kikwete anajua umuhimu wa el lwenye chama,nakuhakikishia chama kiatoka imara na el ataendelea kuwa mnec,na baadae mungu akimpa afya awaongoze watz

Nakubalina na wewe kuwa EL atabaki LAKINI sikubaliani na wewe kuwa kubaki kwake ni kwa sababu ulizotoa! JK hana uwezo hata akitaka kumvua gamba EL. Na Tatu Pamoja na Mungu kuwa na uwezakano mkubwa kusaidia afya ya EL ... but being honest .. The stress and all the frictions politically and socially ..am telling .... has all the ability to compromise the dudes health in a bad way!!
 
Chuki zenu na story za kumchafua lowassa zinawaponza lowassa ni miongoni washupavu walioko tanzania yeye alikubali kujiuzulu kwa dhana ya uwajibikaji ni viongozi wangapi wamekutwa na kashfa tena za moja kwa moja lakini bado wanang'ang'ania nyadhifa zao?

Ya Ngeleja, Jairo hamjayaona? why Lowassa? Chenge alikutwa na hela nyingi tu na akajiuzulu lakini haandamwi kama lowassa jiulizeni kwa nn?

Na siku zote mti wenye matunda ndo hupigwa mawe lakini endeleeni mwisho wa siku mtabaki na aibu ka nilivyosema awali tunarudi arusha na ushindi na mapokezi makubwa yanawangojea ndo hapo mtakapokufa na vijiba vya roho
 
Back
Top Bottom