ALWATAN KIZIGO
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 539
- 642
LOWASSA AISOMA NAMBA MARA TATU(3) CCM.
Vijana wengi wa miaka 80,90 na 2000 wanafikiri 2015 hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Lowasa kuisoma namba ndani ya CCM hadi kuamua kwenda kununua nafasi ya kugombea CHADEMA.
Mwaka1995-kwa mara ya kwanza Lowasa anaonja shubiri ya kuisoma namba ndani ya CCM.
Na aliyehakikisha Lowasa anaisoma namba vilivyo ni Baba wa Taifa Mwl.Nyerere na Kamati kuu na kwa sababu kuu mbili.
1.Kununua watu-wajumbe wa halmashauri kuu na mkutano mkuu(RUSHWA)
2.Uadilifu-Niwakumbushe Lowasa huyu mwaka 1995 wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM wakati Mwl.Nyerere na viongozi wengine wamekwenda dodoma kwa usafiri wa magari,Lowasa alikwenda na ndege ya kukodi Chadema watahoji na ukasema kuna shida gani mtu kwenda na ndege wakati pesa ni yake?-AMEKOSA UADILIFU.
Baba wa Taifa Mwl.Nyerere kwenye mkutano wa NEC alihoji huyu kijana pesa hizi za kununua wajumbe na kukodi ndege kazitoa wapi maana mm ninavyomfahamu hana biashara yeyote wala baba yake?
Kubwa zaidi kwenye mkutano huo wa halmashauri kuu(NEC) wakati mwenyekiti Alhaji Ally Hassan Mwinyi,Mwl.Nyerere na wajumbe wa kamati kuu na secretariat wanaingia wajumbe wote walionunuliwa na kupandikizwa na lowasa walisimama na kuimba nyimbo kama ile ya 2015 ya kuwa na imani na Lowasa kama ilivyofanyika 2015 ndio mpate kufahamu yale ni marudio.
Mwl.Nyerere alisimama na kuwauliza hiki ni kikao cha wahuni?.
Akatoa msimamo wake wote wenye imani na Lowasa na si CCM waondoke,hakuondoka mjumbe hata mmoja. Wajumbe wakafanya maamuzi.
HAPA lowasa ANASOMESHWA NAMBA KWA MARA YA KWANZA KWA MSIMAMO WA CCM NA MWL.NYERERE-kwa kukosa uadilifu na matumizi ya Rushwa kutafuta uongozi ndani ya chama.
Leo hii vyama vya upinzani vinasema CCM haishi kwa Matendo Maisha na misimamo ya Baba wa Taifa Mwl.Nyerere,Je huyu Baba wa taifa si yetu sote?Nyinyi wapinzani mnayaishi maisha ya Baba wa Taifa huyo?
Mwaka 2015 wajumbe wa halmashauri kuu(NEC)walichofanya yalikuwa ni marudio ya mkakati ule ule wa mwaka 1995.
Niwarudishe nyuma kidogo Lowasa tokea miaka ya 90 alifanya kazi kubwa ya kujijenga yeye binafsi na si CCM, kwake CCM ilikuwa daraja tu kuelekea Ikulu, na hili leo ndio nilinalotokea UKAWA madhara yake hasi watakuja kuyaona hapo baadae.Mimi si mtabiri.
Mwaka 2008 akiwa Waziri mkuu muda wa majaribio(probation) alisomeshwa namba mara ya pili.
Mwaka 2012 uchaguzi ndani ya CCM alifanya kazi kubwa kuhakikisha anawekeza pesa nyingi kupata waNEC na wenyeviti wa wilaya na mikoa mfano nzuri umoja wa wenyeviti na mwenyekiti wao alikuwa Msindai kila mtu anajua Msindai alikuwa anakula na kulala kwa Lowasa na umoja huo ulikuwa unalala na kula kwa Lowasa.Ila najua chadema watakuambia hayo sisi hayatuhusu sisi tunataka kwenda Ikulu.Okey,sawa haina neno sasa kwenye katiba mpya mna lilia MAADILI KWA VIONGOZI WA UMMA YA NINI? NA RAIS NDIO KIOO?
HAYA NIMALIZIE KWA KUSEMA MWAKA 2015-MTOTO WA MJINI MTOTO WA MSOGA NAYE ALITUMIA STAILI ILE ILE YA 1995 yaani leo tunasema COPY &PASTE maana sababu za KUMSOMESHA NAMBA NI ZILE ZILE KAMA ZA 1995.Halafu hivi Mbowe anamfahamu vizuri sana Lowasa kuliko JK?masihala haya.Hivi kweli Upinzani nchi hii wapo serious kweli?
Ule wimbo wa CCM ni ile ile,tumejipanga na mwaka huu utaisoma..ni mahususi kwa Lowasa.CCM ni ile ile kweli ya 1995 na 2015 tulijipanga na akaisoma namba.Lowasa hili analijua fika.
[HASHTAG]#IKULU[/HASHTAG] SIO PANGO LA WALANGUZI#