Kuna wakati mtu unakuwa hufikirii kucomment lakini unajikuta unacomment.
Hivi huyu jamaa ana kitu gani hasa kikubwa?
Uchaguzi ulikuwa mwaka juzi na alishindwa uchaguzi kwa ninavyoamini. Kinachonishangaza ni kuwa hata siku moja kama siyo,TV,gazeti,blogs basi itakuwa radio lazima usikie jina lake! Kwa nini? Nmesoma hii story ingawa sijaelewa maudhui yake lakini nmejikuta nawaza sana kumhusu huyu mtu!
Ni fisadi kama nilivyokuwa naamini kweli,kinachonisumbua sasa kwa nini hakamatwi kwa kesi ya ufisadi? Mahakama maalumu ilianzishwa ya ufisadi,binafsi nilijua kesi namba moja katika mahakama hiyo itakuwa ya huyu jamaa! Kwa sasa tulitangaziwa mahakama haina kesi hata moja,yaani zimemalizika kwa maana hiyo no more fisadiz in Tanzania. Jamaa huyu anapepea tu hata kesi hana,kwa maana hiyo sio fisadi!
Maajabu mengine kwa sasa amekuwa kila anakopita attention inakuwa kubwa sana ni kwa nini?
Juzi kati kapita mjini Geita,ile kusalimia wananchi tu tayari polisi wameshafika na kumchukua kesi gani? Hakuna ila kapewa tu ulinzi?
Inanipa wakati mgumu sana kumwelewa huyu mtu,kwa nini yeye tu? Ana nini? Hili jina lina nguvu gani?
Hivi ni kumpa promo au kummaliza?