Lowassa aisoma namba mara tatu (3) CCM

Lowassa aisoma namba mara tatu (3) CCM

LOWASSA AISOMA NAMBA MARA TATU(3) CCM.

Vijana wengi wa miaka 80,90 na 2000 wanafikiri 2015 hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Lowasa kuisoma namba ndani ya CCM hadi kuamua kwenda kununua nafasi ya kugombea CHADEMA.

Mwaka1995-kwa mara ya kwanza Lowasa anaonja shubiri ya kuisoma namba ndani ya CCM.

Na aliyehakikisha Lowasa anaisoma namba vilivyo ni Baba wa Taifa Mwl.Nyerere na Kamati kuu na kwa sababu kuu mbili.

1.Kununua watu-wajumbe wa halmashauri kuu na mkutano mkuu(RUSHWA)
2.Uadilifu-Niwakumbushe Lowasa huyu mwaka 1995 wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM wakati Mwl.Nyerere na viongozi wengine wamekwenda dodoma kwa usafiri wa magari,Lowasa alikwenda na ndege ya kukodi Chadema watahoji na ukasema kuna shida gani mtu kwenda na ndege wakati pesa ni yake?-AMEKOSA UADILIFU.

Baba wa Taifa Mwl.Nyerere kwenye mkutano wa NEC alihoji huyu kijana pesa hizi za kununua wajumbe na kukodi ndege kazitoa wapi maana mm ninavyomfahamu hana biashara yeyote wala baba yake?

Kubwa zaidi kwenye mkutano huo wa halmashauri kuu(NEC) wakati mwenyekiti Alhaji Ally Hassan Mwinyi,Mwl.Nyerere na wajumbe wa kamati kuu na secretariat wanaingia wajumbe wote walionunuliwa na kupandikizwa na lowasa walisimama na kuimba nyimbo kama ile ya 2015 ya kuwa na imani na Lowasa kama ilivyofanyika 2015 ndio mpate kufahamu yale ni marudio.
Mwl.Nyerere alisimama na kuwauliza hiki ni kikao cha wahuni?.

Akatoa msimamo wake wote wenye imani na Lowasa na si CCM waondoke,hakuondoka mjumbe hata mmoja. Wajumbe wakafanya maamuzi.
HAPA lowasa ANASOMESHWA NAMBA KWA MARA YA KWANZA KWA MSIMAMO WA CCM NA MWL.NYERERE-kwa kukosa uadilifu na matumizi ya Rushwa kutafuta uongozi ndani ya chama.

Leo hii vyama vya upinzani vinasema CCM haishi kwa Matendo Maisha na misimamo ya Baba wa Taifa Mwl.Nyerere,Je huyu Baba wa taifa si yetu sote?Nyinyi wapinzani mnayaishi maisha ya Baba wa Taifa huyo?

Mwaka 2015 wajumbe wa halmashauri kuu(NEC)walichofanya yalikuwa ni marudio ya mkakati ule ule wa mwaka 1995.

Niwarudishe nyuma kidogo Lowasa tokea miaka ya 90 alifanya kazi kubwa ya kujijenga yeye binafsi na si CCM, kwake CCM ilikuwa daraja tu kuelekea Ikulu, na hili leo ndio nilinalotokea UKAWA madhara yake hasi watakuja kuyaona hapo baadae.Mimi si mtabiri.

Mwaka 2008 akiwa Waziri mkuu muda wa majaribio(probation) alisomeshwa namba mara ya pili.

Mwaka 2012 uchaguzi ndani ya CCM alifanya kazi kubwa kuhakikisha anawekeza pesa nyingi kupata waNEC na wenyeviti wa wilaya na mikoa mfano nzuri umoja wa wenyeviti na mwenyekiti wao alikuwa Msindai kila mtu anajua Msindai alikuwa anakula na kulala kwa Lowasa na umoja huo ulikuwa unalala na kula kwa Lowasa.Ila najua chadema watakuambia hayo sisi hayatuhusu sisi tunataka kwenda Ikulu.Okey,sawa haina neno sasa kwenye katiba mpya mna lilia MAADILI KWA VIONGOZI WA UMMA YA NINI? NA RAIS NDIO KIOO?

HAYA NIMALIZIE KWA KUSEMA MWAKA 2015-MTOTO WA MJINI MTOTO WA MSOGA NAYE ALITUMIA STAILI ILE ILE YA 1995 yaani leo tunasema COPY &PASTE maana sababu za KUMSOMESHA NAMBA NI ZILE ZILE KAMA ZA 1995.Halafu hivi Mbowe anamfahamu vizuri sana Lowasa kuliko JK?masihala haya.Hivi kweli Upinzani nchi hii wapo serious kweli?

Ule wimbo wa CCM ni ile ile,tumejipanga na mwaka huu utaisoma..ni mahususi kwa Lowasa.CCM ni ile ile kweli ya 1995 na 2015 tulijipanga na akaisoma namba.Lowasa hili analijua fika.

[HASHTAG]#IKULU[/HASHTAG] SIO PANGO LA WALANGUZI#
Na aliyesoma maazimio kwenye hicho kikao kuwa Monduli hafai ni Mzee Kingunge.
 
Umaskini siyo joho la ufahari, Tatizo kubwa aliloliacha huyo marehemu ni sera ya ujamaa, kuwa utajiri ni jinai, Ndiyo ujinga walio nao watanzania wengi leo. Dunia ya leo imebadilika tupo kwenye utandawazi.
Acha kudanganya wewe au umezaliwa mwaka jana?Nyerere hakukataza utajiri mbona kulikuwepo matajiri wengi tu enzi hizo ,alichopinga na kugomba Nyerere ni kujipatia utajiri kwa njia haramu ikiwa pamoja na kutumia fursa ya cheo au mamlaka kujitajirisha hasa kwa watumishi wa umma ndio maana babu yako aliulizwa hizi pesa za kujenga mahekalu umezipata wapi kwani tunajua hujawahi kuwa mfanyabiashara au muekezaji,kwa hiyo acha kudanganya kuwa Mwalimu alikuwa anachukia utajiri na sio kwamba siasa ya ujamaa inakumbatia umasikini kasome tena misingi ya siasa ya ujamaa kabla hujaanza kutulisha sumu
 
Kwa jicho la tatu sambamba na ukweli mchungu, mamvi kaja kuua upinzani.....ni kosa kubwa sana la kiufundi ukawa walifanya kumpokea just kwa ajili ya urais tu.
wafuasi wake watakujibu ameongeza viti vya wabunge wakati ukweli ni kwamba ccm ya kikwete wananchi wengi waliichoka kwa drama zake.
tungeweza kufanya vizuri na bado tukabaki na upinzani unaoaminika tofauti na ilivyo leo, upinzani maslahi na hata wengne waliokuja na mamvi (akina msindai) wamerejea magambani!

Kumpokea Lowasa upinzani na moja kwa moja kumpa bendera ya ukawa lazima tukubali kumefanya vita ya kuing'oa ccm kuwa ngumu maradufu. Mosi, kuja kwake upinzani kumeiua kabisa sera ya upinzani ya kupambana na ufisadi, sera ambayo ndio ilikuwa karata dume kwa upinzani. Pili, kuja kwake kukaigawa ukawa katika makundi, kundi la Slaa/Lipumba na kundi la wale waliomkaribisha na kumpa bendera. Tatu, ujio na ugombea wake ulishindwa kukidhi mategemeo ya wengi kwa kushindwa kwakwe kulimudu jukwaa la kampeni, kiasi cha kutoongea zaidi ya dakika 5. Mashabiki tulitegemea Lowasa amudu vyema jukwaa kwa kuelezea wapi angeipeleka nchi. Kama Lowasa atagombea tena 2020 basi aanze kujenga uwezo wa kulimudu jukwaa na kuongea na wananchi kwa muda unaokubalika.

That said, nadhani ukawa kama wangekuwa tu wamemkaribisha Lowasa pasipo kumpa bendera au cheo chochote Ukawa wangekuwa wamerahisisha vita vya kuing'oa ccm maana angeleta mtaji wa watu ambao wangeungana badala ya kugawanyika. Haya ni mawazo yangu ambayo kamwe silazimishi yakubalike.
 
LOWASSA AISOMA NAMBA MARA TATU(3) CCM.

Vijana wengi wa miaka 80,90 na 2000 wanafikiri 2015 hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Lowasa kuisoma namba ndani ya CCM hadi kuamua kwenda kununua nafasi ya kugombea CHADEMA.

Mwaka1995-kwa mara ya kwanza Lowasa anaonja shubiri ya kuisoma namba ndani ya CCM.

Na aliyehakikisha Lowasa anaisoma namba vilivyo ni Baba wa Taifa Mwl.Nyerere na Kamati kuu na kwa sababu kuu mbili.

1.Kununua watu-wajumbe wa halmashauri kuu na mkutano mkuu(RUSHWA)
2.Uadilifu-Niwakumbushe Lowasa huyu mwaka 1995 wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM wakati Mwl.Nyerere na viongozi wengine wamekwenda dodoma kwa usafiri wa magari,Lowasa alikwenda na ndege ya kukodi Chadema watahoji na ukasema kuna shida gani mtu kwenda na ndege wakati pesa ni yake?-AMEKOSA UADILIFU.

Baba wa Taifa Mwl.Nyerere kwenye mkutano wa NEC alihoji huyu kijana pesa hizi za kununua wajumbe na kukodi ndege kazitoa wapi maana mm ninavyomfahamu hana biashara yeyote wala baba yake?

Kubwa zaidi kwenye mkutano huo wa halmashauri kuu(NEC) wakati mwenyekiti Alhaji Ally Hassan Mwinyi,Mwl.Nyerere na wajumbe wa kamati kuu na secretariat wanaingia wajumbe wote walionunuliwa na kupandikizwa na lowasa walisimama na kuimba nyimbo kama ile ya 2015 ya kuwa na imani na Lowasa kama ilivyofanyika 2015 ndio mpate kufahamu yale ni marudio.
Mwl.Nyerere alisimama na kuwauliza hiki ni kikao cha wahuni?.

Akatoa msimamo wake wote wenye imani na Lowasa na si CCM waondoke,hakuondoka mjumbe hata mmoja. Wajumbe wakafanya maamuzi.
HAPA lowasa ANASOMESHWA NAMBA KWA MARA YA KWANZA KWA MSIMAMO WA CCM NA MWL.NYERERE-kwa kukosa uadilifu na matumizi ya Rushwa kutafuta uongozi ndani ya chama.

Leo hii vyama vya upinzani vinasema CCM haishi kwa Matendo Maisha na misimamo ya Baba wa Taifa Mwl.Nyerere,Je huyu Baba wa taifa si yetu sote?Nyinyi wapinzani mnayaishi maisha ya Baba wa Taifa huyo?

Mwaka 2015 wajumbe wa halmashauri kuu(NEC)walichofanya yalikuwa ni marudio ya mkakati ule ule wa mwaka 1995.

Niwarudishe nyuma kidogo Lowasa tokea miaka ya 90 alifanya kazi kubwa ya kujijenga yeye binafsi na si CCM, kwake CCM ilikuwa daraja tu kuelekea Ikulu, na hili leo ndio nilinalotokea UKAWA madhara yake hasi watakuja kuyaona hapo baadae.Mimi si mtabiri.

Mwaka 2008 akiwa Waziri mkuu muda wa majaribio(probation) alisomeshwa namba mara ya pili.

Mwaka 2012 uchaguzi ndani ya CCM alifanya kazi kubwa kuhakikisha anawekeza pesa nyingi kupata waNEC na wenyeviti wa wilaya na mikoa mfano nzuri umoja wa wenyeviti na mwenyekiti wao alikuwa Msindai kila mtu anajua Msindai alikuwa anakula na kulala kwa Lowasa na umoja huo ulikuwa unalala na kula kwa Lowasa.Ila najua chadema watakuambia hayo sisi hayatuhusu sisi tunataka kwenda Ikulu.Okey,sawa haina neno sasa kwenye katiba mpya mna lilia MAADILI KWA VIONGOZI WA UMMA YA NINI? NA RAIS NDIO KIOO?

HAYA NIMALIZIE KWA KUSEMA MWAKA 2015-MTOTO WA MJINI MTOTO WA MSOGA NAYE ALITUMIA STAILI ILE ILE YA 1995 yaani leo tunasema COPY &PASTE maana sababu za KUMSOMESHA NAMBA NI ZILE ZILE KAMA ZA 1995.Halafu hivi Mbowe anamfahamu vizuri sana Lowasa kuliko JK?masihala haya.Hivi kweli Upinzani nchi hii wapo serious kweli?

Ule wimbo wa CCM ni ile ile,tumejipanga na mwaka huu utaisoma..ni mahususi kwa Lowasa.CCM ni ile ile kweli ya 1995 na 2015 tulijipanga na akaisoma namba.Lowasa hili analijua fika.

[HASHTAG]#IKULU[/HASHTAG] SIO PANGO LA WALANGUZI#
Duuh.... uliposema anasomeshwa namba nilidhani na yeye anakula mlo mmoja kama mimi na wewe!!....
 
Kumpokea Lowasa upinzani na moja kwa moja kumpa bendera ya ukawa lazima tukubali kumefanya vita ya kuing'oa ccm kuwa ngumu maradufu. Mosi, kuja kwake upinzani kumeiua kabisa sera ya upinzani ya kupambana na ufisadi, sera ambayo ndio ilikuwa karata dume kwa upinzani. Pili, kuja kwake kukaigawa ukawa katika makundi, kundi la Slaa/Lipumba na kundi la wale waliomkaribisha na kumpa bendera. Tatu, ujio na ugombea wake ulishindwa kukidhi mategemeo ya wengi kwa kushindwa kwakwe kulimudu jukwaa la kampeni, kiasi cha kutoongea zaidi ya dakika 5. Mashabiki tulitegemea Lowasa amudu vyema jukwaa kwa kuelezea wapi angeipeleka nchi. Kama Lowasa atagombea tena 2020 basi aanze kujenga uwezo wa kulimudu jukwaa na kuongea na wananchi kwa muda unaokubalika.

That said, nadhani ukawa kama wangekuwa tu wamemkaribisha Lowasa pasipo kumpa bendera au cheo chochote Ukawa wangekuwa wamerahisisha vita vya kuing'oa ccm maana angeleta mtaji wa watu ambao wangeungana badala ya kugawanyika. Haya ni mawazo yangu ambayo kamwe silazimishi yakubalike.
Acha uongo.... mbona vyama vya upinzani vya Zimbabwe havijawahi kuchukua mstaafu yeyote wa serikali ya Mugabe lakini bado hawajawahi kushinda....
Ebu rudi kwenye misingi ya Afrika na ushuuda wa Trump ndio utajua kwa nini wapinzani katika nchi za Africa hawashiki dola.
 
Haya ndo matatizo ya nchi kuwekeza kwenye ujinga ambao huzaa umaskini! Ina maana kupanda ndege ni anasa? Hapa nna rafiki zangu wao wakipata likizo, wenye hela hupanda ndege na wasio na hela hupanda basi lakin tunachukulia maisha ya kawaida. Hata sasa bado kuna watu wanadhani kuishi maisha duni ndo ishara ya uadilifu!! Nonsense!
Alichohoji Mwl Nyerere sio kupanda ndege bali matumizi makubwa ya fedha kwa mtumishi wa umma ikiwemo kukodi ndege yote haya katika harakati za kuusaka urais.
 
Kwani kutumia pesa nyingi ni kosa? Kama pesa ninazo shida iko wapi kutumia pesa? Hivi mtumishi wa serikali hana haki ya kutafuta pesa na kutumia anavyotaka? Maana hii poor mentality inarithiwa kizazi na kizazi yaani mtumishi wa serikali ukiwa na hela, ukifanikiwa unaitwa mwizi. Bado tuna safari
 
Haya ndo matatizo ya nchi kuwekeza kwenye ujinga ambao huzaa umaskini! Ina maana kupanda ndege ni anasa? Hapa nna rafiki zangu wao wakipata likizo, wenye hela hupanda ndege na wasio na hela hupanda basi lakin tunachukulia maisha ya kawaida. Hata sasa bado kuna watu wanadhani kuishi maisha duni ndo ishara ya uadilifu!! Nonsense!
Tusaidie kidogo hao rafiki zako WANAPANDA /WANAKODI ndege?
 
Umaskini siyo joho la ufahari, Tatizo kubwa aliloliacha huyo marehemu ni sera ya ujamaa, kuwa utajiri ni jinai, Ndiyo ujinga walio nao watanzania wengi leo. Dunia ya leo imebadilika tupo kwenye utandawazi.
Sio kweli utajiri wowote alionao mtu unaotokana na exploitation ya nguvu za watu wengine duniani kote huchukuliwa kama jinai.
 
Nimeamini Lowassa anawaumiza sana sisiemu. Maana kila mahali wanapambana naye tuu. Si wamfunge tuu awe gerezani maana uwezo wanao wakiamua kwa kuelekezwa na dikiteta toka chato.
 
Acha kudanganya wewe au umezaliwa mwaka jana?Nyerere hakukataza utajiri mbona kulikuwepo matajiri wengi tu enzi hizo ,alichopinga na kugomba Nyerere ni kujipatia utajiri kwa njia haramu ikiwa pamoja na kutumia fursa ya cheo au mamlaka kujitajirisha hasa kwa watumishi wa umma ndio maana babu yako aliulizwa hizi pesa za kujenga mahekalu umezipata wapi kwani tunajua hujawahi kuwa mfanyabiashara au muekezaji,kwa hiyo acha kudanganya kuwa Mwalimu alikuwa anachukia utajiri na sio kwamba siasa ya ujamaa inakumbatia umasikini kasome tena misingi ya siasa ya ujamaa kabla hujaanza kutulisha sumu
Mawaidha maridhawa kwa kizazi kipya.
 
Bc endelea kumfagia huyu mpumbavu wenu magu asiye na hekima wala busara ila nakuhakikishia utaisoma namba adi bibi yako afufuke mana naona kichw box huoni mbele wala nyuma pumbavu ww
 
Huyu mzee ni jeshi la mtu mmoja linalo sumbua mamilioni ya wana ccm
 
Kwani kutumia pesa nyingi ni kosa? Kama pesa ninazo shida iko wapi kutumia pesa? Hivi mtumishi wa serikali hana haki ya kutafuta pesa na kutumia anavyotaka? Maana hii poor mentality inarithiwa kizazi na kizazi yaani mtumishi wa serikali ukiwa na hela, ukifanikiwa unaitwa mwizi. Bado tuna safari
This is not a poor mentality but according to the ethics. Je unajua ni kwa nini kuna tume ya maadili na kwa nini kila kiongozi wa umma anatakiwa kujaza fomu ya kueleza mali anazomiliki na kutokujaza fomu hii au hata kutuoa maelezo ya uongo ni kosa?kwa mtumishi wa umma kuwa na fedha nyingi sio kosa lakini lazima ijulikane chanzo cha mapato yake isije ikawa ni nafasi au cheo alichonacho huu ni utaratibu unaotumika katika nchi nyingi duniani. Sasa tukirudi kwa Mh Lowasa yeye alikuwa ni kiongozi wa umma katika nyadhifa mbali mbali na kwa taarifa yako Mwl Nyerere alikuwa anamjua Lowasa IN and OUT kiliko mimi na wewe tunavyofikiri kumjua ndio maana kwa wanokumbuka Mwl alitamka "Hawa vijana wanapata wapi fedha......"
 
Sio kweli utajiri wowote alionao mtu unaotokana na exploitation ya nguvu za watu wengine duniani kote huchukuliwa kama jinai.
Na siyo Kila tajiri ametajirika Kwa means of exploitation, Kuna wengine utajiri kwao ni Lazima. Matajiri wapo kabla Yesu hajazaliwa huwezi kuwazuia au kuwalaani. Utajiri siyo Dhambi.
 
Acha kudanganya wewe au umezaliwa mwaka jana?Nyerere hakukataza utajiri mbona kulikuwepo matajiri wengi tu enzi hizo ,alichopinga na kugomba Nyerere ni kujipatia utajiri kwa njia haramu ikiwa pamoja na kutumia fursa ya cheo au mamlaka kujitajirisha hasa kwa watumishi wa umma ndio maana babu yako aliulizwa hizi pesa za kujenga mahekalu umezipata wapi kwani tunajua hujawahi kuwa mfanyabiashara au muekezaji,kwa hiyo acha kudanganya kuwa Mwalimu alikuwa anachukia utajiri na sio kwamba siasa ya ujamaa inakumbatia umasikini kasome tena misingi ya siasa ya ujamaa kabla hujaanza kutulisha sumu
Sikushangai kunijibu randomly, kwa kuwa avatar name yako inatosha ku,reflect mawazo yako.
Kabla sijaendelea Nahitaji unambie una elimu gani??? Au umtafute mtu aliyekuzidi elimu, mwambie akwambie misingi ya Ujamaa, Lengo la Ujamaa,
Nahitaji hoja siyo maswala ya umri please. Kama huna kausha.
 
Na siyo Kila tajiri ametajirika Kwa means of exploitation, Kuna wengine utajiri kwao ni Lazima. Matajiri wapo kabla Yesu hajazaliwa huwezi kuwazuia au kuwalaani. Utajiri siyo Dhambi.
Hoja ya msingi ni uhalali wa mali na hakuna dhambi kumiliki mali na ni sehemu ya baraka suala lililozua mjadala hapa ni viongozi wa umma kutumia firsa au vyeo vyao kujilimbikizia mali.
 
Hata Mimi nakubali Lowassa alisoma namba lkn kwasasa ni zamu ya wananchi kusoma namba hadi za kirumi zikisomeshwa na mtukufu MKUU kwa wapiga kura wake maskini. Mwafaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom