palalisote
JF-Expert Member
- Aug 4, 2010
- 8,335
- 1,455
"Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa na kuitwa fisadi kwanini?".
"Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,
"Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo".
"Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,"
Mkuu ebu acheni Ujinga wengine hapa tunatumia akili na sii masaburi... Sasa kama habari hii ni yakweli.. Lowassa alijuaje na kutaka kuuvunja mkataba ikiwa mkataba ulikuwa wa JK rais wake....Halafu JK kusema tu alikuwa akipata ushauri wa makatibu wake (watendaji wa kiserikali) inaonyesha wazi JK alikuwa akifuata sheria na taratibu za kiserikali laa sivyo asingewahusisha makatibu wakuu kama alivyofanya Lowassa na ushahidi upo akiwaamrisha hao makatibu na waziri wafuate maagizo yake....Tafuta jingine!
Hayo ya 1997 we are interested ni kujikosha na kutafuta huruma za JK...Hata mahakamani mkosa baada ya kupatikana na kmakosa, hupewa muda wa kuomba, kujieleza kabla ya kuhukumiwa kifungo..
Wacha hasira mkuu Lowasa anaonekana ana mengi ya kutueleza ila ukumbuke mwanasiasa huongea ukweli kwenye jina lake tuu na sio hoja zake na mengineyo...lowasa haitaji huruma za jk bali jk ndio anahaha atamfadhili vipi lowasa kwa kufichiana siri...ikumbukwe kama jk angejiuzulu yeye ingekuwa balaa zaidi ndio maana akamuomba lowasa abebe adhabu yake ili aweze kujilinda na kumlinda yeye siasa mchezo wa hila
Lowassa na Chenge wameshawajibishwa huko Dodoma au bado?
Ngoma inogile asante mkuu kwa update maana huku kwetu hakuna access ya magazeti..well said Lowasa aka kondoo wa kafara naamini lowasa ana mengi zaidi ya hayo..
we mjinga! Jifunike kichwani maana naona umeacha blanketi likashuka sakafuni. Halafu morning uje humu jamvini. Unakurupuka tu!Lowassa na Chenge wameshawajibishwa huko Dodoma au bado? Ni kwa sababu gani aliamua KUTUFICHA mpaka leo hii sisi walipakodi?
Lowassa mwizi tu anawaleeza nyie mlokuwepo chama na kumwona kwenda kanisani basi mnafikiri mtu mzuri sana..Kama yeye alikuwa mkweli kwa nini asiwahutubie Umma mzima wa Watanzania badala yake anaenda katika mikutano ya chama! anajua huko mmejaa masaburi watupu. Kikao cha chama CC wanatokea watu wanafokea wengine as if wao ni Miungu!..damn.Wacha hasira mkuu Lowasa anaonekana ana mengi ya kutueleza ila ukumbuke mwanasiasa huongea ukweli kwenye jina lake tuu na sio hoja zake na mengineyo...lowasa haitaji huruma za jk bali jk ndio anahaha atamfadhili vipi lowasa kwa kufichiana siri...ikumbukwe kama jk angejiuzulu yeye ingekuwa balaa zaidi ndio maana akamuomba lowasa abebe adhabu yake ili aweze kujilinda na kumlinda yeye siasa mchezo wa hila
nimejaribu kunukuu sehemu tu inayoendana na kichwa cha thread hii. Wakati mwingine "acknowledge" chanzo cha taarifa.Mkuu ungweka kabisa hivi:
soma #2 habari nzima utaelewa mkuu, issue yao imerudishwa cc?? wanaboa kinoma
Kesha edit sii unajua Wabongo kwa kamba!!! hainogi bila kuongeza chunvi...nimejaribu kunukuu sehemu tu inayoendana na kichwa cha thread hii. Wakati mwingine "acknowledge" chanzo cha taarifa.