Lowassa ahusishwa na ufisadi ukodishwaji Mbowe Hotels Ltd

Lowassa ahusishwa na ufisadi ukodishwaji Mbowe Hotels Ltd

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,505
Reaction score
16,006
Lowassa akiwa waziri wa ardhi alimwelekeza aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa NHC Haruna Masebo auze jingo la NHC ilipo Bills Kwa Mbowe Hotels Ltd hata hivyo mwenyekiti wa Bodi Emilius Mzena aliishauri serikali/ikulu kuwa isingewezekana.

Baada ya kushindikana Lowassa akahakikisha NHC na Mbowe Hotels Ltd wanaingia mkataba tata ambao Mbowe hotels walimilikishwa 75% umiliki wa jengo na 25% kubaki kinyume na Taratibu, ingewezekana hivyo kama NHC walitoa ardhi tupu..lakini uhalisia ni kwamba Mbowe Hotels walikuta jengo.

Mbowe Hotels wameshindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba toka mwaka 1993 ambao uliwataka kujenga hoteli ya kisasa yenye vyumba 100,kumbi za kisasa na CASINO ambavyo havijafanyika, uwekezaji ungegharimu milioni 720 mwaka 1993.

NHC walianza mchakato wa kuvunja mkataba februari,2015 pamoja na kuwadai Mbowe Hotels Limbikizo la kodi la zaidi ya shilingi bilioni moja ambapo kwa sasa Mbowe Hotels wanatakiwa kurudisha majengo na kulipa ndani ya siku chache kuanzia sasa.

Chanzo; (Daily News 26.08.2016)
=======

Maoni yangu.

Kwa wale walipo Dar mtakuwa mashahidi kwa takribani miaka miwili/mitatu hii klabu ya bills imedorora na kwa siku za karibuni Lowassa/Mbowe wamekuwa akifanyia vikao vya CHADEMA/BAVICHA/CHASO nk.

Mbowe ni Lazima ulipe kodi ya jengo hilo ili uonyeshe kuwajibika kama kiongozi na sio kutumia vijana kukutetea kwa mambo wasiyoyajua kuhusu biashara na familia.

Mbowe ana historia ya kutokuwa mlipaji mzuri wa mikopo kwani hata NSSF kwa muda mrefu wamesumbuana naye kwa mkopo waliompatia miaka ya 90 wa takrikani shilingi bilioni moja.

Chanzo cha migogoro mingi ya ardhi hasa viwanja vya serikali viliasisiwa na Lowassa alipokuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi. Alijitwalia ardhi Masaki alipojengewa na mabwanyenye nyumba amepangisha ubalozi wa Afrika Kusini katika muda mfupi akiwa waziri, familia yake na marafiki wanamiliki viwanja vingi vyenye utata hasa katika wilaya ya kinondoni na CBD. Mtakumbuka mwaka jana kuna nyumba Tegeta ilibomolewa na mwanafamilia wa Lowassa katika kugombania ardhi.
 
SO SAD
20160826_045820.jpg
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kweli ngoma imekolea.
 
Nyumba nyingi za NHC zilirudishwa kwa wamiliki wa awali katika mazingira tata wakati akiwa waziri wa ardhi!
Si vema kufukua makaburi lakini katika hili kuna maiti inaweza kufufuliwa.
 
1993 - 2016 ni miaka zaidi ya 23 sasa, imepita awamu ya Mwinyi, Nkapa, JK na hawakuwahi kuliona hili. Huyu bosi wa NHC wa sasa amatumia mabilioni ya wanyonge ambao ndio wamiliki wa NHC kujenga majumba kwa ajili ya kumilikisha matajiri na mafisadi kwa kipindi alichokuwepo na hakuwahi kuliona hili pia hadi harakati za UKUTA zilivyoanza!
Ninachojua katika biashara ni kwamba hakuna kampuni isiyofanya mahesabu kila mwaka kwa maana profit & loss na biashara na pande mbili za sarafu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]daaaaaaa iv unakisikia unachokiongea kwel.... Mtamtafuta sana lakin hiyo yote ni kumchafulia jina lowasa.....
 
Kizazi hiki hakitekwi na propaganda za kizamani za kutaka kuwachafua wanasiasa wanaowapinga. Tumieni mbinu nyingine.
 
Mmmmmmmh ndio maana watanzania hatutafika mbali maana wengi ni wajuaji sana.
 
Makelele meengi kumbe ndio source ya matatizo. Na bado tar 1. Things are falling apart
 
Tangu 1985baada ya Mwalimu J.K. Nyerere kung'atuka hakuna kiongozi mkuu ndani ya chama chao na serikali ambaye aliondoka/kustaafu bila kuwa na kashfa ya ulaji/ufujaji/wizi/kutofuata taratibu n.k,enzi ya ruksa tunajua yaliyotokea,enzi ya Ben tumeyashuhudia,ya Jakaya tunayajua na hata aliopo sasa akitoka tutayasikia pamoja na kwamba mengine yanajulikana.
 
Back
Top Bottom