Lowasa kazuiwa kuzungumzia hatima yake

Lowasa kazuiwa kuzungumzia hatima yake

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
2,956
Reaction score
1,116
Wanajamvi anayejua Lowasa yuko wapi atujuze. Wafuasi wake wamechanganyikiwa. Atoe tamko watu watulie ccm au waisambaratishe.
 
Lowasa yuko dar.jana tulikuwa naye kwenye harusi flani apa town
 
Mzee bado haoni vizuri, anaona **** kutokana nna kibao cha uso alichozabwa. Mwacheni atulize maumivu.
 
Lowasa sema kitu chama chako kikisambatatika utatuletea machafuko kwani wenye chama wenzako hawataachia ngazi kirahisi.!


WAZIRI mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amepanga wakati wowote kutoka sasa, kumkatia rufaa Rais Jakaya Kikwete. Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki zinasema, Lowassa amepanga kukutana na waandishi wa habari, Jumatatu au Jumanne wiki hii. Mkutano kati ya Lowassa na vyombo vya habari, unalenga kumshitaki Kikwete kwa wananchi kwa kile kinachoitwa, “kukaidi matakwa ya wengi.”

Lowassa alikuwa miongoni mwa wanachama 38 wa chama hicho waliojitosa katika mbizo za urais, lakini jina lake liliondolewa katika hatua za awali. Kikwete ndiye anayetajwa kumuengua Lowassa kwa maslahi yake binafsi. “Ni kweli kwamba Edo (Edward Lowassa), amepanga kueleza kilichotokea Dodoma kwenye mikutano ya chama chake. Atafanya hivyo kupitia mkutano kati yake na waandishi wa habari,” ameeleza mmoja wa watu waliokaribu na kiongozi huyo.

Haikuweza kufahamika mara moja, ikiwa Lowassa atautumia mkutano huo kueleza mustakabali wake wa baadaye wa kisiasa. Hata hivyo, mwishoni mwa wiki, madiwani 20 kutoka jimboni kwake Monduli, walitangaza kukihama CCM na kujiunga na Chadema; jambo ambalo linadaiwa na wachambuzi wa kisiasa kuwa ni maandalizi ya mwanasiasa huyo kukimbilia Chadema.

Chanzo: MwanaHalisi Online
 
Sidhani kama atatoa tamko. Ni bora akae tu kimya.
 
Sidhani kama atatoa tamko. Ni bora akae tu kimya.


Kukaa kimya wakati mafuriko yanajitafutia njia siyo sahihi. Bora ajitokeze na kuyaongoza mafuriko yake ili madhara yaweza kuwa under control!
 
Ata aje malaika agombee kwa ccm atageika na kuwa pepo kama lusifa alivyogeuka na kuwa shetani.
 
Back
Top Bottom