Lowasa jifunze kwa mrema

Lowasa jifunze kwa mrema

navy boi

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2014
Posts
1,520
Reaction score
482
LOWASA JIFUNZE KWA MREMA:

Mwaka 1995 ni mwaka ambao chama cha upinzani cha NCCR Mageuzi iliaminika kitakitoa madarakani Chama Cha Mapinduzi kwakuwa kilionesha upinzani mkubwa sana na kuungwa mkono kulikokithiri hata gari la mgombea wake, Ndugu Mrema kusukumwa na wanachama kwa mapenzi yao

Baada tu ya kuanguka kwenye uchaguzi huo Mh. Mrema alipata maradhi na hadi sasa afya yake haijakaa sawa, kila kukicha madaktari wanagundua tatizo jipya kwake. Mh. Mrema amefilisika kisiasa hali iliyomsababisha kugombea nafasi ya Ubunge badala ya Urais kwakuwa hata afanyeje hatoweza tena kupata ushabiki

Mtu aliyeweka rekodi ya kujiuzuru wadhifa wake, mtu aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania, mtu aliyeondoka kwenye chama chake na kujiunga kwenye chama kingine cha upinzani, hali kadhalika mtu mwenye afya dhaifu anayefanana kila sifa na ndugu Mrema naye anakwenda kugombea nafasi ile ile ya Urais.

Tofauti kubwa iliyopo kati ya Lowassa na Mrema ni kwamba Mrema aliondoka CCM akiwa shujaa na mtetezi wa haki za wanyonge, aliondoka mwenyewe baada ya kupishana misimamo na chama chake cha Mapinduzi. Lowassa ameondoka CCM baada ya kukatwa jina huku akiwa na kashfa za wizi wa mabilioni ya shilingi na kujilimbikizia mali za umma ikiwemo ranchi za Handeni na Mkata

Kitu kinachokatisha tamaa ni kuona chama kile kile ambacho hakina wanachama wengi kama ilivyo kwenye Chama Cha Mapinduzi, CCM chenye wanachama na uongozi wa chama kila baada ya nyumba kumi, mashina na matawi kila kijiji nchi nzima ndicho kinachokwenda kupeperusha bendera kwa Waziri huyo aliyejiuzulu.

Historia inakwenda kujirudia kwa mara nyingine tena, yaliyotokea 1995 inakwenda kujirudia tena 2015 baada ya miaka 20. Mwenzake keshanyolewa, yeye anapaswa kutia maji.

Pole sana ndugu EL na wenzako wanaokushauri negative.
 
MAGUFULI NA HAPA KAZI TUU!!
Kauli mbiu ya CCM (Hapa kazi tu) na Uchapaji kazi wa Mgombea wake Dr. J.P.Magufuli inaonyesha dhamira ya dhati ya chama hicho katika kumkomboa Mtanzania.Ni dhahiri kwamba tutaijenga nchi yetu kwa sisi wote kuungana na kwa kila mtu kutekeleza wajibu wa kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi hii,hatuwezi kuwa tunataka maslahi yetu ya watanzania ya afya bora,maisha bora na elimu nzuri lakini eti unadhani una mtu ambaye atakuja kukuletea maslahi hayo!Watanzania tubadilike,tunahitajika kiongozi mchapakazi,kujituma na kufanya kazi ipasavyo!!
 
Mimi nikisikia hawa ukawa wanashabikia nawashangaa kabisa nchi hii kuna kundi la maharamia wanaitolea macho gas dhahabu tunawajua kwa majina na ndio wanampa jeuri huyu raisi jamani watanzania mtauzwa mchana huyu mgomea ni kivuli cha uraisi kati ya kundi fulani
 
Na asiye toka kwenye chama kinacho chakata na kuzalisha mafisadi. Watanzania tuseme ccm imetosha
 
Ww kwanza mke. Wa mtu. Unatafuta nn humu utaishia kugongwa bureee.
 
Na asiye toka kwenye chama kinacho chakata na kuzalisha mafisadi. Watanzania tuseme ccm imetosha

Ambacho lowasa kawemo kea miaka 39 na leo anataka kuwaletea mabadiliko?
 
LOWASA JIFUNZE KWA MREMA:
Tofauti kubwa iliyopo kati ya Lowassa na Mrema ni kwamba Mrema aliondoka CCM akiwa shujaa na mtetezi wa haki za wanyonge, aliondoka mwenyewe baada ya kupishana misimamo na chama chake cha Mapinduzi. Lowassa ameondoka CCM baada ya kukatwa jina huku akiwa na kashfa za wizi wa mabilioni ya shilingi na kujilimbikizia mali za umma ikiwemo ranchi za Handeni na Mkata

Pole sana ndugu EL na wenzako wanaokushauri negative.

Hapa nakubaliana na wewe kabisaa. Mrema alikuwa shujaa wa wanyonge wakati Lowassa hajawahi hata kukutana na wanyonge mpaka ilipobidi kupanda Dala Dala kuwalaghai Walala hoi.
 
Mimi nikisikia hawa ukawa wanashabikia nawashangaa kabisa nchi hii kuna kundi la maharamia wanaitolea macho gas dhahabu tunawajua kwa majina na ndio wanampa jeuri huyu raisi jamani watanzania mtauzwa mchana huyu mgomea ni kivuli cha uraisi kati ya kundi fulani

Hizi propaganda zilisha chuja miaka mingi sana, eti tutauzwa mchana!! tuuzwe mala ngapi? kuna kilichobakia ambacho hakijauzwa?? Sasa ndio muda wa kuvirudisha vyote vilivyouzwa tena kitapeli, bora hata ingekuwa halali, tungeona hiyo pesa, iko wapi. Mwaka huu tuna nyie tu.
 
Hapa nakubaliana na wewe kabisaa. Mrema alikuwa shujaa wa wanyonge wakati Lowassa hajawahi hata kukutana na wanyonge mpaka ilipobidi kupanda Dala Dala kuwalaghai Walala hoi.

Labda ulikuwq mtoto au hujazaliwa. Mrema alifukuzwa CCM for your information
 
Mimi nikisikia hawa ukawa wanashabikia nawashangaa kabisa nchi hii kuna kundi la maharamia wanaitolea macho gas dhahabu tunawajua kwa majina na ndio wanampa jeuri huyu raisi jamani watanzania mtauzwa mchana huyu mgomea ni kivuli cha uraisi kati ya kundi fulani

Mimi Najiuliza ataongozwa na watu gani, wenye maslahi gani waliyoyalenga? Ndicho nachojiuliza
 
Usilinganishe NCCR ile na UKAWA hii utakuwa unajidanganya ndugu yng
 
Back
Top Bottom