Lowasa aukana urais

Lowasa aukana urais

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,956
Reaction score
25,345
Lowasa ameukana urais kwa kudai kwamba ‘urais ni uchuro’. Akiongea na vijana waendesha bodaboda kwenye mkutano wa hadhara, mara vijana hao walianza kuimba: “rais, rais, rais, rais wetu wa 2015”. Lowasa aliwakataza waache kumuita hivyo kwani urais ni uchuro na kwamba kufanya hivyo watakuwa wanamchonganisha na watu. Lowasa aliwaahidi vijana hao kuwachangia fedha ili kila mmoja amiliki chombo chake cha usafiri.

Source: Lowasa mwenyewe:israel:
 
Umiliki wa chombo cha usafiri kwa vijana kunawasaidaje vijana kumuwezesha kuwa na maendeleo endelevu (sustainable development) ukizingatia changamoto za kumiliki chombo hicho?
 
Ktk viongozi ambao Chama Cha MIZIGO kimebahatika kuwapata ni pamoja na Huyu EL!HOFU NI AFYA YAKE HAWEZI KUKAA MADARAKANI KWA ANGALAU KWA 5YRS,
 
Always, ukweli ni mchungu, lakini inabidi usemwe.
Lowassa ni fisadi, ni kweli, lakini watanzania wengi wanamkubali, huo nao ni ukweli hata kama hatuutaki.
Katika pita pita zangu kila sehemu ninayofika hata kama ni safari za mikoani huwa najaribu kuchokoza mada za siasa ili kupata mawazo yao. Wengi wanajua kuwa jamaa ana kashfa, ila wanasema ni mchapakazi. Wengi wanasema kama Lowassaa atapitishwa kuwa mgombea bila shaka watampa kura yao. Naomba msinishambulie mimi mgeni jukwaani bandugu:lock1:
 
kwani kuna utafiti umefanyika kujua kwamba anapendwa?
 
Always, ukweli ni mchungu, lakini inabidi usemwe.
Lowassa ni fisadi, ni kweli, lakini watanzania wengi wanamkubali, huo nao ni ukweli hata kama hatuutaki.
Katika pita pita zangu kila sehemu ninayofika hata kama ni safari za mikoani huwa najaribu kuchokoza mada za siasa ili kupata mawazo yao. Wengi wanajua kuwa jamaa ana kashfa, ila wanasema ni mchapakazi. Wengi wanasema kama Lowassaa atapitishwa kuwa mgombea bila shaka watampa kura yao. Naomba msinishambulie mimi mgeni jukwaani bandugu:lock1:

Unaposema Watanzania wengi wanamkubali, una ushahidi?? Maana hata hapa JF tukipiga kura sidhani kama tunaweza kupata hayo matokeo unayoyakadiria!! Hizo pesa za marafiki zake anazozigawa hovyo hovyo ndizo zitampeleka choonini 2015!!
 
Lowasa ameukana urais kwa kudai kwamba ‘urais ni uchuro'. Akiongea na vijana waendesha bodaboda kwenye mkutano wa hadhara, mara vijana hao walianza kuimba: "rais, rais, rais, rais wetu wa 2015". Lowasa aliwakataza waache kumuita hivyo kwani urais ni uchuro na kwamba kufanya hivyo watakuwa wanamchonganisha na watu. Lowasa aliwaahidi vijana hao kuwachangia fedha ili kila mmoja amiliki chombo chake cha usafiri.

Source: Lowasa mwenyewe:israel:

We bwana acha uongo,hajasema urais ni uchuro,hebu jaribu kuwa unasikiliza vizuri magazeti na kusema ama kuandika kama kilivyosemwa ama kuandikwa ktk magazeti ya leo.
Ila kwa mwaka 2015 ni wazi tu kuwa E,L ndio atakayekuwa Rais wa nchi hii kama tu atapewa nafasi na chama chake,maana lengo la vyama ni kushika dola na ni lazima asimame mtu mwenye mvuto na ushawishi kwa watu wa lika zote,E.L ni moja kati ya watu hao,ama magufuli,lakini kama tutataka rais mwanamke basi Mama rose anaweza pata nafasi hiyo.
 
Unaposema Watanzania wengi wanamkubali, una ushahidi?? Maana hata hapa JF tukipiga kura sidhani kama tunaweza kupata hayo matokeo unayoyakadiria!! Hizo pesa za marafiki zake anazozigawa hovyo hovyo ndizo zitampeleka choonini 2015!!

Huyu jamaa pekee atafanya kitu akiwa rais..
Wabunge tuweke vijana... sio hawa wanaoongoza kwa mazoea
 
Utendaji ktk siri kali hii uliishia enzi za Lowassa.
Saiz ni maneno tu... wapigwe tu... Halafu unatengua uwaziri wa watu wanne wakati wew ndio ulitoa go ahead....
Mtazamo tu....!
 
huyu jambazi nani atampa urais...

ni kwamba,wewe unaweza usimpe,lakini waendesha boda boda na marafiki zake,jamaa ndugu na majirani watafanya hivyo,unaweza usiamini kitakachotokea,lakini ndio siasa ilivyo kwani vyama vyote duniani malengo yake ni kushika dola na si kupaka wanja na kikawaida huwezi kusimamisha jiwe kama unahitaji kushika dola,ni lazima umsimamishe mtu mwenye uwezo na mvuto kwa jamii,ndani ya ccm E.L anao uwezo huo,akifuatiwa na Dr. magufuli,Dr.makyembe,lakini kama tutahitaji rais mwanamke basi mama Dr.migiro anaweza kusimamishwa
 
Back
Top Bottom