Lowasa aukana urais

Lowasa aukana urais

Mkuu, unamaanisha kwamba jamaa ni fisadi lakini anawajali wananchi kuliko kina Pinda anayejiita mtoto wa mkulima lakini hana jipya? Kama kweli fisadi Lowasa leo hii kaonekana malaika, pamoja na fedha chafu anazomwaga kwa wananchi na ambazo hazijulikana kazipataje, hiki ni kiashiria tosha kwamba kweli CCM wameishiwa viongozi....kuna ombwe kubwa sana la viongozi ndani ya CCM!!!!

Mkuu mbona umeeelezea vizuri kuliko hata mimi!! Yani ndio nilichotaka kusema. Marekebisho madogo tu, naona umezidisha chumvi kusema tunamwona malaika. Hakuna malaika, tunajua ni fisadi lakini pia ni kichwa he is an intelligent man. Kuna viongozi CCM hata danguro huwezi kuwapa waendeshe lakini lowasa unampa kampuni yako huku ukijua pamoja kuwa utaibiwa lakini faida utaiona na kampuni haitakufa sababu ni mtu mwenye PRIDE na ni mwenye chongo kati ya vipofu!
 
Unaposema Watanzania wengi wanamkubali, una ushahidi?? Maana hata hapa JF tukipiga kura sidhani kama tunaweza kupata hayo matokeo unayoyakadiria!! Hizo pesa za marafiki zake anazozigawa hovyo hovyo ndizo zitampeleka choonini 2015!!
Nilikuwa nahesabu kura kwa sample ya watanzania waliochangia uzi huu tu,naona jamaa amepita! Lakini bado najiuliza endapo jamaa alikuwa ameonewa kuhusu dili la kifisadi la Richmond ambalo bila shaka limeigharimu sana serikali yetu na lilisababisha kibarua cha jamaa(uwaziri mkuu) kiote nyasi.
Pia kwamba inakuaje mtu aliyeliingiza taifa kwenye matatizo makubwa katika cheo cha ngazi za chini(Waziri mkuu) apewe ukuu wa nchi; unaonaje?
 
ni kwamba,wewe unaweza usimpe,lakini waendesha boda boda na marafiki zake,jamaa ndugu na majirani watafanya hivyo,unaweza usiamini kitakachotokea,lakini ndio siasa ilivyo kwani vyama vyote duniani malengo yake ni kushika dola na si kupaka wanja na kikawaida huwezi kusimamisha jiwe kama unahitaji kushika dola,ni lazima umsimamishe mtu mwenye uwezo na mvuto kwa jamii,ndani ya ccm E.L anao uwezo huo,akifuatiwa na Dr. magufuli,Dr.makyembe,lakini kama tutahitaji rais mwanamke basi mama Dr.migiro anaweza kusimamishwa

Umeongea vizuri.lakini umekosea mkyembe na magufuli hawafai.hawa hawafikiri taratibu.watasababisha vita.Anatakiwa Raisi mwenye uwezo wa kufikiri na kutafakari siyo yule anayereact react kwa kutumia media.Kikwete namkubali sana anavyohandle mambo bila papara hata ingekuww issue kubwa namana gani.nimemkubali issue ya kagame na Joyce banda. Angekuwa mwakyembe au magufuli migogoro hii miwili ingekuwa mikubwa sana. Hata migiro hana sifa ya Uraisi ila ubunge anafaa.Huyu Slaa anafaa ila naye anatakiwa apate washauri wazuri sana.
 
Kufikiria kuwa Lowasa atakuwa ni rais ajae wa JMT ni kukosa fikra kwasbb 2015 urais wa JMT ni zamu yetu Wazanzibari. Vinginevyo, ikiwa kwamba ndo mnampenda sana na ni lazima akuongozeni basi mfikirieni kwa urais wa Tanganyika. Angalau serekali tatu zitakundoleeni kiu yenu ya kutaka kutawaliwa na E.Lowasa.
Ombeni sana dua rasimu ya katiba ipite ikiridhia serekali tatu.
 
Kuna jamaa yangu aliwai nimbia msemo huu.."kila kiongozi umuonae madarakani anareflect akili za jamii husika "
Ukiona jamii inamuita mtu mwizi at the same time wanasema huyu ndio anafaa kutuongoza nafikiri hapo unapata picha akili za hiyo jamii zikoje.
Kashfa za ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi yalipelekea EL ajiuzulu lakini leo hii anaitwa PM mstaafu ili kupunguza makali ya kashfa zake.
Sa hivi kajua akili za jamii anayotaka kuitawa ipoje anachofanya anamwaga tu hela afu anasikilizia pembeni...watu weeee raisi raisi raisi
Ni vizuri kwasababu siasa ni vita cha msigi mtu ashinde ila ni kweli kabisa watanzania tumekuwa wepesi kiasi hiki.
Kweli kweli huyu jamaa leo hii ndio anaonekana lulu..mwenye utajiri husiojulikana source mwenye kumwaga hela bila kujali atazirudisha vipi..duh

Ndugu yangu, akili za wadanganyika ni kama za walevi wa gongo…utakumbuka ni juzi tu kodi ya laini za simu (simcard tax) imehamishwa halafu wakadanganywa kwamba eti kodi IMEFUTWA wakakubali na kuanza kukenua mimeno kama mazuzu…kimsingi kodi haijafutwa ila imehamishwa kutoka mkono wa kushoto na kuwekwa mkono wa kulia wa mtu huyo huyo (mvujajasho). Mtu hawezi kukuhamishia mzigo kutoka kichwani akauweka mgongoni na kukudanganya kwamba ameutua halafu wewe ukakubali kama zuzu!

Serikali yahamisha kodi ya simu - Kitaifa - mwananchi.co.tz


Upungufu na uzezeta wa akili za wapiga kura wa Tanzania ndio uliotufikisha hapa. Utadhani watanganyika wanavuta bangi. Wanalalamika kuhusu ufisadi lakini ikifika kipindi cha uchaguzi wanakubali kuhongwa fulana, ubwabwa na gongo, wanatoa kura za kishindo kwa mafisadi. Nchi hii imeishalaaniwa kitambo. Tukiwa na wapiga kura wenye akili za kuku na wenye njaa kama hawa sidhani kama tutafika.

maisha bora,.jpg

Edward Lowasa.jpg
 
haya sasa, bei ya umeme imepanda kwa 67% lakini mkumbuke kwamba huyo fisadi mnayemuunga mkono ndiye aliyetufikisha hapa kupitia ufisadi wake wa Richmond LLC. Msiwe wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau.
 
kama mwizi mbona hawampeleki mahakamani bana, huwezi mwita mtu mwizi tu from no where...na kwa sabb wameshindwa kumpeleka mahakamani hiyo inathibitisha kuwa lowasa sio mwizi..na ndio mana watu tuna imani naye..

ukiangalia kwa mapana yake kunzia serikali hadi wapinzani wote wezi tu!!!!!! kwani hujasikia huyo mbowe anakopesha chama chake hela na baadae anajilipa mamilioni zaidi? anaununua vifaa bya chama mwenyewe na chenji anawekandani..anafanya hayo kwa kushirikiana na watu wake wachache ndani ya cdm..hapo hajapewa wizara au uraisi itakuwaje?
kwa kifupi watanzania wengi hawajui tu kwamba siasa ni ajira na kwamba wanasiasa hawako kwa ajili ya wananchi bali kwa maslahi yao..mpka uelewe haya ndio utaelewa kuwa hakuna mwanasiasa msafi kizazi hiki

Nani wa kumpeleka kwa pilato wakati ni wale wale,yaani kesi ya nyani unampelekea ngedere si watasaidiana tu.
 
Back
Top Bottom